Kuondoka kwa Ronaldo Real madrid kumechangia kuibuka upya kwa tuhuma za ubakaji?

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
12,823
Reaction score
21,210
Habari za weekend wadau wa JF.
Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu kama nilivyo wasilisha kwa mtindo wa swali hapo juu ktk kichwa cha habari.

Kwa jinsi sakata lilivyo zimwa kwa miaka 10 na kuja kuibuka sasa kiasi cha kusababisha kushuka thamani ya hisa za klabu ya Juventus soko la hisa imenipelekea kuwaza kitu cha ajabu.

Kwamba huenda timu ya wale wasiojilikana waliofanikisha kuzimwa kwa tuhuma hizo wanaotambulika kama 'fixers' huenda nyuma ya pazia walifadhiluwa na Real Madrid.
Huenda hawakutambulishwa kama watu waliofanya kazi chini ya maagizo na malipo ya Madrid kwa kukwepa kuiingiza klabu ktk kashifa kubwa hivyo ikatumika mbinu ya kuonekana mchakato mzima uliendeshwa na wanasheria wake binafsi CR7 toka Ureno.

Kilicho pelekea kuwaza hivyo ni hisia tu kwamba Madrid hawakuoendezwa na namna alivyoondoka Ronaldo(CR7) wakaona huyu dogo anajiona mkubwa kuliko klabu yetu basi ngoja tukamstue yule dada binti Mayorga aliamshe dude ili kumchafua Ronaldo na kumfanya wadhamini wake wamtose na klabu ya Juventus waingie hasara kubwa.

Tujiulize kama kweli hii hisia yangu Je, Juve wanaweza kuandaa 'fixer' wao wazime tena sakata hili kuinusuru klabu yao isikumbwe na hasara kubwa ukuzingatia mzigo mkubwa ambao walitumia kumnunua Ronaldo?

Nahisi mambo yakienda vibaya kwa Ronaldo Juve itaingia hasara kubwa sana na kuyumba kwenye mambo ya kifedha na hasa fedha za usajili.

Kama hilo litatokea linaweza kusababisha Juve kukumbana na matatizo ya Uefa financial fair play misimu ijayo.

Wapenzi wa soka bila kujali klabu tunazo shabikia au tunaopenda ushindani wa Messi na jamaa tuombe isiwe hivyo na jambo hili liishe salama na vizuri kwa upande wa CR7.

Alamsiki.
 
Huyo dem anajaribu kuitia ndoa brand kubwa kama ile hawezi hata kiduchu zaidi ya kupoteza muda na kujizalilisha duniani kote pilato mwenyewe shabiki wa Manchester kwanini asimpende ronado
 
Mmmh!! Hii Ishu wakati inatokea Ronaldo alikua bado hajasajiliwa Madrid labda pengine palikua na makubaliano ya kwamba atakwenda madrid. Maana Ishu imetokea June 2009 ambapo msimu ndo umemalizika na Cr7 alikua bado mchezaji wa Man united. So kama kipindi kile Madrid walihusika kumtetea basi pengine ndio hao walioharibu leo. Ila yote ya yote kama mdau wa soka ningependa iishe salama kwa upande wa Ronaldo, maana mazingira yanaonesha wazi kabisa kuna mchezo mchafu unafanyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…