Kuongezeka na kupotea kwa fedha mtaani na wakati sahihi wa kuchukua hatua

Benittotz

Member
Joined
May 24, 2018
Posts
68
Reaction score
123
KUPANDA NA KUPOTEA KWA FEDHA MTAANI NA WAKATI SAHIHI WA KUWEKEZA.

Mzunguko wa fedha unahusisha fedha zote zilizopo kwenye mzunguko za noti na sarafu,zilizopo kwenye mikono ya watu na zilizopo banki. Jumla ya fedha hizi inapopungua mtaani au kuongezeka huleta athari chanya au hasi kutokana na mabadiliko haya ,hasa kiuchumi. Watu wengi utawasikia mtaani wakisema saivi hakuna hell,ziko hazina,au hazina hakuna fedha ndio maana mtaani Hali ni ngumu. Lakini ukweli ni kwamba uwepo au kutokuwepo kwa fedha hazina au mtaani sio jambo la bahati mbaya. Ni mipango na utekelezaji wa Sera za kifedha ambazo husimamiwa na banki kuu.

Sera hizi zilizogawanyika sehemu kuu mbili huwa zinatumika kwa madhumuni ya aidha kupunguza ukosefu wa ajira na kuongeza uwezo wa mlaji wa mwisho au kuongeza thamani ya fedha na kunyanyua mapato ya serikali kupitia makato ya kodi, uuzwaji wa hisa , ongezeko la riba ya mikopo na kadhalika. Pindi fedha inapoongezeka kwenye mzunguko manunuzi houngezeka kwakuwa mlaji wa mwisho ana fedha ya ziada na anaweza kuyamudu, ajira na fursa mpya huongezeka pia. Hali ya maisha ya watu huwa bora na uchumi wa nchi hunyanyuka. Hata hivyo madhara ya kuongezeka kwa fedha mtaani kupita kiwango kinachohitajika hupelekea uhitaji kuzidi uzalishaji na thamani ya fedha kushuka hivyo mwishowe kunatokea mfumuko wa bei.

Upande wa pili ni kwamba fedha inapopungua kwenye mzunguko lengo kuu huwa ni kuongeza thamini yake na kuthibiti mfumuko wa bei. Kuongeza mapato ya serikali . Vivyo hivyo fedha inapopungua kupita kiwango kinachohitajika hupelekea ukosefu wa ajira, kushuka kwa mauzo na uzalishaji kwa kuwa nguvu ya mlaji wa mwisho ni ndogo lakini pia huchangia Hali mbaya kimaisha kwa wananchi husika.

Namna bora ya kuongeza na kupunguza fedha mtaani ni kuuweka mlinganyo huu katika usawa. Na hii ndio changamoto kubwa kwakuwa Mara nyingi huwa vigumu kwa wizara husiku kujua NI kias gan sahihi cha kupunguza au kuongeza katika mzunguko pasi kuleta madhara hasi.

ZIFUATAZO NI NJIA AMBAZO HUTUMIKA KUTHIBITI MZUNGUKO WA FEDHA, SABABU YA KUFANYA HIVYO NA NAMNA UNAVYOWEZA KUONA FURSA KATIKA MABADILIKO HAYA.
1 SERA YA FEDHA INAYOHUSISHA FEDHA ZISIZOTOKANA NA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI .
(EXPANSIONARY AND CONTRACTIONARY MONETARY POLICY)
√ SOKO HURIA. Serikali inapohitaji kuongeza fedha katika mzunguko moja kati ya njia zake kuu ni kuuza hisa zake katika soko huria. Hisa hizi huuzwa kwa mashirika binafsi na mtu mmoja mmoja. Kwa kununua hisa hizi tunakua tumezitoa fedha mifukoni mwetu na kuziweka mfukoni mwa serikali. Hisa hizi huwa zimekadiriwa muda wa kuiva kulingana na muda fedha hizo zinapaswa kupungua mtaani ili kuboresha thamani yake. Pindi mambo yanapokuwa shwari na serikali ikaona umuhimu wa kurudisha fedha mtaani basi hurudi na kununua hisa hizi. Hii ikiwa na maana kuwa fedha wakati huu zinatoka kwa serikali na kuja kwetu,hivyo kupelekea fedha kuongezeka kwenye mzunguko.
Njia hii huwanufaisha zaidi wenye kipato Cha juu na wachache wenye kipato Cha Kati. Kwa kushiriki kununua hisa hizi ambazo huwa na riba hivyo kuja kuziuza katika faida muda wake unapofika.

√ KIWANGO CHA MWISHO CHA AKIBA KWA BENKI ZA KIBIASHARA. Kila banki nchini iko chini ya benki kuu. Benki kuu huweka kiwango cha mwisho ambayo kila benki inapaswa kuwa nacho kulingana na idadi ya wateja ili kukidhi mahitaji ya kila siku ya wateja wake. Pindi serikali inapohitaji kupunguza fedha mtaani huziagiza benki hizi kupitia benki kuu kuongeza kiwango cha mwisho cha akiba. Hii hupelekea benki hizi kuwa na kiwango kidogo kilichobaki kwa mahitaji ya kila siku ya wateja pamoja na shuhuli zake za kibiashara kama vile utoaji wa mikopo na ujenzi wa majengo ya kibiashara. Hali hii huwaathiri wafanyabiashara wanaohusisha miamala mikubwa kwa kuwa masharti na viwango vya utoaji fedha huongezeka na kuwa vigumu zaidi. Hivyo hulazimika kutafuta njia mbadala ya kufanya miamala ya kibiashara bila kutumia benki hizi.
Hii inaweza kuwa fursa kwa mashirika ya mitandao yanayojihusisha na huduma za kifedha endapo yataamua kuongeza kiwango cha miamala yao,kuboresha ulinzi na kulegeza masharti yao kidogo.
Pindi serikali inapohitaji kuongeza fedha mtaani kwa njia hii basi benki kuu huagiza benki hizi za kibiashara kupunguza kiwango cha mwisho cha akiba hivyo kurahisisha benki hizi kuhudumia idadi kubwa zaidi na kujihusisha na shughuli zinginezo za kiuchumi.
Fursa ya kupata mikopo Kama mitaji ya biashara kwa watu wa madaraja yote huongezeka. Ni rahisi pia kupeleka mapendekezo ya kibiashara na kuomba ubia na benki hizi kwa wakati kama huu.

√USIMAMIZI WA MIKOPO. Katika njia hii benki kuu huziamuru benki za kibiashara kuongeza kiwango cha riba na kupunguza kiwango cha utoaji mikopo Hali inayopelekea kupungua kwa kiwango cha fedha mitaani.
Kwa kuwa wawekezaji na wajasiriamali watashindwa kupata mikopo au kupata mikopo kwa riba nafuu kutoka katika mabenki,huu huwa wakati mzuri kwa taasisi zinazojihusisha na utoaji mikopo binafsi kupata faida kwa kutoa mikopo nafuu ambayoni wazi itakua kimbilio la wengi. Angalizo hapa ni kuhakikisha mkopaji ameweka dhamana inayoridhisha kwa kuwa kama Hali ya uchumi itazidi kushuka kutoka na ukosefu wa fedha mtaani ni wazi mikopo mingi haitalipika hivyo uuzwaji wa dhamana hizi utaaaingizai taasisi husika faida maradufu.
Vivyo hivyo ili kuongeza fedha mtaani benki hizi huamuriwa kupunguza kiwango cha riba na kuongeza mikopo kwa kurahisisha masharti. Hivyo wawekezaji na wafanyabiashara wengi hupata mikopo hii kiurahisi na biashara nyingi huchanua.
Huu ni muda mzuri wa kuanzisha na kukuz biashara kwakuwa vitu vingi vitakuwa vinapatikana kwa bei nzuri na yenye faida. Pia tatizo la mtaji hutatulika kwa urahisi kwa kuwa ni rahisi kupata msaada wa kifedha katika wakati huu.

√AMANA MAALUMU.Benki zote za kibiashara huwa zinatakiwa kuwa zimeweka kiasi fulani Cha fedha benki kuu. Mara nyingi kiasi hiki huwa ni 10% ya mtaji wao. Pindi serikali inapohitaji kupunguza fedha mtaani huongeza kiwango hiki. Hi ikiwa na maana kuwa mtaji unafanya kazi wa mabenki haya hupunguzwa kwa asilimia fulani,kwa kuichukua asilimia hiyo na kuiweka benki kuu. Athari za kupunguza mitaji ya kazi ya benki hizi ni Kama ile ya kiwango cha mwisho Cha benki za kibiashara. Benki hizi hupungua uwezo wa kuhudumia wateja kuanzia kwenye viwango na ukubwa wa mialama mpaka kwenye mikopo na shughuli za uwekezaji. (Benki nyingi huwekeza kwenye majengo ya kibiashara)
Kinyume Cha oungezwaji wa kiwango hiki huwa ni upunguzwaji. Serikali hufanya hivyo inapohisi kunauhitaji wa kuongeza fedha katika mzunguko. Kwa kupunguza kiwango kinachotakiwa kuwekwa benki kuu,benki hizi huwa na nguvu kubwa ya kukopesha, kutoa huduma za kifedha na kujihusisha na miradi ya kibiashara hivyo kupelekea kustawi kwa uchumi na hali ya mtu mmoja mmoja katika jamii.

2.SERA YA FENDA INAYOHUSISHA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI.
(EXPANSIONARY AND CONTRACTIONARY FISCAL POLICY).
√MATUMIZI YA SERIKALI.
Serikali inapojenga mabarabara, shule,hosipitali na kadhalika huwa inatoa ajira nyingi sana za msimu katika maeneo husika. Kuanzia kwa wakandarasi,wauzaji wa vifaa vya ujenzi hadi vibarua. Lakini pia hutoa fursa kwa wafanyabiashara wadodo wadogo Kama mama ntilie wanaouza vyakula maeneo haya ya kazi na kuongeza Pato kwa biashara ya nyumba za kulala wageni na biashara zinginezo. Hivyo kwa kuongeza bugeti ya matumizi katika huduma z kijamii serikali huongeza fedha katika mzunguko. Vivyo hivo huduma hizi zinapopungua au kutolewa na taasisi za kiserikali ni ishara ya kuwa serikali inapunguza fedha kwenye mzunguko.

√ KODI Ili serikali yoyote iweze kufanya miradi ya kijamii na kimaendeleo inahitaji kodi. Kodi ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa. Hata hivyo kodi hii Ina mahusiano ya moja kwa moja uchumi wa mtu mmoja mmoja hadi taifa kwa ujumla.
Serikali inapohitaji kuongeza thamani ya fedha mtaani na kupunguza mfumuko wa bei namna rahis ya kufanya hili ni kwa kuongeza kodi kwenye kipato. Ongezeko la Kodi hii humwacha mhusika na kiwakwango kidogo kwa matumizi hivyo kushusha uwezo wake wa manunuzi. Mahitaji yanaposhuka, muuzaji hulazimika kupunguza Bei ili mteja aweze kumudu na kunyanyua biashara yake Tena. Kushuka huku kwa Bei ilihali ujazo au ukubwa uko vilivile huashiria kupanda kwa thamani ya fedha.

Kwa kupunguza makato ya Kodi kwenye kipato, mlaji wa mwisho huwa anakuwa na nguvu kubwa ya kufanya manunuzi hivyo biashara hustawi na Hali za maisha kuwa bora. Ila hii hufanikiwa endapo tu , Kodi zimepunguzwa na Bei za bidhaa na Mambo mengine yako vile vile.
Ili kunyanyua biashara na kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira serikali wakati mwingine hupunguza Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye bidhaa ili kushusha bei ya bidhaa hiyo na kunyanyua mauzo yake. Matokeo yake huwa ni kuimarika kwa uchumi na kuongezeka kwa uzalishaji kunakopelekea ajira mpya na Hali Bora kwa watu.
√RUZUKU MAALUMU. Wakati mwingine serikali hutoa ruzuku kwa wahusika wa sekta fulani pale inapoonekana sekta hiyo inahitaji kukuzwa namchango wake katika kunyanyua uchumi ni mkubwa. Ruzuku hizi husaidia upatikanaji waahitaji muhimu kwa gharama nafuu. Utoaji wa pembejeo za kilimo umekua ni mfano bora wa ruzuku zitolewazo nchini ili kunyanyua sekta ya kilimo. Ruzuku hizi huwa na athari ya moja kwa moja kwenye jamii. Kwani kwa kuboresha uzalishaji Hali za kiuchumi hunyanyuka na kipato cha familia,mtu mmoja na jamii nzima huongezeka.


Jambo la muhumi na la kuzingatia ni kwamba mbinu hizi za kiuchumi hufanikiwa kuleta matunda endapo Hali ya Mambo mengine imebaki Kama ilivyo bila kubadilika. Kwa mfano ili engezo la mishahara na punguzo la kodi ya kipato liweze kuwa na tija, bei za mahitaji muhumu zinapaswa kutokupanda . Tofauti na hapo ongezeko Hilo halitakua na matokeo chanya.

Ni imani yangu kwa makala hii fupi Kuna Jambo moja Kama si mawili umejifunza,au ulikua unalifahamu ila sasa umelipokea na kwa namna nyingine iliyoongeza kitu kwako. Nakaribisha maoni,ushauri na marekebisho pale ambapo kuna taarifa unahisi haiko sawa.
Nitafurahi kusikia kutoka kwako.
Na.
BENSON FLEXON SHIRIMA
MHITIMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAMU,SHULE YA BIASHARA.
WHATSAP +255654859954
SIMU/MSG +255653384656
FACEBOOK: BENSON FLEXON SHIRIMA
INSTAGRAM; @BENITTO_TZ
TWITTER Benittotz.
 
Benittotz ahsante kwa bandiko zuri.

Kuna maeneo mengi yana utata ila mojawapo na la wazi ni hili hapa,
Umesema benki zikiongezewa kiwango cha kuweka pesa benki kuwa zinaongeza masharti kwa wateja wanaofanya miamala.

Sijajua unaziongelea benki zipi lakini sojawahi kuona au kusikia mteja mwenye pesa zake benki ameambiwa masharti yamebadilika tofauti na yale ya taratibu za kawaida zilizozoeleka.
Unaweza fafanua kidogo hapo?

TUTAELEWANA
 
Kuna kitu kinaitwa special deposit,banki zote za kibiashara zinapaswa kuweka kiwango flani benki kuu. Lakini pia ikumbukwe benki hutumia Amana za wateja kufanyia biashara zake Kama kukopesha na kujenga majengo ya kibiashara hivyo hali ya uchumi inapopelekea benki kubaki na kiwango kidogo Cha kujiendesha vikwazo huwekwa ili iweze kumuda wateja wengi na kufanya biashara zake kwa fedha zile zile za wateja. Hujaiona hii kwa kuwa uchumi haujafika uko ila unaweza kutazama haraka haraka kwenye ATM Kuna kiwango cha mwisho,kile NI kikwazo,ukitaka kuchukua cash nyingi bank Kuna taratibuu za kufata tofauti n mtu anaetoa 1,4,5 million,hicho NI kikwazo pia. Nadhan kidog umepata mwangaza hapa
 
Too theoretical....ingia mtaani na hizo stori zako kama hujakula za kichwa....hayo maelezo ni ya kujibia mitihani ya darasani hayana uhalisia wowote uraiani
 
Wew utakuwa umesoma BAE bila shaka,,,, mwanauchumi,,,,, ulikuwa unapambana na COSS pale mliman
 
Bcom in accounting mkuu. Bae walikua wanshare na sisi accounting na finance.
 

Kwenye ATM nakuelewa kwa sababu hata zenyewe zina uwezo wenye kikomo wa kuhifadhi pesa. Na ule mfumo wake pia una kikomo cha kutoa pesa kwa mara moja.

Vinginevyo wateja watatu wanaweza kupiga miamala mtambo ukakauka wakati lengo la ATM ni kusaidia wateja wakati hawawezi kuhudumiwa ndani.

Mwisho, hapo kwenye vigezo au masharti, sana sana utaambiwa utoe taarifa kwa muda flani kuhusu kusudio lako labkufanya muamala wa pesa ndefu lakini haiwezi ikawa kikwazo.

Hizo deposit bank kuu pamoja na mambo mengine, ni kulinda pesa/amana za wateja. Ndio maana zinaendana na ukubwa wa Benki husika.
 
Time is money ule muda fulani unaofatilia ni muda unaowatosha wao kupokea marejesho kibao ya mikopo na kukupa fedha unayohitaji bila kuathiri mzunguko wao. Sababu za kuweka special deposit mbali na security hutumika pia kuadjust uchumi chief. Fatilia vizur hili ugundu nachukuambia kiko sawa.
 
Sasa mbona sijaona way out ya hizo point zako...nilitegemea useme ili tuendane na hali halisi tufanye 1,2,3 but umeishia kutupa mtililiko tu wa hali inavyotakiwa kuwa bila kutupa njia tunazopaswa kufuata. Any way UDBS hukwenda kucheza umejitahidi na kiswahili fasaha pia.
 
Asante,itatoka article ya pili itakayo pick up hii ilipoachia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…