Kuondoa harufu ya kitunguu mikononi baada ya kupika

Kuondoa harufu ya kitunguu mikononi baada ya kupika

dadazuu

Member
Joined
Dec 31, 2013
Posts
46
Reaction score
8
Habari wana jf. Tusaidiane jinsi ya kutoa harufu ya kitunguu mikononi baada ya kupika maana inakera sana
 
Mbinu ya kupunguza harufu ya kitunguu mkononi,kata kitunguu kwanza halafu ndipo ukate pilipili hoho ama nyanya vyote hivyo hukata harufu ya kitunguu na mara unaponawa na sabuni harufu hupungua sana kiasi cha kutoisikia

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
hyo lotion ni baada ya watu kula na kuondoa vyombo ama baada tu ya kula Mrs Kharusy
 
Last edited by a moderator:
kama utatumia limao au ndimu katika mapishi yako tumia yale mabaki(maganda) yake kujisugulia taratibu viganjani hupunguza harufu ya kitunguu pia.
 
kama utatumia limao au ndimu katika mapishi yako tumia yale mabaki(maganda) yake kujisugulia taratibu viganjani hupunguza harufu ya kitunguu pia.

Best hii inafanya kazi. Na hasa unapoanza kitunguu na vingine vikifuata mwishoni. Asante kwa ushauri
 
Ukijisugua na limao naona kama harufu ya malimao ina replace ile ya vitunguu kwa hiyo utanukia malimao,je unawezaje kuondoa harufu ya malimao baada ya hapo?
 
Ukijisugua na limao naona kama harufu ya malimao ina replace ile ya vitunguu kwa hiyo utanukia malimao,je unawezaje kuondoa harufu ya malimao baada ya hapo?

ukiosha na maji mikono uliyosugua limao harufu ya limao inabaki kidogo sana ambayo haisikiki sana na haikeri kama ya kitunguu.
 
Best hii inafanya kazi. Na hasa unapoanza kitunguu na vingine vikifuata mwishoni. Asante kwa ushauri

kila la heri katika kuhakikisha unakua comfortable na matayarisho ya mlo mzuri.
 
Back
Top Bottom