Kunguni wanasababishwa na nini?

Kunguni wanasababishwa na nini?

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Mwenye kujua hili atujuze maana kuna kipindi fulani nyumbani kwetu kulijaa sana kunguni ila tukawaua. Sasa hivi hawapo; hebu tuambieni kunguni wanatokea wapi au wanasababishwa na nini?
 
Mimi nadhani kunguni wapo kama wadudu wengine. Unawapata kama umeenda kulala sehemu yenye kunguni then ukawabeba kupeleka kwenu.

Kuwa makini maana siku hizi kuna hadi mabasi yana kunguni, nyumba za wageni n.k. Na ukishamleta kwenu ndio basi tena. Utatumia nguvu nyingi sana kumuangamiza.

Tofauti na imani ya watu wengi kwamba kunguni ni uchafu. Lakini angalia kwenye baadhi ya vyuo. Unakuta block lina kunguni hadi vyumba vya madada, hivi kuna watu wasafi vyumbani mwao kama wadada wa vyuo?
 
uchafu, maisha yangu yote sikuwahi kumuona kunguni mpaka nilipofika high school nikaenda shule fulani watu walikuwa wachafu sana


Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kweli kunguni wanasababishwa na uchafu mfano chumba changu Ni kisafi lakini kulikuwa na kunguni pia nakumbuka nilienda kwenye Easter comference kwenye shule ya Kisarawe nililala chumba kilikuwa kisafi lakini kilikuwa na kunguni.
 
Kunguni anapenda mazingira machafu, rangi nyeusi, nyekundu na brown, Giza, sehemu isiyoingiza mwanga wa jua vizuri na sehemu mtu sio msafi, apo Kunguni hatoki.

Kunguni hapendi mazingira haya yenye mwanga wa taa nyeupe(energy saver), hapendi kuta zenye rangi ya njano na kijani, hapendi godoro lenye kava ya plastic, hapendi godoro lenye rangi njano/kijani, hapendi alufu za pafyumu, hapendi vitanda vya chuma kwa sababu vinaptisha baridi, sehemu ambazo wanapuliza airfresh hawezi kukaaa kabisa ni hayo.

Hii ni Research ya range management and tsetsefly

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna watu nawaonaga hawafikiri kama wanaosema kunguni wanasababishwa na uchafu. Kunguni wanakaa hata kwenye vitanda vya Hilton Hotel sasa vitanda vya Hilton Hotel na chako cha geto chepi kisafi.

Sababu ya kunguni ni kuletwa na mtu aliyembebeba kutoka palipo na kunguni watazaliana mpaka watajaa...njia pekee yakuwaondosha ni sumu ya wadudu kama LAVA basi.
 
Kunguni wanaishi nasi. Kunguni ni msafiri anasafirishwa na binadamu toka eneo moja kwenda eneo jingine.

Kunguni anapatikana katika mazingira machafu ndiko huzaliana kwa wingi, binadamu atambeba toka saluni, kwenye mabus , hotelini nk.

Utamfikisha, ofisini au nyumbani ambako ataanzisha makao mapya . Kwangu niliwahi kumkaribisha mgeni huyu, kupitia JAMVI la kusukwa kienyeji nililonunua.

Kunguni mijini ni wachache ukilinganisha na vijijini kutokana na mazingira yao. Haikwepeki kunguni ni sehemu ya uchafu. Akibainika sehemu Safi anashambuliwa na kuisha kwa dawa rasmi za viwandani na za kubuni Kama sabuni OMO au AERIAL
 
Ni shule ya Advanced Level
Kama walikua girls tu probably inawezekana...lakini ukifananisha na wanaume aiseeh sisi tukiwa shuleni tuko rough sana.

Kwanza u-rough wetu unaanzia mwilini then kwenye mazingira.

Lakini mabinti wa chuo wako very smart kuanzia mwili hadi mazingira wanayolala.. na bado kama kunguni unakuwa wanakuwa nazo tu.
 
Back
Top Bottom