Kuoa / kutooa kipi bora


Mambo ya ushirikina yana mwisho wake yakiwageuka ndo wataiona dunia ilivyochungu, au nawewe unafurahi maisha mwanaume kukaa kama zezeta ndani ya nyumba. Hebu mtangulize mungu yote yatawezekana
 
Nimekuelewa kiongozi - si kwenye mabaa wala makanisani, wanakwaya wanabanjuanaa, maofisini wakitoka wanapita wanakokujua, kwenye sehemu za kazi mbalimbali tunayaona - utasikia wanasema mke wa fulani huwa anachukuliwa na kijana fulani. Imefikia hatua ya watu kufanyiana ubaya sababu ya ngono. Wataka kunambia unakoishi mambo hayo hayapo?
 
Mbona haujazungumza wanaume ambao sio waaminifu?Umewasakama dada/mama zetu kama vile wao tu ndo wanaovuruga ndoa,kuna wanaume ni kero,hawafai kuitwa baba!
 


ok kawaida binaadamu huwa tunaangali sana makosa
na tunawajadili sana wanaokosea unaweza fikiri ni kila mtu anafanya

humo humo maofisini,mitaani na makanisani na kwingineko
wapo walio waaminifu na upendo tele kwenye ndoa zao

mimi nilikuwa kwenye kampuni inayosifika kwa ngono mjini hapa

na kulikuwa na wanandoa weengi mno waaminifu
na wadada weengi tu wametulia
 
Mambo ya ushirikina yana mwisho wake yakiwageuka ndo wataiona dunia ilivyochungu, au nawewe unafurahi maisha mwanaume kukaa kama zezeta ndani ya nyumba. Hebu mtangulize mungu yote yatawezekana

Siyataki yananiuma ndo maana ya kuanzisha mada hii hili kupanuana mawazo. Dada yangu kuna wamama wanaaga kwenda nje ya nchi kufata mzigo ya maduka yao, yanayofanyika huko usiombe kuadidhiwa. Ukienda nawewe ukaona, siku ukiambiwa wifi yako huwa anasafiri kwenda nchi fulani hakika utamshauri kaka yako azuie hiyo kitu mara moja na akimzuia tu wifi yako ataachana na kaka yako.
 
The Boss, kumbe ninayoyaongelea nawe unayajua? Kwa kweli yanakera. Hao wachache ndo wanachefua na kwa taarifa yako si wachache ni wengi wanaofanya hivyo. Kuna mhubiri mmoja - siku nilipokutana naye kwenye mji tofauti akiwa na mtu tofauti na mmewe - iliniuma sana na kila nilipoenda kanisani nikamkuta anaendesha program nilitoka nje. Nina mifano mingi ndugu yangu.
 
Mbona haujazungumza wanaume ambao sio waaminifu?Umewasakama dada/mama zetu kama vile wao tu ndo wanaovuruga ndoa,kuna wanaume ni kero,hawafai kuitwa baba!

Usichukie ndg yangu, tukiyajadili kwa uwazi tunaweza kupata ufumbuzi kuliko kuyafumbia macho. Mambo hayo yanaanza mapema kabla ya kuingia kwenye mahusiano halali. Kama we ni mfuatiliaji kwenye vyuo vikuu mabinti zetu ndo wachafu zaidi ya vijana, matokeo yake hao mambinti ambao ni wanandoa watarajiwa na wengine ni wanandoa tayari wakiingia mtaani ni baraa tupu. Tusiseme kweli????
 
Hutojitendea haki kwa lipi?!Kumjulisha mtu kama uko ndani au nje ya ndoa hakukupunguzii chochote zaidi ya kuwafumbua macho wanaopokea michango yako kwa kufahamu kama unayosema umeyapitia...umeona au umefikiria tu!!
 
Daaahhh haya mkuu Naona una majibu ya kunyaMambo madogo tu lakini.Hapo juu naona umewakandamizaTu wanawake Je wanaume hawatoki ndani ya ndoa zao?Anyway kama umeoa yaelekea humuaminiMamito wako.. pole Kama hujaoa acha kuongea utumbo.Subiri upitie kwanza ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…