Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
-
- #121
Aajhajhajhajhajhajhajhaaaaaaa........haya sasa. Mwenyewe hatimaye kasema.
Watu mlienda mbaaali na mawazo yenu ya ngono kumbe mwenzenu anazungumzia chores za nyumbani. Walimwengu bana….yaani fikra zao ziko kwenye mambo machafu machafu tu. Teh teh teh
kuna mahali imewahi kusemwa kuwa wanaume hufikiria mambo ya ngono kila baada ya sekunde tisa/kumi; sasa kwa Watanzania kwa ujumla kuna uwezekano kuwa tunafanya hivyo chini ya muda huo. Mti akisema "siagi" mtu anafikiria ngono, mtu akisema "dodoki" mtu anafikiria ngongo, tukisema "samli" basi ni yale yale.. utadhani tunaishi katika ulimwengu wa mafumbo ambapo jukumu letu ni kuyafumbua kila tunaposikia.
Hahahaaa wee acha tu manake watu walikuwa wanakuja renditions zao chafu chafu na za ajabu ajabu sijui hata kwa nini wakati wangeweza kumuuliza Mzee mwenyewe kama tulivyofanya wengine. Lol
Vyombo hivi siyo vile
Vya huku siyo kule
Vya jikoni siyo pale
Vyombo vile vya kulia!
Vyombo siyo vya sirini
Vyombo vile vya mezani
Siyo vya kule chumbani
vyombo vile vya jikoni!
Siyo vyombo vya gizani
Vilivyong'ang'ana mwilini
Vya vyakula vya gizani
Vyenye kuliwa shukani
Vyombo hivi ni sahani,
Na vijiko vya mezani
Sufuria za jikoni
Bakuli za kabatini!
Mlivyonavyo mawazoni
Silo niwaulizeni
Sijui tatizo nini
Mmewaza ya chumbani!
Mkisha kula pamoja
Vitamu tena vya haja
Mtaosha kwa pamoja
Au aoshe mmoja?
Swali nawaulizeni.
M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
halafu wewe pia naona ulichanganya mambo, ha ha...huyu mzee nae tatizo alikuwa anategea na kuwasoma watu kwa fikra zao, halafu ndiyo anatupa jibu baada ya mchanganyiko ule!!..uoshe vyombo na wewe NN siku moja moja!!
We Nyani,, sasa kuna fumbo gani hapa?
Aisee kweli bana. Nisingemtilia mashaka pale mwanzoni nadhani wengi wasingepeleka huko walikozipeleka fikra zao.
Na mimi wala si mchoyo wa ushirikiano. Napika, napakua, natenga, naosha, na kuvipanga vyombo kabatini.
Aksante kakaSijui nisikitike au sijui nishangae manake watu moja kwa moja walirukia huko kwenye hayo mengine wakati mzee wa watu unaongelea mambo ya kusaidiana chores za nyumbani.
Mapenzi ni kusaidiana bana. Siyo kila siku mpishi huyo huyo, mpakuzi huyo huyo, na mfuta meza huyo huyo na muosha vyombo huyo huyo. Khaaa….mapenzi gani sasa hayo? Huo ni utumwa na wala sio mapenzi.
</p>Inatakiwa kuwa makini sana pindi unapo jibu hii kitu lasvyo kama ni mwanaume basi utaingia choo chakike na kama ni mwanamke utaingia choo cha kiume.....wela welaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa///mambo ya malavidavi hayo mmekula wote halafu kuoshaaaaaaaaaaaaaaaaa ........
That one there just sounds wrong dude!!!
</p>hakuna neno,vyombo nitaosha tu mwenyewe,na yeye ajue tu kuna majukumu fulani fulani,unless ye hayupo sitafanya....!!!
Aksante kaka
Mwanakijiji
Ingawa nadhani Mwanakijiji naye amechangia .....ukiona swali lako halieleweki na wengi ujue hata mtungaji naye kakusudia!!
But kama unamaansha vyombo vya jikoni ...mh!! Yangu maswali ni mengi
1.
Katika mapenzi suala la zamu huwa hakuna...........kama unanipenda utajisikia tu kufanya pamoja kama si kunisaidia kile nikifanyacho....kunisaidia kuosha vyombo si lazima ushike maji!! Kaa pembeni ya sinki nitizame nikiosha....shika nyonga, busu shingo nitaridhika na nitaosha bila lalamiko. Ni sawa na kufua pants za mwenza.tusiichukulie kama ni wajibu wa mke la hasha ni vilel nakupenda and am happy to do it whole heartedly......The same na kuosh vyombo usitegemee nikupangie zamu
2. Kwa maisha yetu ya uafrika ambako mfumo dume umetawala na hata wale ambao wanajiamini kuwa hawako kwenye mfumo dume bado kuna aspect za mfumo dume ambazo zimewatawala likiwemo la kushare domestic chores........bado ni ngumu. Sipati picha kumwambia mwandani wangu eti........Hun unajua leo ni zamu yako kuosha vyombo!! amerudi saa ngapi toka huko kwenye viti virefu na washkaji?? mi nafikiri bado saaaana kufikia huko...na
3. Je hapa unazungumzia kapo changa isokuwa na watoto au ndugu wengine wanaoishi nao au? kuwa baba ana zamu ya kuosha vyombo vya nyumba nzima???
Mwanakijiji hebu nisaidie.
Sijui kama ni swali la kizushi au uchokozi: Wote mlikuwa na njaa, mkaenda jikoni na mkapika kwa kushirikiana vilivyo na mkakipenda chakula. Mkakaa chini mkala kwa furaha zote na kuteremshia na mvinyo kidogo. Baadaye mmoja ndiye anatoka na kuanza kuosha vyombo. Hii kweli ni sahihi? Ni lazima wakati wote mshirikiane na kuosha vyombo kama mlivyoshirikiana kupika na kula? Ni swali tu.
Hehehe MwanajamiiOne na wewe bana mfukunyuziiii.
Tatizo watu wengi hatuna subira. Tukiona kitu tu basi tayari tunajenga picha na kufikia hitimisho. Ndiyo maana nikamwuliza.
Sasa inawezekana kweli Mwanakijiji kaandika hivyo kwa makusudi kabisa (knowing him, I can't put anything past him lol) lakini kwa vile keshasema alichokuwa anamaanisha kwangu mimi utata umekwisha.
Huyu lazima atakuwa hauzigeli tu anabembeleza kazi lol...Je, na yule anayekosha chombo kabla hajapakua, ni hila au tabia?
<p></p>
<p> </p>
michele bwana,acha kunchekesha,majukumu gan tena na jamaa keshakula labda kama unataka msubiri mle tena alafu umwambie this time is your turn kuosha vyombo.kuna mtu kasema anamlipa house girl kwa nn yy aoshe vyommbo. tuwe makini na mwanakijiji.
hope mnakumbuka lili shairi la sijui,sipati picha kama ****** analijua.