Neno onya linabakia hapo hapo. Huwezi kusema kuonyesha, ukimaanisha kutoa onyo. Ila linaweza kubadilika tu na kuwa 'onyo'.Samahani kama nitakuwa nimekosea kwasababu lugha siyo taaluma
yangu lakini ninavyo fahamu ni kuwa:
Onyesha inatokana na mzizi wa neno 'ONYA' yaani tahadhari kwahiyo
matumizi sahihi ya hili neno lazima yaendane na tahadhari. Vivyo
hivyo "onesha" inatokana na mzizi wa neno 'ONA' yaani tazama, angalia
n.k. Mtumiaji wa hili neno nilazima amaanishe uangalizi wa kitu fulani.