Kuongezwa kwa muda wa maombi ya mikopo 2024/2025

Kuongezwa kwa muda wa maombi ya mikopo 2024/2025

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
1725109854472.jpg

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwafahamisha Waombaji wa mikopo na Umma kwa ujumla kuwa muda wa kuwasilisha maombi ya mikopo umeongezwa mbele hadi tarehe 14 Septemba, 2024.

Hatua hii imechukuliwa ili kuwapa fursa wale ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kufanya maombi ya mikopo katika muda uliokuwa umepangwa.

Itakumbukwa kuwa, awali Bodi ilianza kupokea maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao tarehe 1 Juni, 2024 na mwisho wa kuwasilisha maombi ulipangwa kuwa tarehe 31 Agosti, 2024.

Kupitia tangazo hili, waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2024/2025 ambao hawajakamilisha maombi yao wanashauriwa kukamilisha na kuwasilisha maombi yao ya mikopo ndani ya muda ulioongezwa.

Bodi inapenda kusisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe 14 Septemba, 2024.
.
 
Back
Top Bottom