Rose Akombe ambaye alikuwa mmoja wa watumishi wa tume ya uchaguzi Kenya amejiuzulu rasmi na amekimbilia Marekani na kudai kunauwezekano uchaguzi wa marudio kutofanyika Kenya tarehe 26th October kutokana kujitoa kwa mmoja wa wagombeaji Raila Odinga.
Mrs Akombe aliyekuwa ameenda kikazi Dubai kukagua uchapishaji wa karatasi za kupiga ameeleza ameamua kukimbilia Marekani kwa kuhofia maisha yake baada ya kupokea vitisho kutoka kwa baadhi ya wanasiasa Kenya
Akombe aliyekuwa msaidizi mkuu wa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Chebukati anahodhi uraia wa nchi mbili Kenya na USA.
sources: BBC