Kunock kwa injini 7A.

swamila

Senior Member
Joined
Apr 4, 2015
Posts
176
Reaction score
81
Wanajamvi naomba msaada gari langu aina ya premio old model injini yake ni 7A ilikuwa inatoa moshi mwingi nikikanyaga moto moshi mwingi sana nikaenda kwa fundi kaniambia ring piston nikabadilisha tatizo la moshi likaisha ila tatizo jingine likajitokeza la gari kukoshwa nguvu kwenye mlima gari halipandi nikamshirikisha fundi tena kaniambia injini imenock halivyosema tu hivyo nikakata simu. Sikutaka kujua tena maana ya injini kunock naomba msaada maana ya injini kunock.
 
Pole mkuu, Maelezo yako hayajitosheleza.
Walk us kwenye previous mechanics zilizo fanyika kwenye gari yako.
Alikuambia ring zimekwisha okay, ulinunua nini na nini kwa ajili ya hii kitu.
Tukijua haya ndio itakua rahisi kukusaidia.
 
Kupoteza nguvu kwa gari wala siyo Engine ku-Knock...

Engine kun-knock ni kwamba kuna piston/mikono zimepinda na engine haitoweza hata kuwaka...

Kubadilisha ring piston peke yake haitoshi, rudi kwa fundi akuchekie pia piston kama zipo vizuri na sleeve zake...


Cc: mahondaw
 
Mzee Engine kunock ni crank shaft au ile mikono inayoshikilia piston kupinda na ikitokea ivo gari haiwaki hata ufanyeje
 
Nimeipeleka tena kwa fundi lakini gari inawaka ila sasa kama nilivyosema kwenye milima ata mlima mdogo ni shida kupanda nimefika kwa fundi kashusha injini yote halafu akaniambia ni shaft imekufa
 
pole sana aisee , mpaka likae sawa, chamoto umekiona
 
Samahani mkuu Smart, utakuwa umechanganya kidogo, engine iki "seize" ndo haiwaki lakini knock huwa engine inawaka ila inakuwa inagonga .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…