Kuongeza ukubwa wa kiwanja

Kuongeza ukubwa wa kiwanja

Rusumo one

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
3,458
Reaction score
4,283
Wakuu habari za mchana.
Naomba kufahamu iwapo naweza kuongeza ukubwa wa kiwanja changu ambacho nimeongeza kwa kufanya land reclamation na kubadili hati kuwa na ukubwa zaidi. Naomba kushauri wakuu
 
Mmmhh!
Hicho kiwanja kimepimwa (yaani surveyed or unsurveyed)? Hicho chanzo Cha maji ulichofukia ni Cha asili au man-made??
 
No sijafukia Kuna kipande nimeongezewa na Mzee wangu hapa Sasa nilitaka kuzungusha fensi niache Kama MITA 10 toka ukingo wa kijito ambacho hutililisha maji toka vichem chem. Kiwanja cha awali kipo surveyed Ila kidogo na nikiunga na hiki kinakuwa kikubwa Kama sqm 800, jirani zangu wamefanya ujenzi Hadi kwenye ukingo Sasa nikaona nije kwa wadau kupata mwongozo. Pili sheria naona inazungumzia mito,mabwawa,maziwa na bahari kuhusu umbali wa kufanya shughuli za kibinadami miongozo pls kwa vijito
 
Wakuu habari za mchana.
Naomba kufahamu iwapo naweza kuongeza ukubwa wa kiwanja changu ambacho nimeongeza kwa kufanya land reclamation na kubadili hati kuwa na ukubwa zaidi. Naomba kushauri wakuu
Unaweza bila kikwazo, zipo njia mbili ambazo unaweza kutumia mojawapo, unaweza kuchimba shimo mfano wa bwawa mita elfu moja mraba ua unaweza ukatengeneza mlima mita elfu tano mraba kwenda juu, mimi nilitumia hii ya mlima na ina faida kubwa hasa kwa Royo Tua.
 
Ok kumbe nami naweza tengeneza maporomoko ya maji kwa kutengeneza kingio kubwa watu wakaja kutalii
 
Mmmhh!
Hicho kiwanja kimepimwa (yaani surveyed or unsurveyed)? Hicho chanzo Cha maji ulichofukia ni Cha asili au man-made??
Ni mfereji Fulani ambo mvua za mwaka huu umetanua na kuwa Kama mto ambao mwaka mzima haukauka coz Kuna asili ya wet area maeneo hayo,pili eneo langu limepimwa nilishalipiwa Ila sija process hati
 
"nilishalipiwa", haki ya nani Farouk mkarimu sana, mungu ambariki.
 
Kulingana na maelezo yako,
  • Hapo ni kuna chanzo cha maji
  • Kinachangia maji kwenye mto (tributaries)
  • Ni mali ya umma.
  • Kwa sheria za nchi...Hauruhusiwi kuingilia mfumo wa chanzo cha maji asilia,ama kufanya mabadikiko ya aina yoyote.
  • Hakuna mtu mwenye umiliki wa chanzo cha maji au njia ya maji asilia.
  • Wenzako kujenga kandokando,hakuhararishi uvunjifu wa sheria.
  • Unaweza pata hati ya hapo kwa njia za magumashi, lakini mbeleni inaweza batilishwa.
 
Wakuu habari za mchana.
Naomba kufahamu iwapo naweza kuongeza ukubwa wa kiwanja changu ambacho nimeongeza kwa kufanya land reclamation na kubadili hati kuwa na ukubwa zaidi. Naomba kushauri wakuu
Unayo TP ya hilo eneo? Au Survey plan ya eneo lako?
Kama huna, tafuta, halafu uombe marekebisho manispaa ofisi ya ardhi. Marekebisho yataombwaa na baba yako (ambaye ni mmiliki/occupier wa servient land) kwa kujaza Land form #59 i.e cancellation of an easement.

Akikubaliwa, ndiyo anaweza ku-dispose hiyo ardhi kwako, kwa kuuza au by deed of gift. Ikikubaliwa, basi utaomba reparcellation.
 
Mkuu nafanyia kazi maoni yako soon July 2024, TP ninayo na eneo ni langu nilinunua kwa Mzee wangu nikimaanisha Mzee mmoja jirani yangu baadae ndo akaniongezea kipande ambacho kimepakana na kijito kinacho tiririsha maji na awali eneo lilipimwa na jiji Mwanza baadae likapelekwa Ilemela kimipaka so ramani iliyopo ni ya kale natumaini marekebisho yatawezekana. Asante Sana kwa ushauri
 
Back
Top Bottom