Mkuu,
Nadhani waliojadili hapo juu wengine wapo sawa wengine wamechanganya habari. Hisa maana yake ni kununua umiliki katika kampuni kwa kiasi fulani. Maana nyingine unakuwa mmoja wa wamiliki, kutokana na ukubwa wako wa share. Kama kampuni ina share 100, na wewe unamiliki 10 maana yake wewe una own 10% ya ile kampuni. Faida ni kwamba wewe unahusika katika maamuzi ya kuchagua mkurugenzi mkuu, na mambo mengine kutegemeana na sheria na kanuni za share yako. Vile vile kumbuka ya kwamba kama kampuni inapata hasara na wewe unapata usara, lakini share zako zinabaki vile vile quantity, ila bei yake nitazungumzia badae.
Kampuni inapokwenda kujiandikisha ikapewa certificate of incorporated, inaruhusiwa kuhuza share kadhaa. Let say TBL wameruhusiwa kuuza share 100,000 (huu ni mfano). Maana ya kwamba TBL maximum number of shares wanazo weza kuuza ni 100,000 wakitaka zaidi inabidi warudi kwa serikali and other procidure zifanyike (beyond the scope of this explaination). Sasa TBL wakisha kubaliwa kwamba wao wata issue 100,000, then wao wanakaa chini na kuamua labda wanauza only 50,000 kwa sasa. Na hamsini watauza badae..... So, TBL wataweka bei share ambao wao wanaamini ni fair kutokana na asset, earnings na mambo mengine. Kisha wanauza kwa primary buyers, then hawa primary buyers ndio wanakuja kuuza kwa sekondary buyers kama mimi na wewe pale DSE.
Mmiliki wa share anapata faida kwa njia mbili, kwanza kwa kupanda kwa share yake sababu ya demand and supply forces. Maana chukulia wewe umechukua shares 100 za TBL kwa shili 50 kwa shares mwaka 1998, mwaka 2000 demand ya shares za TBL imekwenda juu na soko lime determine price ni 70 TSh, wewe ukaamua kuuza nusu ya share zako 50 maana ni kwamba umepata faida ya shilingi ishirini kwa share. Kitaalamu tunaita Capital Gain.
Njia ya pili ni pale kampuni inapopata faida, CEO na uongozi wa kampuni unaweza kuamua kwamba kiasi fulani cha faida zinagawiwa. na hapa ndio wengine wamepazungumzia, hii ni dividend payout. Maana ule mfano wetu wa TBL kama wana share 50,000 kwenye market (outstanding), na wanataka kugawa dividend kiasi cha shillingi 50,000 then kila share itapata 1 shilling (50,000/50,000) dividend. Sasa wewe kama una share 100, utapata shilling 100. Hii ni mara moja kwa mwaka, na ugawiwa only kampuni ikiwa imetengeneza faida na baada ya kulipa TAX.
Nimezungumzia faida tuu, lakini kumbuka hasara ni pamoja na share kuanguka vibaya kwenye soko. Maana less demand with high supply. Nadhani mfano kama Tanzania Oxygen walivyo issue share zao mwanzoni kabisa.
Soko la share la Tanzania bado linasafari ndefu sana.... Nimeshawai kuandika huko zamani kwenye gazeti mmoja la biashara hapo nchini kuhusu share. Nitaitafuta ile article na kuiweka hapa.