Kununua share au Fixed Account?

Mayu

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2010
Posts
7,621
Reaction score
12,505
Wakuu nina pesa kama millioni 100 kwasasa sina mpango nayo kuifanyia chochote hadi baada ya miaka miwili

Naomba ushauri wenu kati ya kununua share na baada ya miaka miwili nije niziuze au niweke fixed acc niwe napata gawio kila mwezi?

Pili je ni bank gani wanatoa rate nzuri fixed acc? Na je Hisa si zinaweza kishuka ikawa hasara? Na mgawo wa faida ya hisa ni kila baada ya muda gani?

Sihitaji ushauri wa biashara yoyote baada ya masahibu nisije nikapoteza hela yote bure, nahitaji miaka 2 nitulie
Naombeni mwanga kabla sijaenda kwa wahusika
 
Mayu, Mbii?

Fixed account. Tanzania Postal Bank walikuwa na interest nzuri 12% kama sijakosea ya miaka miwili. Sijui kama bado wanaendelea. Utakatwa withholding tax lakini nafikiri ni 10%.

Hisa ni pata potea.
 
Mkuu kama umeshasema kwenye hisa kuna hasara basi achana napo...wewe tia mpunga kwenye fixed deposit
 
Mkuu kawekeze kwenye government bond, haziongopi zile
Itategemea ameamkaje,
Na huna la kumfanya Wala hutoweza kufungua Kesi popote kudai chako.

Maana kwa mswada mpya,
hairuhusiwi kwa mwananchi wa kawaida kuifungulia mashtaka serikali yako isipokua mamlaka hayo kapewa MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI.

Jiulize Sasa,
inawezekana vipi MWANASHERIA mkuu wa serikali asimame upande WAKO kuishitaki serikali inayomlipa yeye mshahara?

Kwa kifupi, HAIWEZEKANI.

Binafsi naona
Kuwekeza huko kwa hali ya Sasa nako Ni Kama kucheza tu KAMARI.
 
Kwenye hiyo milioni 100 toa 10m kawekeze kwenye crypto kama vile ethereum & bitcoi
 
Nafikiri weka on Govt bonds za 20 year upate 15% annually au unaweza kugawa, some ukanunua hisa za makampuni yanayoeleweka. Ila bora umtafute mshauri wa masuala ya kifedha kwanza ili akushauri vizuri.
 
Kwa Tanzania ni Bora Bora ukaweka izo pesa kwy Fixed account tuuu, izi Shares, Bond and Treasury Bills bado Kwa Tanzania hazina uelekeo muhimu
 
Nunua hatifungani za serikali, hazina mambo mengi, riba kubwa.
 
Mayu umemuweka kanji sawa mkuu, maana nlikuona sana kwenye jukwaa letu
 
Tafuta utaratibu wa Bond-certificate ununue hio.
 
Miaka miwili iliisha Julai 19 2022, tupe za juu juu ulifanya nini, tujifunze na sisi [emoji4]
 


Sasa ukawekeze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…