EBF= Exclusive Breast Feeding,ni njia mojawapo inayoshauriwa kwa kinamama sero+ve.
Katika hili mama anashauriwa kutompa kitu chochote mtoto zaidi ya maziwa yake na dawa atakazoshauriwa kitaalam kwa miezi 6 za mwanzo.
Baada ya miezi hiyo mama anashauriwa kumwachisha ziwa mtoto na kumwanzishia lishe mbadala.
Akizingatia utaratibu huu na mwingine atakaoshauriwa kituoni uwezekano wa kumwambukiza mtoto kwa njia hii utadhibitika.