Kundi la Choka Mbaya

Kundi la Choka Mbaya

Mtamile

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
2,838
Reaction score
1,274
WanaJF
Leo naomba tuzungumzie kidogo kundi la choka mbaya kwa walionza kusikiliza muziki wa bongo fleva miaka ya nyuma kidogo nazani watakuwa wanakumbuka kundi la choka Mbaya kwa haraka haraka nakumbuka lilikuwa likiundwa na kina Profesa Jay, Adili, Black Ryno na kina kipindi nazani hata Fid Q naye alikuwa Choka Mbaya (sina uhakika sana). Kwa sasa ukisikiliza nyimbo nyingi za profesa Jay mara nyingi utasikia neno "Amani kwa wanachoka"
1.Nataka msaada kidogo kwenu anayejua hasa members wote waliokuwa wanaunda kundi hili
2.Nataka kujua pia kama hili kundi bado lipo
3.Kwa anayeweza pia kuelezea hostoria ya hili kundi anaweza kutiririka

N:B kama umeanza kusikiliza mziki wa bongo fleva enzi diamond anahiti ni bora tu kuwa tu mfuatiliajo ili upate maarifa zaidi
 
Sidhani kama bado lipo hai maana sikuizi hata hawalizungumzii kama zamani... na huyo mdogo ake J nadhani sukuiz keshaacha mziki
 
Sidhani kama bado lipo hai maana sikuizi hata hawalizungumzii kama zamani... na huyo mdogo ake J nadhani sukuiz keshaacha mziki

Mkuu hivi kulikuwa ma memba wengine tofauti na hao wa juu
 
Sidhani kama bado lipo hai maana sikuizi hata hawalizungumzii kama zamani... na huyo mdogo ake J nadhani sukuiz keshaacha mziki

Black rhyno hajaacha muziki..Ana ngoma mpya yupo na the late ngwair.
 
Kuna wanao imba muziki kama kazi zao na pia wapo waliojaribu hivyo wakachemka wakaona bora waimbe tu for fun.. hao tutasema wameacha maana hata show hawana na waliamua kujiendeleza na sasa wanafanya kazi kutokana na elimu zao sio muziki.
 
Black rhyno hajaacha muziki..Ana ngoma mpya yupo na the late ngwair.

Ni kweli mkuu nimeupata huo wimbo unaitwa Lookie Lookie ila naona kaifanya pengine kiburudani zaidi na siyo Kibiashara
 
Babu Ayubu pia alikua mwana choka, Adili nadhani alijitoa mapema tu hivyo kundi likabaki na Jay pamoja na wadogo zake kama Simple X, Black Rhino, Dj Choka na Babu Ayubu. Lakini kama utakumbuka ni kua kundi hili halikuwahi kua kali kama makundi mengine ya ECT na TMK wanaume, Kundi hili lilikua ni kama wasanii walioshirikiana na Prof ktk nyimbo tu kama ilivyokua walume ndago chini ya Inspector Haroon.
 
Choka mbaya ipo haijakufa according to Jay ila memba wake wengi ni kama muziki wanafanya kama option nyingine mf simple x aka mzee wa ngano ni baba mtu kwa sasa , black rhino kaoa tangia mwaka juzi nae ana mtoto though anafanya ngoma mara chache, Adili alikua na chapakazi film , prof yupo kama kawa dj wao alikuwa bonge hivi nadhan ndio dj choka yupo.
 
Babu Ayubu pia alikua mwana choka, Adili nadhani alijitoa mapema tu hivyo kundi likabaki na Jay pamoja na wadogo zake kama Simple X, Black Rhino, Dj Choka na Babu Ayubu. Lakini kama utakumbuka ni kua kundi hili halikuwahi kua kali kama makundi mengine ya ECT na TMK wanaume, Kundi hili lilikua ni kama wasanii walioshirikiana na Prof ktk nyimbo tu kama ilivyokua walume ndago chini ya Inspector Haroon.

Ni kweli mkuu kuna makala moja nilikuwa naisoma Bongo5 ni ya 2006 ni ya Black Rhyno alikuwa anamlalamikia kaka yake Pr Jay kwamba kaka yao hawasadii chochote na kwamba amefikia hapo kwa juhudi zake na kulikuwa pia na Nyimbo ya kundi (choka mbaya) ilikuwa inafanyika Bongo record wote walikuwa wameshaingiza vocal akawa amebakia tu Pr Jay lakini akawa kama anazingua ikabidi waahirishe tu kufanya hiyo nyimbo nadhani toka hapo hawajafanya tena nyimbo
 
Vp kuhusu Terry, hakuwa mwanachoka?
Kuna mchizi alishilikishwa kwe ngoma ya Q chief-mwana mnyonge sijui ndo nani vile?
 
Vp kuhusu Terry, hakuwa mwanachoka?
Kuna mchizi alishilikishwa kwe ngoma ya Q chief-mwana mnyonge sijui ndo nani vile?

Nsumbanzunya ulimhola!!! Huyu Terry siyo kwamba yeye alikuwa ni member tu Hard Blasters Crew (H.B.C)
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom