Kunji Katika Chuo Kikuu cha Ohio

Filipo Lubua

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2011
Posts
339
Reaction score
578
Wale wanaofikiri kunji ziko Bongo tu, wanakosea. Ziko mpaka katika Vyuo vikuu vya Marekani. Wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Ohio walikamatwa na Polisi kwa kuvamia kikao cha Bodi ya Wadhamini (ambacho kina mamlaka ya kupandisha ada ya chuo) kupinga ongezeko la asilimia 1 katika ada kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza. Walivamia mkutano huo baada ya tukio lingine la Jumanne, walipoandamana kupinga ongezeko hilo.

Walivamia mkutano huo wakiwa na bango lenye maandishi: ELIMU SI BIDHAA, WANAFUNZI SI WATEJA.

Bila hofu waliingia kikaoni hapo, wakubwa wa chuo wakajaribu kuwabembeleza watoke ila wakakataa. Hata polisi walipofika, hawakuwagusa hata kidogo bali walisimama tu kuwatazama na kuwabembeleza watoke nje. Hata hivyo walipotoka nje walikataa kuondoka eneo la mkutano hadi pale polisi walipowaamuru. Wanne miongoni mwao (wasichana)walikataa kuondoka na ndipo walipokamatwa kwa kosa la kuingilia/kuvurua mkutano halali wa Bodi ya Wadhamini.

Nimeupenda ujasiri wa wanafunzi hawa, ila pia nimependa weledi wa askari polisi katika kuwakamata na kuwatoa wanafunzi hawa. Ikiwa jeshi letu la polisi lingejua haki waliyo nayo wananchi, haki ya kutoa maoni, haki ya kuandamana na haki ya kuonyesha hisia zao katika maswala mbalimbali, basi nchi yetu ingekuwa na amani. Tazama video hiyo hapo chini:
 
Last edited by a moderator:
Nimeipenda kwa kweli,ingekuwa ni kwa hawa askari wetu ambao hawana vichwa,tungesimulia mengine.
 
Hapo kwenye RED umenikumbusha mbali sana mkuu wangu!! MSUASO nini?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…