Kuongezeka na kupotea kwa fedha mtaani na wakati sahihi wa kuchukua hatua

Uchambuzi mzuri... Kny heading kuna maneno "...wakati sahihi wa kuwekeza".. Sioni kama umeelezea hili kny makala. Nadhani wakati wote ni sahihi kuwekeza, kutegemea aina ya uwekezaji/bidhaa
 
Uchambuzi mzuri... Kny heading kuna maneno "...wakati sahihi wa kuwekeza".. Sioni kama umeelezea hili kny makala. Nadhani wakati wote ni sahihi kuwekeza, kutegemea aina ya uwekezaji/bidhaa
Asante kwa feedback. Itakuja makala ya pili itakayoeleza kuhusu kuwekeza
 
Nimekuelewa tena baada ya ile post yako JINSI YAKUPATA MTAJI na hii pia mkuu.
 
Mkuu Benittotz hongera kwa uchambuzi,naongezea kitu kidogo pale ulipomjibu mwajf kuwa kuna special deposit ile pia inaitwa "Statutory Minimum Reserve(SMR)" ambacho ni kiwango kinachotakiwa kwa mabenki yote ya biashara kuweka amana Bank of Tanzania(BoT).Hii ina sababu kuu nyingi sana kiuchumi rejea kisa kufungiwa baadhi ya mbenki kama Efata Bank
 
Sure mkuu niliiandika Kama reserve requirements kwenye moja Kati ya points. Asante Sana kwa nyongeza
 
Tunaomba utuelezee majarida mbali mbali ya kiuchumi na fedha, Maana maswala ya fedha na uchumi yanakuwa magumu kwa watu wengi. Tena maswala ya kutunza thamani ya Pesa inakuwa ngumu kwa izi nchi zetu za dunia ya tatu
Swali langu ivi kwa nchi kama yetu Tanzania kuwa na nyumba za kupangisha na kuwa na kiwanda cha kuzalisha malighafi IPI? Ni uwekezaji wenye tija kwa nchi kama Tanzania
 
Uchaguzi wa Aina ya malighafi unahitaj kuprocess au eneo namna unataka kufanya biashara ya kupangisha ndio utachagua ipi kuwa Bora zaidi. Ingawa zote NI biashra zinazoingiza kipato kikubwa na zenye soko. Kwa mfano,mabadiliko ya kiviwanda kwa Sasa yatahitaji wingi wa malighafi hivyo ukiziona fursa unapiga hell,lakini pia ukuwaji wa viwanda unaenda sawia na wingi wa wafanyakazi ikiwa na maana wengi watatoka katika mazingira yao ya kila siku au majumbani kwao na kusogea karibu na maeneo ya kazi hivyo kuwezeka kwenye nyumba za kupanga karibu na maeoneo yao ya kazi inaweza kuwa wazo zuri pia . Nitaandika kwa mapana zaidi kuhusu hi mada katika makala zijazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…