Kuongea ni tiba ya maradhi ya afya ya akili

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Imegundulika sasa karibia asilimia 90% ya maradhi ya mwanadamu yanatokana na afya ya akili, ingawa kiuhalisia tukiumwa tunapata changamoto katika miili yetu lakini chanzo chake ni afya ya akili.

Kwahiyo kama tukifanikiwa kutatua changamoto ambazo zinatukabili katika afya zetu za akili basi tutakuwa tumefanikiwa kwa asilimia kubwa kuepukana na maradhi mengi ambayo yanatukabili katika maisha yetu ya kila siku.

Ebu kabla ya kuendelea tuone mfano mmoja tu kuonyesha jinsi afya ya akili ikiwa haipo sawa ni kiasi gani uharibifu mkubwa unapatikana katika mwili wa mwanadamu, mtu ambaye hajapima ukimwi na kujua status yake, anaweza kuishi vizuri tu bila kupata hathari za malazi hayo kwa mda mrefu tu, lakini atakapo pima na kujua kuwa yupo positive na kama hajaikubali hali hiyo ni dhahiri kabisa ataanza kuwa na msongo wa mawazo.

Na huo msongo wa mawazo ndio kutetereka kwa afya ya akili na kinachofuatia ni kuanza kupatwa na maradhi mbali mbali,hapo tumeona chanzo cha maradhi ya kimwili ni kutokuwa na afya nzuri ya akili.

Kwahiyo kuwa na afya nzuri ya akili ni jambo muhimu sana kwa kila mwanadamu, hakikisha siku zote uko vizuri sana katika jambo hilo,njia moja wapo ambayo ni tiba tosha ni kuongea (talk it out), usipende kuyaweka mambo kifuani kwako,share na mtu unaye mwamini shida zako na changamoto zako,kwani hiyo ni tiba tosha ya kuondoa mzigo mkubwa moyoni mwako.

Si ajabu miongoni mwa sababu kubwa za wanaume kufa mapema ni kutoongea changamoto zetu kwa watu wetu wa karibu,huwa tumefundishwa kutoka zamani kwamba mwanaume lazima ajikaze na hatakiwi kulialia bali awe imara kukabiliana na changamoto zake.

Hii tabia huenda ndio chanzo cha maangamizi yetu pia,kwasababu tunajikuta tunajaza maumivu mengi katika vifua vyetu na matokeo yake tunakufa mapema.

Lakini tofauti na wanawake wao ni watu wa kuongea sana hisia zao na machungu yao hata kwa mambo madogo tu, na mengine ya kutia aibu lakini atakwambia tu,mfano ni kawaida mwanamke kukwambia leo naendesha kweli lkn ni tofauti mwanaume kumwambia mpenzi wake kuwa leo tumbo limezingua kwahiyo naendesha balaa.

Wanawake ni watu wa kushare sana mambo yao na hii huwa ni tiba tosha ya kuondoa sumu katika vifua vyao na huwasaidia kuondokana na msongo wa mawazo ambao ndio chanzo cha maradhi mbali mbali katika miili yetu.

Daktari Karl Meninger amefundisha katika kitabu chake "The vital Balance" kwamba ugonjwa wa afya ya akili si uwepo wa magonjwa mbali mbali bali ni uwepo wa tabaka tabaka mbali mbali au mjumuisho wa matatizo ya afya ya akili yaliyo lundikana pamoja.

Kwahiyo unaweza ukawa na changamoto fulani unaimeza tu kifuani kwako,inatokea nyingine nayo unaimeza na nyingine na nyingine mwisho wa siku unakuwa na tatizo kubwa la afya ya akili,lakini kumbe kama ungeongea changamoto zako namtu ambaye unamwamini huenda ungetatua chamgamoto ambayo inakukabili kwa urahisi sana.

Mfano watu wengi ambao huwa wanajinyonga ni wale ambao wanabaki na msongo wa mawazo wao wenyewe bila kuwashirikisha wengine shida zao,matokeo yake wanaona dunia imewaelemea na njia pekee ni kujinasua kwa kukatisha uhai wao.

Kwahiyo wataalamu wanasema kuongea shida zako ni tiba mujarabu sana ili kuepukana na maradhi mbali mbali,kwahiyo.let's talk it out, tutoe madukuduku yetu katika nyoyo zetu na kuwa wepesi vifuani mwetu.

Kikubwa jua unaongea na nani, maana kama utaongea mambo yako na watu ambao sio waaminifu na watunza siri ujue kesho mtaa mzima watajua siri zako,chagua watu sahihi kushare changamoto zako.

Huwa mara nyingi hapa jukwaani watu wanashare mambo yao lkn cha kushangaza kuna watu huwa wanawadhihaki watu hawa,utasikia kauli kama "hilo nalo ni jambo la kuandikia uzi hapa?"

Msichojua nyie watu wa namna hii ni kwamba,mpaka mtu anaandika huo uzi ujue anataka kupata faraja na ni njia ya tiba pia kwake,kwako wewe waeza ona ni jambo dogo lakini kwake ni mzigo wa msumari mgongoni mwake, kwahiyo tusiwe wepesi wa kujaji mambo bila kujua tunazidi kuwaumiza watu wengine.

Wasomaji wangu, ongea changamoto zako na zitoe kifuani kwako kwani hii ni tiba kubwa sana kwa afya yako ya akili,haijalishi watu wengine watasemaje tambua upo kwenye mchakato wa kupona na kuondoa taka sumu moyoni mwako.

Ni hayo tu!
 
Vichaa wanaongea ila bado wanamatatizo ya akili!!
Hao tayar walishaathirika na kuwa hivyo unavyo waona,lkn hapa tunazungumzia mtu ambaye ana stress mingi na msongo wa mawazo ambaye anatakiwa kutoa yanayo msibu ii aponye maradhi yake
 
Imegundulika sasa karibia asilimia 90% ya maradhi ya mwanadamu yanatokana na afya ya akili, ingawa kiuhalisia tukiumwa tunapata changamoto katika miili yetu lakini chanzo chake ni afya ya akili.

Kwahiyo kama tukifanikiwa kutatua changamoto ambazo zinatukabili katika afya zetu za akili basi tutakuwa tumefanikiwa kwa asilimia kubwa kuepukana na maradhi mengi ambayo yanatukabili katika maisha yetu ya kila siku.

Ebu kabla ya kuendelea tuone mfano mmoja tu kuonyesha jinsi afya ya akili ikiwa haipo sawa ni kiasi gani uharibifu mkubwa unapatikana katika mwili wa mwanadamu, mtu ambaye hajapima ukimwi na kujua status yake, anaweza kuishi vizuri tu bila kupata hathari za malazi hayo kwa mda mrefu tu, lakini atakapo pima na kujua kuwa yupo positive na kama hajaikubali hali hiyo ni dhahiri kabisa ataanza kuwa na msongo wa mawazo.

Na huo msongo wa mawazo ndio kutetereka kwa afya ya akili na kinachofuatia ni kuanza kupatwa na maradhi mbali mbali,hapo tumeona chanzo cha maradhi ya kimwili ni kutokuwa na afya nzuri ya akili.

Kwahiyo kuwa na afya nzuri ya akili ni jambo muhimu sana kwa kila mwanadamu, hakikisha siku zote uko vizuri sana katika jambo hilo,njia moja wapo ambayo ni tiba tosha ni kuongea (talk it out), usipende kuyaweka mambo kifuani kwako,share na mtu unaye mwamini shida zako na changamoto zako,kwani hiyo ni tiba tosha ya kuondoa mzigo mkubwa moyoni mwako.

Si ajabu miongoni mwa sababu kubwa za wanaume kufa mapema ni kutoongea changamoto zetu kwa watu wetu wa karibu,huwa tumefundishwa kutoka zamani kwamba mwanaume lazima ajikaze na hatakiwi kulialia bali awe imara kukabiliana na changamoto zake.

Hii tabia huenda ndio chanzo cha maangamizi yetu pia,kwasababu tunajikuta tunajaza maumivu mengi katika vifua vyetu na matokeo yake tunakufa mapema.

Lakini tofauti na wanawake wao ni watu wa kuongea sana hisia zao na machungu yao hata kwa mambo madogo tu, na mengine ya kutia aibu lakini atakwambia tu,mfano ni kawaida mwanamke kukwambia leo naendesha kweli lkn ni tofauti mwanaume kumwambia mpenzi wake kuwa leo tumbo limezingua kwahiyo naendesha balaa.

Wanawake ni watu wa kushare sana mambo yao na hii huwa ni tiba tosha ya kuondoa sumu katika vifua vyao na huwasaidia kuondokana na msongo wa mawazo ambao ndio chanzo cha maradhi mbali mbali katika miili yetu.

Daktari Karl Meninger amefundisha katika kitabu chake "The vital Balance" kwamba ugonjwa wa afya ya akili si uwepo wa magonjwa mbali mbali bali ni uwepo wa tabaka tabaka mbali mbali au mjumuisho wa matatizo ya afya ya akili yaliyo lundikana pamoja.

Kwahiyo unaweza ukawa na changamoto fulani unaimeza tu kifuani kwako,inatokea nyingine nayo unaimeza na nyingine na nyingine mwisho wa siku unakuwa na tatizo kubwa la afya ya akili,lakini kumbe kama ungeongea changamoto zako namtu ambaye unamwamini huenda ungetatua chamgamoto ambayo inakukabili kwa urahisi sana.

Mfano watu wengi ambao huwa wanajinyonga ni wale ambao wanabaki na msongo wa mawazo wao wenyewe bila kuwashirikisha wengine shida zao,matokeo yake wanaona dunia imewaelemea na njia pekee ni kujinasua kwa kukatisha uhai wao.

Kwahiyo wataalamu wanasema kuongea shida zako ni tiba mujarabu sana ili kuepukana na maradhi mbali mbali,kwahiyo.let's talk out, tutoe madukuduku yetu katika nyoyo zetu na kuwa wepesi vifuani mwetu.

Kikubwa jua unaongea na nani, maana kama utaongea mambo yako na watu ambao sio waaminifu na watunza siri ujue kesho mtaa mzima watajua siri zako,chagua watu sahihi kushare changamoto zako.

Huwa mara nyingi hapa jukwaani watu wanashare mambo yao lkn cha kushangaza kuna watu huwa wanawadhihaki watu hawa,utasikia kauli kama "hilo nalo ni jambo la kuandikia uzi hapa?"

Msichojua nyie watu wa namna hii ni kwamba,mpaka mtu anaandika huo uzi ujue anataka kupata faraja na ni njia ya tiba pia kwake,kwako wewe waeza ona ni jambo dogo lakini kwake ni mzigo wa msumari mgongoni mwake, kwahiyo tusiwe wepesi wa kujaji mambo bila kujua tunazidi kuwaumiza watu wengine.

Wasomaji wangu, ongea changamoto zako na zitoe kifuani kwako kwani hii ni tiba kubwa sana kwa afya yako ya akili,haijalishi watu wengine watasemaje tambua upo kwenye mchakato wa kupona na kuondoa taka sumu moyoni mwako.

Ni hayo tu!
Asanteee sanaaa boss
 
kuna sie tukiongea ndo tunaonekana akili fyatu
Pole kpnz,hakikisha unaongea na watu sahihi ambao watakusikiliza kwa lengo la kukusaidia na si kukudhihaki

Tafuta watu ambao wana huruma na hekima pia
 
Woooiiii nazimwa na kofi zito kama gundi ya mdomoni
 
vp nikishare kwa mtu na nisipo saidiwa si nitaendelea kubaki na mzigo moyoni .
Kama tunavyojua binadamu tunatofautiana uelewa na ufahamu pia,huenda wa kwanza kashindwa kukusaidia lkn wa pili na watatu watakusaidia

Kwa wenzetu wa nchi zilizo endelea kuna wataalamu kabisa wa mambo ya saikoloji wamebobea katika hii fani,lkn kwa huku naona jambo hilo bado hatujalipa uzito wa kutosha

Lakini kuna watu wenye busara na hekima zao ambao wanaweza kutusikiliza na kutupa ushauri mzuri pia
 
Yaan mishangazi isimfelishe ije kuwa wewe😂😂
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🏃🏾‍♀️🏃🏾‍♀️🏃🏾‍♀️🏃🏾‍♀️
 
Back
Top Bottom