SoC02 Kuongezeka kwa kodi na tozo na athari za kiuchumi Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

MWANAHARAMU

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
4,041
Reaction score
10,699
Tafakuri ya leo sitoanza na salamu bali kujaribu kuelezea athari zitakazo sababishwa na kuongezeka kwa Kodi na tozo kwenye kila nyanja ya uchumi wa nchi.

Duniani kote Uchumi uongozwa na sera.

Sera hizi huwa hazifanani na kila Moja Ina faida na hasara zake.

Sera ziko mbili ambazo ni:
(1) Monetary policy
(2) Fiscal policy

Hii sera ya fiscal policy ilifuatwa zaidi na hayati Magufuli raisi wa awamu ya tano na tukaona athari zake kwenye ujenzi wa miundombinu ya Taifa hili na kupambana na wafanya biashara wakwepao Kodi, huku kundi kubwa la wanyonge likiachwa na tabasamu.

Kwa Sasa serikari yetu chini ya Samia inaegemea kwenye sera ya Fedha ya Monetary policy,

Ndiyo maneno kama tunafungua nchi ili tuweze kuruhusu uwekezaji toka nje(Foreign direct Investment) na kuweza kutengenezwa ajira na kukuza Pato la Taifa.

Lakini hii sera ya fedha Ina athari zake ikiwemo kupanda kwa bei ya bidhaa(inflation) na kuongezeka kwa pesa ya ziada kwenye mzunguko hivyo kuathiri Uchumi.

Na serikari inamitigate hali hii kwa kuongeza Kodi na tozo mbalimbali kwa wananchi wa Taifa husika ili kuimarisha hali ya kiuchumi ya Taifa husika.

Shida huku mtaani hiyo pesa iliyoongezeka ni kidogo mno na matunda yake hayajafikia Watanzania wengi na Watanzania wengi bado wanateseka na kuganda kwenye matumaini ya serikari iliyopita.

Serikari iliyopita ilihaidi kuwa nchi itakuwa ya asari na maziwa ikiwa miundombinu mikubwa ikikamilika hivyo kupelekea kutoongeza mishahara kwa miaka zaidi ya sita na kupiga marufuku uuzaji wa mazao nje ya nchi, kutoajili, kuchelewa kwa malipo ya pensheni, kutolipa kwa wakati madeni ya wazabuni hivyo ilipelekea shida kwa raia ambao waliamini mema yatakuja ila tukaishia njiani,

Kumbuka kipindi chote hicho biashara nyingi zilianguka na mfumo wa kifedha wa nchi ulitikisika ila Watanzania waliishi kwa matumaini kama wagonjwa wa Ukimwi,

Waliamini siku moja hali itakuwa nzuri zaidi ila hawakujua Mwanadamu anapanga ila kudra ya Mungu haizuiliki na kilichotokea kimetokea.

Kwa nini Sasa kilio kimekuwa kikubwa zaidi?

Ni kwa sababu hali ya mwananchi mmoja mmoja kiuchumi haijabadirika ila Kodi na tozo zinaongezeka hivyo kumbebesha raia wa kawaida mzigo mzito ambao hata Punda atashindwa kuubeba.

Tendo hili litaleta athari zifuatazo kwenye uchumi wetu:

(1)NGUVU YA MWANANCHI KUNUNUA KUPUNGUA(Purchasing power)
Sasa pesa itakatwa kila hatua inayopitia hivyo kutofautiana na kanuni ya Kodi:
Inayosema pesa itakatwa Kodi mara moja ikiwa imetoka kwenye chanzo kimoja.

Hali hii inafanya kiasi kikubwa Cha pesa kubaki serikarini huku raia wakiachwa makapuku hivyo kuleta athari kiuchumi.

Kivipi?
Uchumi wa kisasa unajengwa na kukua kwa Kasi pale raia wanapokuwa na nguvu kubwa ya kununua na sio kuweka akiba.
Hali hii italazimisha pesa kuzunguka kwa Kasi hivyo kuongeza thamani yake.

Mfano pesa ya Marekani inafanya uchumi wa Marekani uwe mkubwa kwa sababu ya raia kuwa na nguvu kubwa za kununua hivyo kufanya pesa kuzunguka na u humid kupaa.

(2)UWEZO WA KUWEKA AKIBA HUPUNGUA
Nani asiyejua ongezeko la Kodi na tozo inaenda Moja kwa Moja kuathiri uwezo wa Wananchi kuhifadhi fedha kwenye taasisi za kifedha ambao hutumia fedha hizo kufanyia biashara na kukuza uchumi.

Kinachofanyika Sasa ni wananchi kupunguza kuweka akiba hivyo kuzidhoofisha taasisi za kifedha.

(3)DOUBLE TAXATION (Kutozwa Kodi zaidi ya mara moja)
Kwa hali ilivyo pesa kutoka chanzo kimoja kitatozwa Kodi zaidi ya mara moja ambayo ni kinyume Cha Sheria ya Kodi.

Mfumo huu ukiendelea Serikari inakuwa ndiye mnyang'anyi na jambazi kwa raia wake.

Mfano:Tuwachukulie Wafanyakazi wa Serikari ya Tanzania na mishahara Yao.
Mshahara wa mwajiriwa kabla na baada ya Kodi.
Gross Salary xxxxxxxx
Paye xx
Nhif. Xx
Psssf. Xx
Net Salary. Xxxx

Lakini pamoja na kuwa umekatwa Kodi, lakini bado akipenda kuuchukua benki,
Atakatwa Tozo ambayo itatolewa Toka kwenye chanzo kile kile ambayo serikari imeshakata tayari , huu ni wizi na bado makato ya benki yapo pale pale.

Kumbuka hayo makato ya benki Bado serikari pia itachukua fungu lake.

Mfanyakazi huyu tuseme Mwalimu akitaka kumtumia mzazi wake pesa, kumbuka chanzo ni pesa ya mshahara watamkata wakati wanaituma na mzazi wake akitaka kuitoa kwenye mtandao wa simu ili atatue shida zake nayo watakata pia.

Mpaka Sasa makadilio ya kutuma kwa mzunguko huo yanafikia robo ya thamani halisi ya pesa iliyotakiwa ikatwe na hapa ni kumuongezea mzigo mwananchi.

(4) WATU WATAWEKEZA KWENYE VITU MBADALA.
Kwa mtindo wa tozo unaoendelea Sasa tusishangae Watanzania wakaanza kuweka fedha zao kwenye bidhaa ambazo thamani yake haishuki kirahisi mfano Dhahabu.

Kumbuka ukihifadhi kwenye bidhaa ya aina hii basi Kuna uwezekano mkubwa wa pesa yako kuongezeka kwa sababu bei ya dhahabu uongezeka kila mwaka hivyo kutunza thamani ya pesa yako na faida pale mtu atakapo taka kuuza.

(5)SOKO LA MITAJI/HISA KUYUMBA
Unagundua Moja kwa Moja kuwa tozo na Kodi hutikisa mpaka kwenye soko la hisa na mitaji mfano Dar es Salaam stock exchange (DSE) na UTT hivyo kupeleka athari Moja kwa Moja kwenye thamani ya makampuni na soko la mitaji.

(6)KUSHUKA KWA THAMANI YA FEDHA
Ndio hakuna atakaye shangaa pale shilingi itakapo zidi kuporomoka dhidi ya dora ya kimarekani.

Kwa nini?
Pesa ya Sasa ipo kwenye mfumo wa Currency neno lilitoholewa toka neno Current kwenye umeme.

Kama ulivyo umeme ili taa ziwake inabidi electrons zisafiri au kufanya mzunguko Toka positive charge kwenda negative charge, ndio hivyo hivyo ili pesa ipande thamani inatakiwa iwe inatumika zaidi kwenye mzunguko na ndio maana watu husisitizwa kuweka pesa kwenye mabenki na mifumo mingine ya kifedha.

Nini kitatokea ni kwamba Sasa watu wataanza Kutoa pesa kwenye taasisi za kifedha na mifumo mingine ili kukimbia tozo na kuziweka majumbani hivyo kupunguza mizunguko ya fedha, hatimaye kusababishwa thamani ya fedha kushuka kabisa kama sio kuanguka.

(7)KUTOTENGENEZWA KWA MITAJI( CREATION OF CAPITAL) NA UTAJIRI.

Kwa Sasa nchi ilipofikia kila bidhaa anayotumia mwananchi basi italipiwa Kodi ya ongezeko la thamani V.A.T.

Ukimjulisha na Tozo pamoja na Kodi basi serikari inatengeneza mazingira magumu kwa raia wake kuweza kutengeneza mitaji,
achilia mbali utajiri.

Hii itapelekea Watu au Makampuni kutoka nje ya Tanzania yaliyo na mitaji huku yakipewa misamaha ya Kodi(tax relief) na serikari yetu kuhodhi rasilimali na njia kuu za uchumi na Watanzania kuendelea kuwa vibarua na manamba katika Taifa lao.

Mfano😀ouble taxation kwenye Ardhi na Jengo, kumbuka Kuna Watanzania wamewekeza kwenye nyumba za kupangisha.

Hapa Mtanzania analipa Kodi ya Ardhi na Kodi ya jengo wakati vyote vipo sehemu Moja na maumizi ni yale yale

Na Kodi mpya ya upangaji(Rental tax) ambayo inaongezeka kuongeza ugumu wa maisha kwa Wala hoi.

(8)KUPUNGUA KWA WATEJA KWENYE HUDUMA YA KIBENKI NA TAASISI ZA FEDHA.

Hili halina maelezo mengi kwa sababu mpaka Sasa Watanzania wenye akaunti ni asilimia 20 kwa Watanzania wote.

Kitendo Cha kuongeza tozo itapelekea baadhi ya wateja kuniondoa kwenye mifumo ya kibenki.

Madhara yake ni kupungua kwa Kasi ya ukuaji wa uchumi na ndoto za Tanzania kuwa donor country, lakini pia zigo la misumari kuhusu ugumu wa maisha kwa Watanzania halitotuliwa ila kumuongezea mzigo.

Aina hizi za tozo hazikubaliki Kuna umuhimu mkubwa kwa watu wenye Mamlaka kujitafakari na kuja na vyanzo mbadala bila kugusa maisha ya wanyonge moja kwa Moja.

Naomba kuwasilisha.

JamiiForums-9985586.jpg
 
Upvote 6

View attachment 2329948
Unatakiwa uwe waziri

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom