Kununua Gari/Kukuza Biashara /Kujenga nyumba ya kupanga

Chukua 15M ingiza yote kwenye hio biashara yako ya awali, Ustapanye hela baada ya mwaka utakua na uwezo wa kununua gari na mkopo utakua umeurejesha wote.Kumbuka jinsi mkopo unavyochukua muda mrefu kurejesha ndivyo na riba yake inavyokua iko juu.
 
mhh hizi hesabu za bank gani bro??[emoji2298][emoji2298][emoji2298]

milioni 20 makato laki 9,kwa miezi 72!!!!serious

ukikatwa laki 9 maana yake mkopo ndani ya miezi 28 tu umekwisha mpaka riba.
Niko serious..acha kubisha..huo ni mkopo wa miaka 6 kama alivyosema hapo..mkopo wa mwaka mmoja ni kwa ajili ya wafanyabiashara..na ndio maana nimemshauri achukue huo wa biashara. Mkopo wa watumishi ukiungalia kwa macho ya kawaida unauona nafuu lakini sio..ni wizi mkubwa.
 
Chukua 15M ingiza yote kwenye hio biashara yako ya awali, Ustapanye hela baada ya mwaka utakua na uwezo wa kununua gari na mkopo utakua umeurejesha wote.Kumbuka jinsi mkopo unavyochukua muda mrefu kurejesha ndivyo na riba yake inavyokua iko juu.
Uko sahihi..huo mstari uliomalizia kuna mtu amenibishia hapo juu.
 

kama ni miaka 6,kiasi + riba= ndicho kitaamua makato.

kwa hesabu za haraka hapo inakuja kama 29ml hivi/kwa miezi 72 ni laki nne kwa mwezi makato.
sasa marejesho ya milioni 11000000,kwa mwaka mmoja kibiashara unajua yanakaaje mkuu!!!hatujui biashara yake inaendaje.
 
Uko sahihi..huo mstari uliomalizia kuna mtu amenibishia hapo juu.

riba inavyozidi kuwa kubwa ndivyo makato yanazidi kupungua.

makato yakiwa makubwa muda unapungua na riba pia.
 
Dada kama unakiwanja Jenga, kama huna Kiwanja Nunua kea hiyo hela

Kama unaanza nayo biashara ACHA
Gari Usinunue ila maamuzi ni yako

Kama una kiwanja Jenga nyumba ya Kuishi uachane na Kodi.

Mwisho maisha ni ya kwako KUPANGA NI KICHAGUA
 
Dah...Acha ujinga...nyumba uijenge kwa mkopo wa miaka 6? Chukua pesa kidogo hapo...kale maisha kwanza...akili ikae vizuri..Raha jipe mwenyewe... Kisha ukirudi chukua calculator....Chukua mkopo kisha gawanya kwa kiasi ulichokula maisha ...utapata idadi ya siku zilizobaki kula maisha....halafu chukua hizo siku ...gawanya kwa 365 kisha gawanya tena kwa 6 kisha zidisha kwa 100...utapata asilimia ya siku za kula maisha ndani ya miaka 6 ijayo...namba hazidanganyi ,,[emoji2960][emoji482]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani nimesoma huku nacheka....hhahahahaha.....ww akili yako unaijua mwenyewe🀣🀣🀣
 
1. Kopa mkopo wa muda mfupi mwaka mmoja. Mana 15m riba kwa mwaka ni kama m1.5 ukikopa miaka miwili riba itakuwa 3m nk nk.

2. Mkopo wako wa kwanza wote uweke kwenye biashara, hiyo biashara ni biashara gani, biashara mara zote hazishibi ni Ubuntu tu, mfano unaweza kuongeza uwakala wa pesa za mtandaoni tigopesa nk.

3. Pesa yote izungushe kwenye kukuza mtaji.

4. Mwaka unaofuata kopa tena kipindi cha mwaka mmoja tena, nunua gari na kiwanja kilichosehemu ambayo utajenga nyumba yako na upande unaweza kupangisha.

Karibu
 
Kopa million ishirini then nunua bajaj used za million 3-4.5 nunua 4 then hela inayobaki funga track kila bajaji tafuta madereva wakupe 150k kwa week ndani ya mwezi mmoja una 2-2.4m hapo una uhakika kila siku kuingiza 100k....
Kuwa mpole na mnyenyekevu kwa mwaka mmoja 2m-2.4m mara 12 unacheza million 24-28 sasa una jeuri ya kufanya lolote lile..

Kwa mfano ukiwa na bajaj nne za million 4.5 zitakupa million 4-4.8 ndani ya miezi 2 hivyo unaweza kuongeza bajaj ya 5.Ukiwa na bajaj 5 zinakupa hadi million 3 kwa mwezi hivyo ndani ya miezi miwili unaongeza tena bajaj 1.

Zikifika 6 sasa una jeuri kubwa sana 25000 mara 6 bajaj mara 26siku ni 3,900,000 kwa mwezi punguzA tuseme unapata million 3.

Anza kulipa deni kwa vurugu kubwa sana kama kwenye mshahara unakatwa laki 7 basi ongeza million 3 kwa mwezi lipa deni 3.7million ni miezi sita tu inakutosha kumaliza deni max miezi 7.

Usimamizi tafuta kijana mwenye bajaji anayekaa kijiwe cha bajaji mpe 200k kwa mwezi kusimamia bajaji zako kijiweni hapo siku za kazi ila siku za service uwepo na zifanywe na fundi mmoja....

Track inakusaidia pia kujua vyombo vyako vipo wapi na vinafanya nini


Turudi kwenye nyumba nzuri ya million 30 na assume umekopa 20 na million 10 unazo.Utaipangisha kwa laki 4 bei ambazo ni common tuseme upo mjini dar au arusha.Nikinunua pikipiki used tu za million 1.5 ziwe 3 ni 4.5million.Pikipiki moja inanipa max 200k kwa mwezi zikiwa tatu ni 600k tuseme zinanipa 400k sio 600k.

Kwahiyo wewe na nyumba yako ya million 30 unaingiza pesa sawa na mwenye pikipiki tatu used za 4.5million.

Kuwa makini na kuzika hela.
 
Fanya kukopa huo wa kurudisha ndani ya miaka 6.

Cha muhimu usinunue gari kwa hiyo hela ya mkopo bali ifanyie biashara ikikulipa ndio utanunua gari huko mbele.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Hujui hesabu kabisa bro. Watu wanalilia mikopo ya biashara ya muda mfupi wewe unamshauri akope salaried loan, mkopo wa mshahara hio mil 20 atarudisha si chini ya mil 50.

Mimi najua wewe mleta uzi unataka vyote. Unataka biashara nyingine na unataka gari. Sasa maisha ni mafupi sana ipe roho yako raha ukingali hai lakini kwa hesabu kali sana.

Kwakuwa una biashara inayofikia mil 15 tayari hii inakuinguzia kipato bila shaka. Bado mshahara una maana upo wa kutosha haujakopewa. Chukua mil 15 ya mkopo wa biashara ila hii hauwezi kujenga utafeli labda kama unajenga kupangisha nyumba simple sana, itatosha. Yan unalenga vyumba vya kupangisha elfu 50, then vyumba simple hio mil 15 utapata vyumba viwili self-contained. (Nakwambia nilichowahi fanya) sioti.

Lakini waweza tafta biashara nyingine tu kwa hiyo mil 15, ukawekeza mil 10. Alafu mil 5 ukanunua gari ili uwe navyo vyote. Siku hizi mil 5 kupata gari ni kawaida sana.

Lakini kuhusu gari kuna makampuni saizi unatoa nusu, wanakupa toka japan nusu unamaliza taratibu mwaka mzima. Lakini njia hii ya pili itakutesa maana utakuwa na mikopo miwili. Japo malipo ya gari waweza kuyabebesha kwenye mshahara.
 
Ni kweli bro ndio maana nimesema mimi sio mtaalamu wa hayo mambo na nafurahi mtaalamu umefafanua. Vizuri. πŸ˜‚
 
Makato hayafiki laki9 kwa 20m
 
Mimi ningekushauri Usikope Bank...
Kama unaweza katwa let say laki5 kwa kila mwezi kwa miezi 60 nn kinakushinda kuhifadhi iyo laki 5 walau kwa mwaka 1 alafu ukafanya jambo Lako. ..hakuna faida yyte unayopata ukikopa bank sana sana unawafaidisha wao. ..bora uwekeze pesa yako hata ukipata hasara haiwi hasarA mara2
 
Mbona simpo tu. Hakuna investment nzuri kama REAL ESTATE. Chukua 20m bank kwa marejesho ya 6yrs. Hakikisha inaiwekeza ktk ujenzi kikamilifu. Kama ni kujenga vi-apartment vya kibachelor unapata viwili. (Chumba, sebule, choo). Hapo unapata wastani wa kodi 150k kwa mwezi. Meaning ndani ya mwaka unaingiza 1.8m kwa kila moja. 3.6m kwa zote mbili. Hata mshahara wako ukikatwa bado una uwezo wa kusurvive kibingwa huwezi.kupotea sana kiivyo.
Pia komaa na biashara uliyonayo iendelee kusimama ili baada ya muda uone mwelekeo wake. Maana biashara nazo tatizo kubwa ni usimamizi.
Ni hayo tu.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hapa nadhani ushauri kila mtu ataangalia chenye manufaa kwake....muhimu sasa za kuambiwa changanya na zako.
 
Agiza gari Japan Nissan xtrail unalipa nusu nyingine unalipa kidogokidogo kupitia mshahara kata bima kubwa ya kibabe baada ya miezi minne hiyo gar itaibiwa na kukatwa spea unavuta mkwanja wako toka kwa wapemba wa ilala unahangaika na watu wa bima pamoja na waliokukopesha mwishowe watakupa gari nyingine na maisha yataenda km hakuna kilichotokea kikubwa zaid usikurupuke kwenye mambo haya lazima ujue namna ya kucheza kwa sabab michezo hii wanaokukopesha na watu wa bima wanaijua vzr kwa sabab na wao wanaifanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…