Kunyimwa goli: Yanga yaenda CAF kudai point 3

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Medeama, uongozi wa klabu ya Yanga umeliandikia barua Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) KULALAMIKA uamuzi mbaya ulioonyeshwa na mwamuzi aliyechezesha mchezo wao huo
.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Rodgers Gumbo alikiri kuandika barua ya MALALAMIKO kwa CAF “Ni kweli tumepeleka barua ya malalamiko kwa CAF kutokana na kuwa na ushahidi wa matukio ambayo ni wazi hatukutendewa haki ambayo ni pamoja na rafu ambayo mchezaji wetu Nickson Kibabage alichezewa na mchezaji wa Medeama ambaye alistahili kuonyeshwa kadi nyekundu lakini refa hakufanya hivyo.
.
“Lakini pia kuna tukio la bao letu halali ambalo Kibabage alifunga lakini refa akalikataa akiwaaminisha watazamaji na wachezaji kuwa waliotea hivyo sio bao sahihi lakini baada ya kulitazama kwenye video tumebaini uonevu; Tumewaandikia ili wajue nini cha kufanya kwa sababu matukio kama yale yananyima timu haki ya kupata ushindi na kuipa nyingine matokeo ambayo haijastahili,” alisema Gumbo

My Take
Utopolo at work
 
Ni vizuri kuwaandikia barua CAF, Lakini sidhani kama kuna sheria au kanuni ambayo inaweza kuipa Yanga ushindi kwa maamuzi mabaya yaliyofanywa na muamuzi wa mchezo kwa kukataa goli halali, kilichobaki wabadilishe sheria au waanzishe matumizi ya VAR katika group stage.
 
acha uongo hawajaenda kuomba pointi,wamelalamika ili caf watafute njia ya kutatua dosari hizo,yanga inaongozwa na ceo bingwa kabisa ambae alishafanya kazi caf,hawezi kuomba points kwa mchezo ulioisha
 
Kazi imeanza. Huko kwenye hizo ofisi ikiwezekana kuwe na ofisi maalum chumba kikubwa cha barua za malalamiko. Wawasiliane na TFF kwa maelekezo kuwa ni mafaili gani yanahimili karatasi nyingi maana wana uzoefu.
 
Wewe mhasibu feki hunaga akili hata robo kichwa cha habari na maelezo vinapishana
 
Kazi imeanza. Huko kwenye hizo ofisi ikiwezekana kuwe na ofisi maalum chumba kikubwa cha barua za malalamiko. Wawasiliane na TFF kwa maelekezo kuwa ni mafaili gani yanahimili karatasi nyingi maana wana uzoefu.
Umelelamikiwa wewe mbona kiherehere?
 
Kwani nimesema kuna ubaya? Nimesema wajiandae kisaikolojia kwa malalamiko.
 

Mechi inaweza kurudiwa kwenye neutral ground
 
Suala la point 3 halipo, sana sanam wamuzi anaweza kupata adhabu kama kweli kuna kosa la wazi kabisa alifanya.
 
Mechi inaweza kurudiwa kwenye neutral ground
Ikiwa hivyo itakuwa si haki, kwani tatizo ni la waamuzi na si la timu iliyofungwa goli, waamuzi (lines man & referee) ndiyo waliyotoa hukumu ya kukataa goli, hata wakirudiana kwenye neutral ground na refa yuleyule itakuwa hakuna faida. Ikiwezekana waamue kuwe na kamati ya kuchunguza mechi kwa njia za video baada ya michezo kwisha na kutoa hukumu ndani ya masaa 24 kwa hizi mechi ambazo hazina VAR ili kutoa haki iliyopokwa aidha kwa bahati mbaya au makusudi kwa aliyedhulumiwa na watendaji makosa wapewe adhabu inayostahiki.
 
Hii mechi Yanga wakiongea vizuri inaweza kurudiwa vizuri sana. Blv me
 
Wewe bado haujapona.
Orodha ina bali wale wale wa 4.
Kikwete,manara mkubwa,gamond na jana kaongezeka msigwa.
Endelea kutumia dozi utapona na wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…