Kuota umerudi shule uliyosomea

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
Tofautisha Ndoto hizi mbili!!
Kuota umerudi shule uliokua unasomea, na kuota ukiwa umeenda shule tena.

Kuona umerudi shule uliokua unasomea inamaanisha Kuna roho nzito imetumwa kurudisha mambo yako nyuma, au maagano yaliyofanyika kinyume chako ukiwa shuleni yanakuandama kukurudisha nyuma.

Pia ukiota umerudi shule uliokua unasomea huwa inamaanisha umewekewa Laana, au kifungo Cha kukuweka mahali pamoja Katika maisha...

Maana ingine ya Ndoto hii ni kushindwa Katika jambo unayoyafanya na kurudi nyuma kimaisha...
➡️Kama ulikua umepanga kupata ndoa inashindikana.
➡️Kama ulikua umepanga kupata kazi inashindikana.
➡️Kama ulikua umepanga kufanya biashara inashindikana.
Yaani mipango yako inashindikana na unarudi nyuma kimaisha.

Nakuombea maroho yote yanayokuletea Ndoto za kurudi shule uliosomea zishindwe Katika jina la Yesu.
LEO NANENEA MTU NENO LA KINABII UFUNGULIWE..PASTOR Vincent Kamadi Nakuru, 0758 869224...Isaiah 42;22....njoo tuombe, na ulete Ndoto inayokutatiza ,God speaks through dreams...
 
Nilivyokuwa chuo, niliwahi ota niko shule, halafu ticha mnoko alikuwa akitupa bakora za kufa mtu
😛

Lakini sema siku hizi, walimu wa vile hawapogo tena. Walimu walikuwa na uchungu na wanafunzi yaani mpaka unashangaa
 

Sikusoma mpaka mwisho.
Hayo maagano mnayodanganyana kila kukicha ndiyo mwanzo wako wa kushindwa kuganikisha mambo yako. Maana umekuwa umejawa na woga uliopitiliza.
Hapa duniani hakuna maagano, zaidi ya bidii/juhudi, maarifa, consistence, kumcha Mwenyezi Mungu, maisha ya middle class + utayapata tu. Achana kushinda kwa minabii ya uongo inayowaibia watu
 
Sioni Tatizo la kupata kumbukumbu zako za zamani na jamaa zako ulikuwa nao wakati mwingi shuleni... Kwasisi TULIOSOMA boarding school ni ngumu kutoota kumbukumbu zako ukiwa shule
 
Nadhani watu uota wapo shule sababu

Shule zilikuwa ni gold days mostly

Nadhani unakumbuka vitimbwi vingi ulipo kuwa shule

Kuliko vitimbi ambayo umekutana navyo kwenye utafutaji

So matukio yana rewind sometime mimi pia nilikuwa naota ndoto hizo lakini for I don’t care na mambo yanaenda mbona
 
Niliwahi kuota ndoto nimerudi shule, ni ndoto ambayo ilikuwa ni real kabisa, kweli huo mwezi nilirudi sana nyumba, kazi zilikuwa ngumu, nilikuwa sipati pesa kabisa na nikipata inayeyuka, hufanyi kazi hupati pesa.

-Nataka kufahamu, hizo ndoto ni mpango wa shetani au ni Hila za wanadamu?

-Kingine naomba kufahamu ni Aina gani ya masharti ya kikrosto ambayo hayatarudisha Tena hii ndoto.
 
Binadamu ambaye akili yake inafocus na Mambo ya mbeleni hawezi kuwa na wingi wa mawazo kipindi cha nyuma. Ubongo wa mwanadamu unacopy millions of information Kwa siku, siyo rahisi Kwa mwanadamu kukumbuka maisha ya nyuma wakati akili yake imefocus na Mambo ya mbeleni.

Huwa siyo rahisi huwa inakuja automatically.
 
Inaweza kuwa unajua kuna muda imani ya unacho kiamini ndicho kinakutokea

Umeota umerudi shule basi siku nzima unawaza basi nimerudi nyuma kiasi fulani

Naota nimerudi shule na nina endelea na mambo yangu as usual na hakuna kitu kinachange

Sisemi kuwa hakuna uchawi no uchawi upo
Ila namaanisha sidhani kama kila ndoto zinakuwa na maana sawa kama watu wengi wanavyo zipatia maana
 
Ndoto utoka kwa Mungu pia kwa shetani pia ni reflection ya yale uliyoyaona mchana.
Kuzitafsiri hizi ndoto ni lazima uwe na elimu ya ndoto au utafute wataalamu wa ndoto.
Kabla ya kupata na lolote jema au baya huwa ujumbe unaanza kwenye ndoto na ukiona ndoto inajirudia rudia ina ujumbe ndani mwake
 
Siyo kila ndoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…