Mie nilikuwa nawaona watoto wa Kizungu miaka ileee. Unakuta Binti akiwa na Mcongo basi anaondoka Kwasakwasa hadi unakaa chini.
Akiwa na Mtanzania, Mduara hadi anajua kuimba "Kachirii Kachirii, Saga."
Akiwa na West Africa, basi anaondoka Mapouka ni kasheshe. Akiwa na Mnigeria/Ghana basi Fufu ndiyo home.
Yupo mmoja kwa sasa Dar kaolewa na Mshikaji, yeye unamkuta hadi mtoto kambeba Mgongoni na khanga
🙂
Wanawake wote ni sawa ila UTALALA ULIPOTANDIKA. Samaki usipomkunja yungali mbichi, basi UTAKUNJWA WEWE.
La muhimu ni kufahamu wewe na yeye (muelimishe) sasa ni mwili mmoja. Haya ya kufanyiana mashindano nani anatawala ili akajisifie nje, mnarudishana sana nyuma wote. Inatakiwa msaidiane kwa kila hali ili muendeleze maisha yenu kwani mkikwama, ni aibu yenu wote. Mkifanikiwa basi ni Heshima yenu nyote. Mkishaanza kushindana ndani ya nyumba kuwa nani ni mkali, ili tu mkajisifu kwa marafiki zenu, basi huo mji ujuwe umekwisha. Fanya mahesabu yako vizuri na ukiamua kuowa, hata awe ni Mzee, kaa naye chini na mueleze nini unakitegemea kwake kama Mke na kipi akitegemee kwako kama mume.
Haya ya kupika, kuosha nguo kwani ni shida gani? Kama mkeo yuko kazini bado na wewe umerudi mapema, kwa nini usipike? Kwa nini usisaidie kusafisha nyumba? Unakuta mama na Mimba yake mtumbo huo, bado alikuwa kazini na akifika lazima apike, na jamaa limekaa tu kwenye TV linabadilisha Chanel za TV na kama Ngereja kakata umeme, basi katoka kwenda kupata Moja baridi na kitimoto. Kwa nini usiwe na huruma kwa mkeo na kumsaidia baadhi ya kazi? Unaogopwa kuchekwa kuwa "Mwanaume anapika" khaaaa!!!!! Kwanini unajali wanayosema watu wa mbali kuliko kujali anavyojisikia MKEO/MUMEO?
Mkiwa na wanawake/wanaume na hasa siku za mwanzo, waonyesheni hasa tabia zenu ili mwisho wa siku kusiwe na kulia/kusaga meno. Mtavuna mlichopanda. Ukiwa mkweli kwa mkeo, basi hatakuacha hata kuweje. Atakuwa na wewe na kukusaidia bila kujali anapata kipato kikubwa kiasi gani.
Nilishaona Film Documental ya Wageruman wanaoishi nje. Mmoja alikuwa kaolewa na M-Jamaica na wakawa wamehamia Jamaica. Mama ni meneja wa Mzinga wa hotel ya Kitalii na jamaa ni Mkulima. Mchana mama yupo kazini, gari zuri, ofisi safi na jioni anarudi nyumbani kwa mumewe na binti yake na nyumba hata umeme haina. Jamaa anaenda shambani kulima na kutunza mifugo, time to time anavuta JANI, anarudi mapema kupika na usiku wanapata wote chakula nyumbani (kumbuka mama kazini ana misosi mizuri tu). Ila kama Mwanamke kakupenda, basi ataacha kazi German, atakuja Jamaica na kwenda kuishi kwenye nyumba ya hali ya chini huku akiacha mazingira ya hali ya juu ambayo akitaka, muda wowote anaweza kurudi kuishi kwenye nyumba ya hali ya juu. Ila hilo siyo lengo la MAPENZI.
Mwingine aliyenifurahisha ni Mama President wa kampuni ya BOSCH akiitwa IZA BOSCH. Huyu mama na UTAJIRI wake woote, anaishi na Boyfriend aliyetokea Eastern German. Jamaa ni masikini sana. Anatembelea gari la kizamani mno la Easter German (Trabant). Sasa siku moja wanaonyesha jamaa ana Birthday na mama anahangaika kumtafutia zawadi. Angeliweza kumpa hata ndege akitaka ila mama anadai hiyo itamnyanyasa sana jamaa maana siku yeye akiwa na birthday, jamaa atakuwa anahaha amnunue nini yeye Iza ili afurahi? Mama alienda kiwandani na kuwaambia Wahandisi watengeneze chuma fulani cha ndani ya gari (pambo) ambalo jamaa alikuwa akikitafuta kwa siku nyingi. Siku hiyo jamaa alipopata kichuma cha TRABANT yake, alifurahi sana sana. Chuma hicho ni bei nafuu tu kama ukikipata kinauzwa. Jamaa alikuwa happy na kujua hata yeye hahitaji kununua kitu cha bei kubwa kwa sababu mama hana Complex nyingi na kufanya SHOW OFF.
Doo, unaweza kuandika GAZETI ila ukweli ni kuwa haya mambo hayana Formula. Unaweza kuowa mke wa RANGI yoyote ile na yakakupata. Kuna kaka yangu aliowa Mke huyoo, na tena ana asili ya Kisukuma, ni heri hata angelikuwa kaowa ngozi Nyeupe/Nyekundu/Njano.
Nina rafiki yangu, mwanaume, mzungu wake amecorp vizuri kweli, yuko kama mswahili kabisa hana shida, hadi ugali anajua kupika