Kuota umebeba maiti kwenye gunia ina maana gani?

Kuota umebeba maiti kwenye gunia ina maana gani?

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Leo nimeota ndoto kama ifuatavyo.

Nimeota nimebeba maiti ya mtu aliyeuliwa nilikuwa nimebeba kwenye gunia.

Cha ajabu hiyo maiti sijui hata nani alimuua hata huo mwili siijui cha ajabu nilikuwa nabeba nachoka nilikuwa nimeambatana na rafiki yangu lakini cha ajabu rafiki yangu alikua hataki kunisaidia kubeba aliniacha nibebe mwenyewe na kwamba eti nilikua napeleka mahali ukazikwe japo sijui ni maiti ya nani.

Hii ndoto ina maana gani? Huwa sioti ndoto za ajabu ajabu kabisa lakini nimeota hivi.
 
Uliangalia muvi gani siku nne nyuma?
 
Siku ukiacha kuikashfu Israel hutaota tena hizo ndoto

Usipotubu utaendelea kuota mauza uza tuu
 
Unatumika na wachawi kubeba maiti na vitu vyao Kupeleka sehemu.

Sijajua imani yako ikifika katika hali kama hii unafanyaje.

Kumpokea Yesu kuwa bwana na mwokozi katika maisha yako.

Hakuna njozi ya kawaida hapo Pharaoh aliota ikawa, Yusuph aliota ndoto ikawa. ndoto zinakuwa dhahiri

Wakati Mwingine ndoto zinasababisha na uchovu wa Siku lakini kwa ndoto yako kuna jambo
 
Dalili nzuri za kuwa Utapata pesa hivyo endelea kukaza haijalishi magumu kiasi gani unapitia na jinamizi la kukata tamaa linakuzunguka kila kukicha lakini pesa ipo karibu inaweza kuwa ya aina yoyote ile.....
 
Nimeambiwa hivi na zaidi ya watu watatu kama tafsiri yake

Asante sana
 
kwa tafsiri ya haraka haraka ni kua
kiroba ulicho kibeb kile ni Nchi ya Iran na maiti iliomo mule ni Ayatollah yaaan israel kawapelekea moto tehran ime teketea bwana msemaji
 
kwa tafsiri ya haraka haraka ni kua
kiroba ulicho kibeb kile ni Nchi ya Iran na maiti iliomo mule ni Ayatollah yaaan israel kawapelekea moto tehran ime teketea bwana msemaji
Hahaha nimecheka daah
 
Back
Top Bottom