Kuolewa SIO bahati...USIBAHATISHE!

Kuwa mtoto wa mama na kuona kua kuoa/olewa ni bahati kunahusiana vipi?
Maana yake mtoto wa mwanamke mwenye Jinsia ya Kiume lazima apate bahati kutoka kwa MUNGU.
Mwanamke mwema anatoka kwa MUNGU au unasemaje?
 
Kitendo cha kuolewa ni bahati hayo mengine ni matokeo tu. Na mara nyingi husababishwa na tamaa na uchu wa mali wa akina dada wengi. Wachumba wazuri wanaojiheshimu ila wasio na uwezo hukataliwa kwa misingi ya kukosa mali. Mifani ninayo mingi sana.
 
Kuolewa ni bahati ukimpata mtu ambae anaelewa nini maana ya ndoa na kuiheshimu ndoa yake, anaempenda mwenzi wake, anaemheshimu mwenzi wake pamoja na mawazo yake, anaemsikiliza mwenzake, anaejielewa na kujitahidi kumwelewa mwenzake, aliye tayari kujitoa kwa mwenzake, anaejua na kutimiza majukumu yake, anaejitahidi kumfurahisha mwenzake kwa maneno na matendo. Vivo hivyo kwa wanaume. . . . wenye bahati sio waliooa bali ni waliooa wanawake wenye sifa nilizotanguliza hapo juu.

Tunasema ni bahati kwa kuwa wenye sifa ulizotaja hapo juu hawako wengi,hivyo ukibahatika kumpata lazima ujione mwenye bahati.

Tena Lizzy kuna wanawake wanatamani tu harusi nae eti avae shela,afanyiwe send off,mawazo ya ndoa na changamoto zake wala hayamuumizi kichwa.....mradi naye katoka kwa wazazi kahamia kwa mwanaume, akazae huko na kuishi huko....!!
 
Ni hadi wanawake watapojitambua ndio wataweza kuona haya.
 
kuolewa ni bahati 2 pale ambapo utakuwa umebahatika kuishi na m2 anayekupenda!
 
kuolewa ni nini?
 
Tatizo nyie wanawake good husband ni yule mwenye pesa. Ingekuwa kweli mnatafuta good husband msinge lialia hivi.
Tatizo la baadhi ya wanawake, kama ambavyo ni tatizo la baadhi ya wanaume kutumia kigezo cha sura kuchagua mke.
 
Maana yake mtoto wa mwanamke mwenye Jinsia ya Kiume lazima apate bahati kutoka kwa MUNGU.
Mwanamke mwema anatoka kwa MUNGU au unasemaje?
Kama kupata mwanamke mwema kutoka kwa Mungu ndio bahati basio KUOA sio bahati ila KUMUOA MWANAMKE ALIYETOKA KWA MUNGU ndio bahati.
 
Tatizo la baadhi ya wanawake, kama ambavyo ni tatizo la baadhi ya wanaume kutumia kigezo cha sura kuchagua mke.
Duh sasa uwe na mwanamke ambaye humtamani?
Sura lazima ndio vitu vya ndani. Unajua kila mtu huwa na kitu anachovutiwa kwa mwanamke.
 
Kama kupata mwanamke mwema kutoka kwa Mungu ndio bahati basio KUOA sio bahati ila KUMUOA MWANAMKE ALIYETOKA KWA MUNGU ndio bahati.
Nimekupata sasa
Nipo na wewe
 
Tatizo la baadhi ya wanawake, kama ambavyo ni tatizo la baadhi ya wanaume kutumia kigezo cha sura kuchagua mke.

Sura ni kigezo muhimu sana, haswa ukipata mwenye Sura nzuri na tabia nzuri, dunia utaiona tamu. Lakini akiwa na sura mbovu sana na tabia nzuri ndi mwanzo wa nyumba ndogo.
 
Kitendo cha kuolewa ni bahati hayo mengine ni matokeo tu. Na mara nyingi husababishwa na tamaa na uchu wa mali wa akina dada wengi. Wachumba wazuri wanaojiheshimu ila wasio na uwezo hukataliwa kwa misingi ya kukosa mali. Mifani ninayo mingi sana.

Uzuri wa mtu haupo kwenye kuwa na mali ama kutokua na mali. Wapo wanaume wasio hata na uwezo wa kununua suruali ya tatu ila tabia zao haziwezi kumfanya mwanamke aone alibahatika kuolewa nae.
 
kuolewa ni nini?

Hata sijui...ningesema kukubali kwa sababu anazojua mhusika kuishi na mwanaume kwa taratibu zinazotambulika kidini,kiserikali,kijamii etc,...but siku hizi nasikia wanawake wanaoa wanaume na wanawake wenzao, wanaume nao wanaoa wanaume wenzao....jitahidi tu na wewe Smile kutafsiri....lol....umefanikiwa ile ishu??? he he he...tukutane mailisita!
 
Hehehehe I know dearest. Wenyewe bahati ipo kwenye kuonekana nae kaolewa na sio kwenye maisha yatakavyoenda baada ya hizo chereko chereko za siku moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…