Kunani msimbazi?

senyagwa

Member
Joined
Jun 1, 2015
Posts
72
Reaction score
23
Jamani mi nasikia Mo Dewji kagoma kutoa pesa za usajili kisa Ni kukosa hati ya timu ya Simba ambayo inashikiliwa na Mzee Kilomoni. Na hiyo ndo iliyopelekea michakato ya kuwasajili baadhi ya wachezaji kama Ajib,Tuyisenge,Kahata,Bwalya, Kambole,etc imebaki kua tetesi maana huku vyura wananipa shida.Wadau ufafanuzi plz mwenye uhakika na hili. Povu ruksa!!!!
 
Ajib hawezi kucheza Simba tena na hata ikitokea karudi kwa baba yake Simba misimu sita ijayo atakaa benchi tu.

Alafu ishu ya Mo kutokutoa pesa ni maneno ya mtaani tu (Tetesi) Gor mahia fans wamethibitisha Kahata si mchezaji wao tena wenye chuki wanamponda na wenye kumpenda wanampongeza .
group lipo facebook na hadi linatambuliwa na Gor mahia Fc kwa sababu linaendesha mashindano ya kupata mashabiki wataolipiwa tikiti n.k na Gor mahia official page wana_share.
 
Kwa hiyo Dripboy unataka kusema je sasa .
Akiondoka Gormahia ndo kaja Simba.
Kwa mujibu wa mashabiki wa Gor ndivyo wanavyosema na kuna maji ya mdimu (tetesi) msimbazi kuwa Francis kahata atatua msimbazi
 
Tuliza mcheche ndg. Simba kwa sasa inafanya mambo yake kisayansi sio kwa mbwembwe na mihemko kama upande wa 2 mwisho wa siku mbwembwe na kuandikwa magazetini uwanjani sifuri.
 
Mkuu simba kwa sasa mambo yetu tunafanya kimyakimya kelele tumewaachia vyura...angalia hii,hii ni kabda hata timu ya taifa haijaenda egypt but tuliamua tu kukaa kimya
 
Mkuu simba kwa sasa mambo yetu tunafanya kimyakimya kelele tumewaachia vyura...angalia hii,hii ni kabda hata timu ya taifa haijaenda egypt but tuliamua tu kukaa kimyaView attachment 1123804
hata Yanga masimu ulopita walisema tunasajili kimyakimya baadae wakaibukia kwa Boban.Kiukweli kuna mkwamo ila wabongo wabishi kuelewa maana wanapenda timu kuliko mpira wenyewe
 
Duh kweli hii Kali,msimu huu mnasajili kwa kutumia Facebook?
 
hata Yanga masimu ulopita walisema tunasajili kimyakimya baadae wakaibukia kwa Boban.Kiukweli kuna mkwamo ila wabongo wabishi kuelewa maana wanapenda timu kuliko mpira wenyewe
Mkwamo gani mzee baba....nyinyi ndo mnataka kuwepo na mikwamo kitu ambacho hakipo...alafu mbona haya maswala mashabiki wa makwasukwasu wanatumia nguvu kubwa ku force ionekane na simba kuna matatizo kama wao....MTAPATA TABU SANA TULIENI DAWA IWAINGIE
 
Ko simba hawana kamati ya usajili / mtu anayesimamia usajili?
Maana naona mo mwenyewe ndo kashika karatasi za mkataba.
Kitu ambacho hutamwona tajiri yoyote wa timu akikifanya.
Kamati za usajili ni za wana Yanga, ngoja nikupe mfano Pale Barcelona kuna Abdal ni mkurugezi wa ufundi lakini anayemsainisha mchezaji ni Raisi wa Barcelona.
 
Kamati itoke wapi? Mikia mwenye pesa ni mtu mmoja. Akiugua, wote wanahaha
Hao wa kamati ya usajili ndo nini, acheni ushamba. Kazi ya kamati ni kutafuta mtu anayehitajika, kumsainisha sio kazi ya kamati ni kazi kiongozi mkuu wa klabu.
Labda nyie Yanga ndo mfumo wenu kamati ndo inamsajili mchezaji, sasa mstake hata wengine watumie mfumo huo.
 
Mkwamo gani mzee baba....nyinyi ndo mnataka kuwepo na mikwamo kitu ambacho hakipo...alafu mbona haya maswala mashabiki wa makwasukwasu wanatumia nguvu kubwa ku force ionekane na simba kuna matatizo kama wao....MTAPATA TABU SANA TULIENI DAWA IWAINGIE
We ushabiki mandazi unakusumbua.Simba na Yanga toka lini zikaanza kusajiri kimyakimya?Hakuna timu duniani inasajiri kimyakimya.
Kama unayo smartphone na ni msomi mzuri,ukienda instagram hata sasaivi au tweeter uone vitu Mo anapost utajuwa kuwa kuna vitu haviko sawa kwake na hasa mambo ya simba.

Mwakajana mlisajiri mapema kikosi kikajulikana mapema.Leo huo utaratibu gani mpya wa kimyakimya.

Subiri vuguvugu hili la msimbazi lipite ndio utaona usajiri ukifanyika nje na hapo basi wachezaji waliopo wanatosha kuivusha simba mwakani.sio lazima kusajiri kiviile.
 
Unasubiri mtafaruku eeeh....we ndo shabiki maandazi ambaye kila unachosikia mtaani na mitandaoni basi unaamini kweli...eti moodewji vitu anavyopost vinahusiana na simbaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚....we sikihizi umekuwa mtaalamu wa kuingia kichwani kwa watu na kutafsiri anachowaza???or wewe ni mpiga ramli mzee baba???...fisi kawaida siku zote akiona mtu anatembea huwa linafuata nyuma likiwa linajua eti mikono itadondoka...TULIENI DAWA IINGIE VIZURI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…