Kuongezeka kwa ujenzi wa vituo vya mafuta DSM

UFIPA:uchumi unasinyaa[emoji50][emoji50]
MTAA:nyumba mpya zinajengwa.
TPA:kodi ya kuagiza gari iongezwe,maana yanakuja
kwa kasi.
 

wenzako wenye sheri wanaangalia mahitaji,wewe unaangalia kelele za mtandaoni.
 
wenzako wenye sheri wanaangalia mahitaji,wewe unaangalia kelele za mtandaoni.
Mahitaji ndiyo petrol station ijengwe pembeni mwa shule?? Ijengwe nyuma ya nyumba za makazi ya watu??
Siku likitokea la kutokea watasema walizingatia mahitaji??

Petrol station ijengwe kwenye mahitaji, ikizingatia usalama pia, hizo barabara vijijini pia zipo zinawahitaji, kwanini wasiseme vibali vya mjini vimetosha, sasa ni huko vijijini kama umeme umeshaenda.
Labda kama wanahalalisha, biashara ya mafuta ya vidumu.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kwahiyo wakiibia serikali ni haramu, ila wakiibia sekta binafsi ni halali??
Kuwe na aina mbili za wezi!
Au sijakuelewa??😂😂😂

Everyday is Saturday................................😎
 
Shida yenu bado mnapenda tuishi kama mashetani, wakati tulikuwa tunaishi kama malaika.
Ni kweli mkuu, watu walipofushwa na mapambio ya "mtetezi wa wanyonge" wakasahau kbs kuwa malaika alitaka tuishi kama mashetani.

'Haijawai tokea watu kukamatwa kwa kusherehekea kifo!
Kamanda alisema "walikutwa wamepika supu ya mbuzi na pombe ya kienyeji lt.sijui 20 vileee!!? Haahhaaa haaa!

Ona hata kamanda mzima hajui kama aliekuwa anamtuma kufanya hivo ameshakufa! Anaona labda ni kawaida tu!!

Bado tunakazi kubwa ya kuendelea kuwaombea hawa wafuasi wake wote wamfuate.
 
Tanzania Ni Tajiri
Ni Nchi Nzima Vituo Tena Havizingatii Umbali
Kweli kabisa hawazingatii umbali. Najiuliza hamna sheria kutoka kituo kimoja hadi kingine? Pale St. Peters kuna Total mbele baada ya nyumba nne kuna kingine kipya kinajengwa. Kigamboni kwenye round about ukitoka darajani kwenda Kibada kuna kituo, mbele yake baada ya nyumba moja kuna kituo kipya cha ENGEN kinajengwa. Njia hio hio mbele kipande cha km 3 kuna vituo karibu 6 vinajengwa, ni wazi kuna uhitaji mkubwa wa mafuta ya magari.
 
Sheria na taratibu zilizopitishwa mwaka jana kuhusu makampuni ya Mafuta zimewafanya wenye makampuni hizo kufanya Petrol stations kuwa plan B
 
Nimekuja nduki, kunakitu umesahau kukizungumzia: je, ongezeko/ujenzi huu haukiuki sheria⁉️ nijuavyo mimi sheria inaelekeza umbali unaotakiwa kitoka kituo kimoja hadi kingine - sasa naona kama kuna bituo vimesogeleana
 
Kiukweli linenishangaza pia, ni dar nzima. Kilwa road nimeshughudia kama mbili. Njia ya mbezi kutokea goms zaidi ya tano. N.k
 
Sio bagamoyo road tu ni sehemu nyingi

Usiseme hela hakuna

Wewe ndo huna hela...!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati naingia Dar miaka kibao iliyopita, Dar kulikua na vituo vya petroli 17. Hivyo Ni pamoja na kile Cha BP terminal one kule eapot.
Kipindi hicho hakuna daladala, uda zilikua zinaishia Temeke, eapot, Ubungo, Mwenge na kawe.
 
Wakati naingia Dar miaka kibao iliyopita, Dar kulikua na vituo vya petroli 17. Hivyo Ni pamoja na kile Cha BP terminal one kule eapot.
Kipindi hicho hakuna daladala, uda zilikua zinaishia Temeke, eapot, Ubungo, Mwenge na kawe.

Mkuu nimekucheki inbox sana ila kimya tu__naomba ntumie namba zako (kuhusu yale mambo yetu)
 
Benki nazo hazikuwa na fedha?
 
tunajegewa kituo cha mafuta amana ilala kwenye mbanano wa majumba ya kuishi watu na hospital ya amana wanajenga shell mtaa uhuru/arusha
 
Kuna kimoja cha Lake Oil kimejengwa katikati ya Makazi ya Watu na nimejiuliza Maswali mengi mpaka nikakosa majibu yake.
 
Nyinyi mliamini Magufuli ni mungu, kumbe alikuwa anatupeleka shimoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…