Kuongezeka kwa wimbi la walimu wa ujasiriamali na Uchumi huku wengi wao wakijiita majina ya Coach, mentor, n.k

Lasway.Jr

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
233
Reaction score
413
Ndugu wana Jf leo naomba nieleze kuhusu wimbi la watu wengi hasa mijini wanaoelekeza nguvu nyingi kuwafundisha watu hasa vijana Biashara hasa ujasiriamali !
Mimi katika pita pita zangu nimekutana na watu wengi sana kwenye mitandao na hata ana kwa ana na watu hawa wanajiita Walimu, coach, mentor na majina mengine mengi yenye kuvutia kulingana na kile anachokifanya.
Na vijana wengi na akina mama wamekuwa mstari wa mbele kuwasiliza na hata kuwalipa pesa nyingi ili tuu wafundishwe ujasiriamali au namna ya kujiajiri, pia hawa watu wameandika vijitabu ambavyo mara nyingi hulazimisha wale wanaowafundisha kuvinunua na kuvisoma pia wamekuwa wakidharau sana watu walioajiriwa na kuwaona kama waliopotea njia.
Hapa nina maswali au mambo machache ambayo wadau nataka tuisaidie jamii yetu hasa vijana
1. Je ni qualifications zipi mtu anatakiwa kuwa nazo ili ajiite mwalimu, coach, au mentor kwenye ujasiriamali?
2. Je kuna chomba gani au vigezo gani jamii hutumia ili kubaini waalimu, coach, mentor wa kweli kwenye ujasiriamali?
3.Ni wapi hasa watu hawa wanapatia katika kufundisha au ni wapi huwa wanafanya makosa sana?
4. Je kuna haja ya serikali kuingilia kati na kusimamia ubora na ueledi wa watu hawa ili wasiipotoshe jamii au kudanganya?

Wakati wadau mkiendelea kuchangia nimalizie kwa kusema kuwa kwa dunia ya sasa the next group of people ambalo litasikilizwa sana na kupewa uzito sio tena wanazuoni au wasomi bali ni watu wale ambao wameweza kutatua matatizo ya watu na kuwapa solution stahiki na matajiri au entrepreneurs

Lakini tusipojenga misingi imara ya kukua tumsilize nani na wapi tutapata taarifa au elimu sahihi ya haya mambo tutaishia kuwa na kizazi cha hovyo kabsaaaa
Karibuni[emoji91][emoji41]
 
Wanapokosea ni kutowaambia watu ukweli. Kuwa wanaweza toboa kwa mazingira yotote yale. Mwisho watu wanaishia kuwa frustrated.
 
Mi niliacha kuwafatilia nilipokuja kugundua wengi wao wameshindwa kujiendesha wenyewe maisha yao....
Wengi hawana mafanikio wanayoyaelezea na kudai kuwapa watu mbinu za maisha
 
Ulitaka waje kukuomba hela ya kula??
Usiichoshe akili yako kufikiri vitu ambavyo havikudhuru kwa namna yeyote
 
Nianze kwa kuungana na wewe katika sentensi yako ya mwisho, Katika dunia ijayo, tena hasa kwa nchi yetu Tanzania, wanaoitwa wasomi au wanazuoni hawatosikilizwa tena.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba wamekuwa si watu wakutatua matatizo bali wameenda mbali zaidi na kuwa vyanzo vya matatizo hayo. Nikuulize tu Mkuu, unahisi miswada ya sheria kandamizi hapa nchini inaandaliwa na nani kama si hawa wanaoitwa wasomi wabobezi???

Nikija katika upande wa maswali yako.

Mwalimu ni mtu yeyote mwenye ujuzi wa jambo fulani, ambalo anawezakuwafundisha wengine. Unaweza ukaamua leo uanze kufundisha majirani zako jinsi ya kujiunga na kutumia JamiiForums kama chanzo chao cha kupata habari muhimu hapa nchini, wewe utaitwa mwalimu wa Jinsi ya kutumia JF.

Vigezo ambavyo watu wengi hutumia kubaini walimu na mentors ni kuangalia mafanikio ya mwalimu pamoja na matarajio wanayoahidiwa kuyapata baada ya kufundishwa ujuzi huo. Watu wengi hukwama hapa, Mentors karibia wote hapa nchini, wamejifunza copywriting na selling. Hii huwafanya kuweza kuwa na ushawish mkubwa lakini ukweli ni kwamba wengi wamekariri tu yale wanayofundisha, hii ndio sababu ukisoma vitabu vyao karibia wote utagundua ni tafsiri ya maandishi ya wazungu. No innovation at all.

Mfano mzuri kuhusu hili, ni mentor fulani maarufu hapa nchini. Wiki hii nilimu-unfollow baada ya kugundua kwamba anafanya plagiarism kutoka kwa James Clear. Kama mnafuatilia alipost makala kuhusu Pareto rule.

Mentors wa hapa nchini hupatia zaidi katika kutoa hamasa kwa watu, hasa wale waliokata tamaa na kujiona kumbe they can still make something. Kwa upande wa pili hukosea katika kufundishia mifano isiyokuwa na uhalisia hapa nchini. You can name few.

Kuhusu suala la serikali kuingilia kati sidhani kama ni wazo zuri, kwani liccha ya walimu wengi kuonekana kutokidhi vigezo bado kuna wanafunzi wachache ambao hufanikiwa kutokana na kile kidogo wanachofundishwa.

Jambo la msingi, tunaweza kuanzisha platform. Lets say website ambayo itakuwa ikitoa reviews kuhusu hawa watu. Hii itasaidia kuwatambaua waliobora miongoni mwao.
 
Ndugu wana Jf leo naomba nieleze kuhusu wimbi la watu wengi hasa mijini wanaoelekeza nguvu nyingi kuwafundisha watu hasa vijana Biashara hasa ujasiriamali !
Mimi katika pita pita zangu nimekutana na watu wengi sana kwenye mitandao na hata ana kwa ana na watu hawa wanajiita Walimu, coach, mentor na majina mengine mengi yenye kuvutia kulingana na kile anachokifanya.
Na vijana wengi na akina mama wamekuwa mstari wa mbele kuwasiliza na hata kuwalipa pesa nyingi ili tuu wafundishwe ujasiriamali au namna ya kujiajiri, pia hawa watu wameandika vijitabu ambavyo mara nyingi hulazimisha wale wanaowafundisha kuvinunua na kuvisoma pia wamekuwa wakidharau sana watu walioajiriwa na kuwaona kama waliopotea njia.
Hapa nina maswali au mambo machache ambayo wadau nataka tuisaidie jamii yetu hasa vijana
1. Je ni qualifications zipi mtu anatakiwa kuwa nazo ili ajiite mwalimu, coach, au mentor kwenye ujasiriamali?
2. Je kuna chomba gani au vigezo gani jamii hutumia ili kubaini waalimu, coach, mentor wa kweli kwenye ujasiriamali?
3.Ni wapi hasa watu hawa wanapatia katika kufundisha au ni wapi huwa wanafanya makosa sana?
4. Je kuna haja ya serikali kuingilia kati na kusimamia ubora na ueledi wa watu hawa ili wasiipotoshe jamii au kudanganya?

Wakati wadau mkiendelea kuchangia nimalizie kwa kusema kuwa kwa dunia ya sasa the next group of people ambalo litasikilizwa sana na kupewa uzito sio tena wanazuoni au wasomi bali ni watu wale ambao wameweza kutatua matatizo ya watu na kuwapa solution stahiki na matajiri au entrepreneurs

Lakini tusipojenga misingi imara ya kukua tumsilize nani na wapi tutapata taarifa au elimu sahihi ya haya mambo tutaishia kuwa na kizazi cha hovyo kabsaaaa
Karibuni[emoji91][emoji41]
Kwanza tambua kwamba Ujasiriamali haufundishwi. Kokote kule. Ujasiriamali ni hari.

Ujasiriamali ni sawa na Mapenzi. Je usha ina chuo cha kufundisha watu kupenda?

Kufall in love ni spirt na huwezi kuifundisha.

Wanao enda kutafuta Elimu ya Ujasiriamali ni kutaka kuficha uoga na pia ni kujiongezea uoga tu na pia hakuna Chuo cha Kufundsha ujasiriamali.

Vipo vyuo vya kufundisha Business skills na sio Ujasiriamali.

Business skills kama vile Marketing, Business planing, Marketing planing, sales, Accounting na kadhalika hivyo ndo hufundishwa.

Huwezi fundisha mtu commitment, huwezi Fundisha Confidence.

UJASIRIAMALI NI WEWE KUJIKANA TU BASI.

So Mjasiriamali anahitaji Business skills ili kusonga mbele.

Na wale kama wanatoa Business skills kwa wajasiriamali nitawaelewa ila kama ni kuwafanya watu wawe wajasiriamali basi hakuna kitu hapo.

ILE NI BIASHARA TU KWA SASA NA IPO HADI VYUO VIKUU KWAMBA WANATOA DEGREE ZA UJASIRIAMALI ILA SASA WATAFUTE HAO GRADUATE WA UJASIRIAMALI KAMA HUJAKUTANA NAO POSTA WAKIWA NA VYETI WANASAKA AJIRA
 
Nianze kwa kuungana na wewe katika sentensi yako ya mwisho, Katika dunia ijayo, tena hasa kwa nchi yetu Tanzania, wanaoitwa wasomi au wanazuoni hawatosikilizwa tena.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba wamekuwa si watu wakutatua matatizo bali wameenda mbali zaidi na kuwa vyanzo vya matatizo hayo. Nikuulize tu Mkuu, unahisi miswada ya sheria kandamizi hapa nchini inaandaliwa na nani kama si hawa wanaoitwa wasomi wabobezi???

Nikija katika upande wa maswali yako.

Mwalimu ni mtu yeyote mwenye ujuzi wa jambo fulani, ambalo anawezakuwafundisha wengine. Unaweza ukaamua leo uanze kufundisha majirani zako jinsi ya kujiunga na kutumia JamiiForums kama chanzo chao cha kupata habari muhimu hapa nchini, wewe utaitwa mwalimu wa Jinsi ya kutumia JF.

Vigezo ambavyo watu wengi hutumia kubaini walimu na mentors ni kuangalia mafanikio ya mwalimu pamoja na matarajio wanayoahidiwa kuyapata baada ya kufundishwa ujuzi huo. Watu wengi hukwama hapa, Mentors karibia wote hapa nchini, wamejifunza copywriting na selling. Hii huwafanya kuweza kuwa na ushawish mkubwa lakini ukweli ni kwamba wengi wamekariri tu yale wanayofundisha, hii ndio sababu ukisoma vitabu vyao karibia wote utagundua ni tafsiri ya maandishi ya wazungu. No innovation at all.

Mfano mzuri kuhusu hili, ni mentor fulani maarufu hapa nchini. Wiki hii nilimu-unfollow baada ya kugundua kwamba anafanya plagiarism kutoka kwa James Clear. Kama mnafuatilia alipost makala kuhusu Pareto rule.

Mentors wa hapa nchini hupatia zaidi katika kutoa hamasa kwa watu, hasa wale waliokata tamaa na kujiona kumbe they can still make something. Kwa upande wa pili hukosea katika kufundishia mifano isiyokuwa na uhalisia hapa nchini. You can name few.

Kuhusu suala la serikali kuingilia kati sidhani kama ni wazo zuri, kwani liccha ya walimu wengi kuonekana kutokidhi vigezo bado kuna wanafunzi wachache ambao hufanikiwa kutokana na kile kidogo wanachofundishwa.

Jambo la msingi, tunaweza kuanzisha platform. Lets say website ambayo itakuwa ikitoa reviews kuhusu hawa watu. Hii itasaidia kuwatambaua waliobora miongoni mwao.
Umenena vyema ndugu
 
Kwanza tambua kwamba Ujasiriamali haufundishwi. Kokote kule. Ujasiriamali ni hari.

Ujasiriamali ni sawa na Mapenzi. Je usha ina chuo cha kufundisha watu kupenda?

Kufall in love ni spirt na huwezi kuifundisha.

Wanao enda kutafuta Elimu ya Ujasiriamali ni kutaka kuficha uoga na pia ni kujiongezea uoga tu na pia hakuna Chuo cha Kufundsha ujasiriamali.

Vipo vyuo vya kufundisha Business skills na sio Ujasiriamali.

Business skills kama vile Marketing, Business planing, Marketing planing, sales, Accounting na kadhalika hivyo ndo hufundishwa.

Huwezi fundisha mtu commitment, huwezi Fundisha Confidence.

UJASIRIAMALI NI WEWE KUJIKANA TU BASI.

So Mjasiriamali anahitaji Business skills ili kusonga mbele.

Na wale kama wanatoa Business skills kwa wajasiriamali nitawaelewa ila kama ni kuwafanya watu wawe wajasiriamali basi hakuna kitu hapo.

ILE NI BIASHARA TU KWA SASA NA IPO HADI VYUO VIKUU KWAMBA WANATOA DEGREE ZA UJASIRIAMALI ILA SASA WATAFUTE HAO GRADUATE WA UJASIRIAMALI KAMA HUJAKUTANA NAO POSTA WAKIWA NA VYETI WANASAKA AJIRA
Mkuu nakubaliana na wewe kuwa ni ngumu sana kumfundisha mtu ujasiriamali
Lakini kuna vyuo vinatoa degree za ujasiriamali hata hata Tanzania chuo
Ipo masters of science in Entrepreneurship
Pia ipo Bachelor of business adm and entrepreneurship development
Je hawa wanakosea kuwafundisha watu ujasiriamali?
 
Ujasiriamali haufundishwi.
 
Mtoa uzi naanza kupata mashaka na wewe, huenda ukawa ni moja ya hao wanaojiita malife coach, motivational speaker, mentor n.k maana naona unatafuta dondoo hapa kwetu, pia uandishi wako unasadifu (unaandika Sana)
 
Tunaweza kupata kitu kutoka katika mwongozo huo nimeweka kitabu kwa mujibu wa serikali. Hard copy waweza kupata pale ofisi za NEEC
IMG_20181216_112915.jpeg
View attachment NETF-KISWAHILI-book-pdf2.pdf
 
Mtoa uzi naanza kupata mashaka na wewe, huenda ukawa ni moja ya hao wanaojiita malife coach, motivational speaker, mentor n.k maana naona unatafuta dondoo hapa kwetu, pia uandishi wako unasadifu (unaandika Sana)
Haa haaa haoan mkuu mimi siko miongoni mwa watu hao na wala mimi sio mjariamali bali mimi ni mfanyabiashara na mtaalamu kwenye fani yangu

Point yangu kubwa ni kuona namna ya kutambua hawa watu kwa sababu wimbi la vijana walio wengi wanawasikiliza na kusahau kufanya mambo ya msingi
 
Kweli kabisa tuzidi kufanya vitu real na siyo kuimagine.
 
Back
Top Bottom