bhikola
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,131
- 1,663
Habari wana Jamii,
Ninamshukuru sana Mungu kwa kunijaalia kuiona tena siku mpya.
Watu wengi wanapopatwa na matatizo ya kifedha, jambo la kwanza hufikiria ni kwasababu wanapata mishahara midogo. Ukiwauliza wafanyakazi walio wengi kuhusu njia bora ya kuboresha maisha yao, watakwambia ni kuongezewa mishahara, na hata wasio waajiriwa - hasa vijana wanaotoka mashuleni na vyuoni, ndoto yao kubwa juu ya kuwa na uhuru wa kipato hivyo kuwa na maisha mazuri watakwambia ni kupata kazi nzuri yenye mshahara mkubwa.
Changamoto ya jambo hilo ni nini?
1. Kuongeza mishahara kunaongeza gharama katika uzalishaji, kumbuka mshahara ni fixed cost, kwa hiyo ili kuongeza mishahara kuwe na tija ni lazima uzalishaji uongezeka. kwa mfano ukisema mishahara iongezeke kwa asilimia 10, kama ulikuwa unapata 1m utakuwa unapata 1.1m. lakini kutokana na kupanga kwa gharama za bidhaa zalishwa au hudumu, tunategemea pia kutakuwa na ongezeko la bei katika huduma ama bidhaa tajwa. Hivyo utajikuta uwezo wa mshahara wako kununua unapungua kuliko uliokuwa nao mwanzoni. maana umepata ongezeko la laki 1 lakini karibu kila huduma na bidhaa imepanda hivyo nyongeza ya ongezeko lake kwa mwezi ni zaidi ya 1k.
2. Mshahara ni moja ya njia duni kabisa za kupata kipato endelevu - sustainable earning, kwasababu mshahara unaupata ukiwa tayari umeshautumia ama kuupangia matumizi, lakini pia ukikoma kupata mshahara unakuwa duni zaidi. Angalia wastaafu tulio nao utaelewa naongea nini.
3. Kuongezwa mshahara kunaendana na kuongezeka kwa makato mbalimbali hasa yale yanayoendana na asillimia kama kodi, bima na mengine. So kuongezwa mshahara ni kuongezewa kiasi cha makato.
Tufanyeje sasa?
1. Tafuta njia ambayo itatatua matatizo yako ya kifedha - spend less on liabilities and more on assets
2. Punguza wategemezi, tunakulipa mshahara kwaajiri yako na mkeo au mmeo, na watoto 4 tu basi. sasa wewe unataka uwalipe mshahara mashangazi, wajomba, wajukuu, na ukoo mzima kijijini kwenu, it wont work.
3. Ongeza kipato kwa kufanya uzalishaji wa vitu vidogovidogo vya kutumia nyumbani. kwa mfano badala ya kuhangaika na mayai, fuga kuku hata 5 tu utatatua tatizo la mayai kwako. Badala ya kuhangaika na mboga, lima matuta 2 tu nyumbani kwako utapata mboga mboga angalau kwa uchache.
4. Budget fedha zako vizuri, na ufuate bajeti yako. tatizo watz wengi hatuna budget
Kwa leo ni hayo tu.
J3 njema, na Mungu awabariki..