Kwa uongo hujamboKweli bwana hata mimi nishawahi kuota hivyo mpaka nikajiuliza au niliingiwa na pepo la kiinglish
Asubuhi hii nimemsikia mwendesha kipindi LULU ZA KISWAHILI,TBC akisema kama we in Mswahili,hujui Kiingereza huwezi kuota kwa Kiingereza!
Naomba kutofautiana naye: Mimi naongea Kiingereza kwa kiwango cha chini( kadri),lakini kuna nyakati naota nikiwa kwenye mikutano,naongea Kiingereza cha hali ya juu(nagundua hilo baada ya kuamka na kukumbuka ndoto hiyo,na hata kuangalia kwenye dictionary yale maneno magumu niliyoyatumia ndotoni)
Kumbe kuota kwa Kiingereza inawezekana!