Kuna faida na hasara zake.
Kwa kuanzia faida ya kuchelewa kuoa, unakuwa more mature, umemaliza pilika pilika za moto wa ujana, hivyo unakuwa umetulia.
kitendo cha kutokimbilia kuoa mapema, kinakupatia muda wa kutafakari kwa makini, wewe ni mtu wa aina gani, na ungetaka nani awe sehemu ya maisha yako mpaka mwisho wa maisha yenu, hivyo by waiting,you have everything to gain and nothing to loose.
Ila huko kungonja, kusiwe kungonja sana mpaka umri wa ujana unakutoka, ndipo unao umri wa uzee inapoanza.
Hasara za kuchelewa sana kuona ni kuwa modern life is very fast, hivyo kuchelewa kuoa, unachelewa kujenga familia, life fun inapungua hivyo unaendesha boring life for the rest of your life. Watoto wako badala ya kucheza na baba, wanacheza na babu-baba au baba-babu.
Tatizo jingine la kuchelewa kuoa, ni kukomaa kwa tabia za ujana kwenye maisha yako na kuwa ndio order of the day, hivyo ikiwa womanizer, katabia hako kanaingia kwenye damu, hata ukioa, haubadiliki.
Pia sio vibaya nikumegea faida za kuoa mapema sana na hasara zake.
Mimi nilioa at 25 mara tuu baada ya kumaliza chuo, mke nae nilikuwa nae chuo. life mwanzo ni vurugu tupu, unajidhania ulipenda huku damu inachemka, ukisikia wife anasafiri, unafurahi maana ni viwanja kwa kwenda mbele. Hivyo nilikuwa sijatulia na kabinti kadogo wivu mwiingi.
Faida ni kujenga maisha mapema, kujipanga vizuri na kujenga familia at the fun time. by now, my boys ni kama wadogo zangu na vibinti ni vidogozake wife and sasa ndio kwanza goodtime life imeanza, no more viwanja, ni family outings ama mambo ya starehe za kiutu uzima kama bend.
Pia usiogope kuoa mapema utapitwa, haupitwi kwa sababu mambo ya kujinafasi bado yapo, yalikuwepo na yataendelea kuwepo na yanakuwa ni ya kiutu uzima zaidi, ni ya staha na heshima mbele, fujo fujo no.