jamadari
JF-Expert Member
- Feb 13, 2010
- 295
- 92
Siku hizi watu wengi wanapenda kuonekana vijana, kuanzia kwa watu mashuhuri hadi kwa watu wasio mashuhuri, hakuna mtu
anayetaka kuzeeka. Tafiti zinaonesha kuwa kuna baadhi ya matendo ambayo waweza kufanya au kuyaepuka huweza kukusaidia kupunguza au kukufanya uonekana mzee kabla ya muda.
Baadhi ya matendo yanayoweza kukufanya usionekane mzee harraka ni kama; kulala chali, kula kwa wingi samaki wa jamii ya salmoni,
kujiupusha na mionzi ya moja kwa moja ya jua, kutovuta sigara na mengineyo. Lakini je unafahamu kuwa kuosha sana sura yako
hukufanya uonekane mzee?
Tafiti zinaeleza kuwa, maji huondoa unyevunyevu (moisture) na mafuta ya asili yanayoilinda ngozi ya sura na mikunjo inayokufanya
uonekane mzee. Hivyo, kuosha uso mara kwa mara pia huosha unyevunyevu huu.Hivyo unashauriwa kuwa kama una ulazima wa
kuosha sura mara kwa mara, basi tumia sabuni zilizo na unyevu (moisturizers)
Chanzo. Kuosha uso mara kwa mara hukufanya uonekane mzee