Kwani wewe unataka kufanya nini? Ungetuambia unataka kurudisha au hutaki basi tukushauri.
Je wewe unagari lako mwenyewe? Je rafiki yako hivyo sana hadi unakosa usingizi na kuuliza humu? Kama hamna urafiki ule wa sana unajua sana as naona ungemkopa kama mngekuwa karibu hivyo bila yeye kuuza gari.
Jua huyo kashauriwa na mtu/watu aje aombe gari lake. Pia labda alijua atakufanyia hivi yaani mchezo huu usimwamini.
Sasa pia unaweza test urafiki wenu mwambie nduguyo kalinunua toka kwako yupo mkoa mwingine, hapo utamsikia.
Ila kuwa makini na watu wa namna hii, usi trust mtu sana katika urafiki. Kwa hiyo kuanzia sasa mwangalie. Usipompa anaweza kukuibia gari, au kuwapa tipu majambazi basi tu mkose wote.
Pole nakuonea huruma as lazima ulishapangia kitu hilo gari, labda ndio lako moja kwa sasa. Mwingine ameshauri uende jukwaa la sheria ushauriwe.
Tujibu tuzidi kukusaidia.