Kununua Gari/Kukuza Biashara /Kujenga nyumba ya kupanga

Mimi nipo tofauti na wote,nimefatilis comments zako unapo wajibu wadau inaonekana Biashara yako ipo vizuri tatizo in mtaji na supervision.

Huu ushauri ungekuwa mwanaume ungekufaa zaidi ila kwa vile ni KE sijui hata kama utaufikiria maana wanawake ni waoga kuchukua maamuzi.

Kwanza, Chukua mikopo yote ambapo utakuwa na jumla ya 35M weka kwenye Biashara yako 10M inayobaki 25 nunua bajaji 3ambazo zitakupa 900K-1M kwa mwezi utatumia haya kufanya marejesho ya 15M uliyokopa.

Pili,Acha kazi kasimamie Biashara yako hiyo uliyoweka 10M.pia utapata muda wa kusimamia na hizo bajaji.Baada ya kuacha kazwaone watu wa Bank pale ulipokopa Mkopo wa utumishi vunja Mkataba wambie muingie Mkataba wa kulipa Mkopo ndani ya mwaka 1 utatumia mapato ambayo unayapata dukani kulipa hilo deni.Baada ya mwaka tu utanunua gari uipendayo na kuanza ujenzi wa nyumba ya kupangisha.
 
Yaani una biashara ya mtaji wa mil.15 unakopa 20 maana yake kama ukiinject yote inakuwa mil.35 afu bado unapanda boda usafiri wenye risk kubwa hivyo?.
Acha ubahili. Toa mil. 10 nunua gari ya economy ya mafuta. Tumia kufuatilia biashara hiyo. Hizo mil. 10 boresha hiyo biashara inayosuasua. Katika huo mshahara baada ya makato ya mkopo naamini hutaweza kukosa hela ya service ya gari.
Aidha kama umeshatathimini hiyo biashara uliyokwisha wekeza mwanzo ina return nzuri iboreshe ili kuikuza zaidi. Kama haifanyi sawa buni biashara nyingine (diversification).

Kwa sasa ujenzi wa nyumba ambaye inaweza kukuletea marejesho mazuri ni ghali kwa sasa hiyo 20 mil. haitoshi.

Zaidi ya yote wewe mwenyewe ndiye unayejua life standards zako ulizojiwekea mwingine kuwa na gari ni moja ya basic need yake mwingine ni luckshary. Nadhani umenielewa.
Usikope mkopo wa 15 mil. Nguvu kubwa itatumika katika kufanya marejesho unless hiyo biashara iwe inafanya vizuri monthly.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚uko vizuri Mkuu πŸ€›πŸΎ
Fanya kukopa huo wa kurudisha ndani ya miaka 6.

Cha muhimu usinunue gari kwa hiyo hela ya mkopo bali ifanyie biashara ikikulipa ndio utanunua gari huko mbele.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Mkuu under normal circumstance.milioni ishirini inatakiwa izalishe sh. Ngapi kwa mwaka.
Kama bank inakata 60 miaka sita basi hio hela inatakiwa iwe imezalisha pesa nyingi sana.
 
Mkuu umetumia kanuni gani ya biashara ya kula mtaji badala ya faida?
 
Huo wa mwaka mmoja utaulipa kupitia biashara au salary slip?
Una umri gani?
Umeolewa?
Kwa maelezo yako ni kama umejenga unaishi kwako.
Nipe majibu ili niweze kukushauri
Kwa nini nichukue mkopo wa miaka 6 na si mwaka mmoja, naomba sababu ya kiuchumi hapa mkuu
 
Makampuni gani hayo yanakopesha magari naomba contacts tafadhali.
 
Hahahhaa aisee nahisi kwa sababu tu si mwanaume labda siwezi kufanya lolote kati ya uliyosema

Paragraph one upo sahihi
 
Sasa nani ataiba hahahaha nimecheka kama chizi

Mimi siwezi hayo mambo
 
Kwa maoni yangu .

Kuhusu mikopo
Lazima kwanza hiyo 20m ( mkopo wa mwajiriwa ) una riba kiasi gani
Na hii itakusaidia kufahamu unalipa tsh baada ya muda wa mkopo wako.
Pia
Kwenye huo mkopo wa biashara unariba kiasi gani ?

Ukishajua una lipa kiasi gani baada ya maturing ya hiyo mikopo
( Kama ipo reasonable naomba nikupe ushauri wa kutumia hiuo pesa yako ya mkopo )

Kwenye 20mil
Tafuta bajaji tatu ( 3) used zenye afya zenye gharama ya 3.5-4 million kwa kila bajaji ( 3.5m*3= 10.5mil ) kwenye pesa yako utabaki na 9.5 mil
( 9.5 mil unaweza kupata gari used nzuri Kama mpya )
Au la sio nunua Uber πŸ˜‚πŸ˜ƒ
Hii itakusaidia kwenye safari zako lakini pia itakuingizia pesa
Uber inapay 35000-40000 kwa siku ( so hapa kuna pesa pia unaweza pata )

Kwenye bajaji tatu kwa miezi 10 utapata
( 3*25*30*10=22,500,000 )

Lazima ujue hzo pesa utazipata baada ya usimamizi mzuri wa pesa yako na Mali zako .


Kwa upande wa 15mil
Tumia 8-10 mil uwekeze kwenye biashara yako unayoifanya sasa, pesa inayobaki weka pembeni Kama miscellaneous uses itakusaidia pale penye tatzo

Lakini pia hapa pia unaweza ukanunua pikipiki hata mbili za kuongea pesa yako
(Usimamizi mzuri ni muhimu sana )
 
Nitarudi hapa soon
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji2] apa ulitupeleka chaka afisa mikopo BRN yaan apo na riba jumla haizidi milioni 30. Marejesho ni 400k na sehem kidogo for 6yrs
 
Mambo haya
 
Wengi wamekazana kwenye nyumba na biashara, lakin hawajui biashara nayo inafeli.

Lakini kwa maoni yangu kopa acha ela ambayo utakula na kulipia bills za mwez zima, mf kama mshahara wako laki 9 baada ya makato kopea laki nne ibaki laki tano kwa ajili ya familia.

Thn fanya jambo ulilo kusudia, kama gari nunua, kama nyumba jenga japo nyumba ujenz hauishi.

Asikutishe mtu wapo walio kopa wakafanya biashara wKafilisika na alie jenga wakapata majanga ya kubomolewa na gar kuibiwa au kuungua.

Kikubwa fanya kitu moyo wako unapenda 75% ya watumishi magar yako wamekopa na hata nyumba na biashara pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…