Kununua Gari/Kukuza Biashara /Kujenga nyumba ya kupanga

Umechambua vyema mkuu.
 
Kopa 20m toa m12 nunua ht ist ikurahisishie maishaa
8m weka kwa biasharaa,simamia biashara vzr zaidi faida jengea vyumba vya kupangisha hapo unapoishi taratibu

Maisha mafupi hayaa usijistress sana woiii
Naam [emoji23][emoji23]
 
Umenifikirisha sana asante
 
Kopa 20m toa m12 nunua ht ist ikurahisishie maishaa
8m weka kwa biasharaa,simamia biashara vzr zaidi faida jengea vyumba vya kupangisha hapo unapoishi taratibu

Maisha mafupi hayaa usijistress sana woiii
Duh,
 
Ana mawazo mazuri lakini Million 20 haijengi nyumba. Itaishia kuwa pagala. Halafu kujenga nyumba unawekeza hela ndefu halafu returns zake kiduchu
 
Umemwambia ukweli ingawa watanzania huwa hatupendi kuambiwa hivyo. Ninavyojua mimi mtu mpaka uchukuwe mkopo, unakuwa umeshafanya upembuzi yakinifu usio na shaka na kujua mkopo wako mara unapouchukuwa tu unakwenda kuufanyia nini. Mimi huwa sishauri sana mtu aulize ushauri wa kuchukuwa mkopo sehemu kama hapa kwa sababu kufanikiwa kwa lengo la mkopo inategemea factors nyingi sana na hizo factors zinategemea mtu na mtu, mazingira husika na pia wakati etc. Ushauri utakaomsaidia Mrs A unaweza kabisa usimsaidie Mrs B japo unafanana. Cha msingi hapa achukuwe wazo la jumla tu na alifanyie kazi kulingana na mazingira yake. Na mwisho huwa naamini ukishaona mtu anataka kuchukuwa mkopo na hajui aufanyie nini au anapita huko na huko akiulizia aufanyie nini basi uwezekano wa kufeli ni mkubwa.
 
Huna mwazo ya kufanyia hiyo pesa so ghairisha kukopa mpaka mwakani.

Kopa mkopo wa biashara wa 5-7.5 M then ongezea kwenye biashara, after a year ukijirudishia hata 10M kutoka kwenye biashara na niashara ikawa imesimama vzr basi utakuwa na mawazo plus mtaji wa kuanzia inachowaza kufanya kabla ya kuchukua huo mkopo
 
Line ya mwisho imebeba ujumbe wote
 
Fanya kukopa huo wa kurudisha ndani ya miaka 6.


Cha muhimu usinunue gari kwa hiyo hela ya mkopo bali ifanyie biashara ikikulipa ndio utanunua gari huko mbele.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Kweli kabisa ila asikope huo mkopo wa kurudisha miaka 6
Badala yake akope wa kurudisha mwaka mmoja kisha apambane
 
1. USIKOPE
2.kama ni lazima kukopa usije ukanunua gari na wala usipeleke hela kwenye biashara ambayo teyari ina mil15 haijatengamaa
3. Mkopo maliza ndani ya mwaka 1
Siyo kwamba haijatengamaa
Ila ina mahitaji mengi, ni kama biashara ya hardware ina vitu vingi sana ambavyo unaweza kuuza so mpaka uwe na kila kitu inahitaji mtaji mrefu sana,

Kusema haijatengamaa ni kwamba kuna vitu naweza kuuza ila bado sina, ila biashara inaenda vizuri,
Kwa lugha rahisi nahitaji kuipanua zaidi niwe na kila kitu
 
Ana mawazo mazuri lakini Million 20 haijengi nyumba. Itaishia kuwa pagala. Halafu kujenga nyumba unawekeza hela ndefu halafu returns zake kiduchu
Inategemea na aina ya nyumba, mimi nina experience kidogo, milion 20 kwa eneo nililopo naweza kujenga sevant quarter nzuri kabisa ya kodi ya 250 hivi, au vyumba vya kawaida viwili au vitatu vya kodi ya 50-70 kwa mwezi
 
1. USIKOPE
2.kama ni lazima kukopa usije ukanunua gari na wala usipeleke hela kwenye biashara ambayo teyari ina mil15 haijatengamaa
3. Mkopo maliza ndani ya mwaka 1
Point 1&2 is taken
 
Napenda kuambiwa ukweli
Asante
 
Kama ni kuikuza unaweza ukope ila mkopo ulipe ndani ya mwaka
 

mhh hizi hesabu za bank gani bro??[emoji2298][emoji2298][emoji2298]

milioni 20 makato laki 9,kwa miezi 72!!!!serious

ukikatwa laki 9 maana yake mkopo ndani ya miezi 28 tu umekwisha mpaka riba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…