Kuosa mpangilio wa hedhi msaada tafadhali

Doly

Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
16
Reaction score
2
Hongera kwa majukumu na pole kwa uchovu wa wikiend.

Mie ni mwanamke wa miaka thelathini na mmjo 31). Nimevunja ungo nikiwa na umri wa miaka 16 na nikiwa kidato cha tatu. Sasa tangu nivunje ungo sina kabisa mpangilio mzuri kwani inafika wakati nakaa hata miezi sita bila kupata hedhi, na kuna wakati nilikuwa nikipata inakuwa ni mfululizo hata zaidi ya mwezi mmja na ikikoma ndo hivyo tena. Nimeenda hospitali mbalimbali wakanambia eti labda hadi nipate mtoto nikaamua nizae lakini shida inaendelea japo kwa sasa haifiki mwezi labda kati ya ck 3 na kumi hivi. Ila nikishapata hedhi kwa mfano mwezi huu sijui tena nitapata. Na sijawahi kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango labda kuna miezi itatu ambayo nilitumia vidonge ambavyonilipewa hospitali kama tiba.

Tafadhali naumia sana naombba nisaidiwe kwani inafika hata wakati najihisi sipo sawa na watu wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…