Kuota vinyama sehemu ya haja kubwa

Kuota vinyama sehemu ya haja kubwa

bejamini

Senior Member
Joined
Sep 13, 2013
Posts
121
Reaction score
13
Wakuu heshima kwenu. Naombeni kufahamishwa chanzo halisi na tiba ya tatizo la kuota vinyama sehemu ya haja kubwa, Tatizo hili huambatana na maumivu yanayovuta na kuachia kama vile una kidonda au jipu linalotunga usaha kimaumivu. Je kuna dawa ya kutumia pasipo kufanyiwa operesheni na mtu akapona kabisa?? Naombeni msaada kwa kuzingatia mazingira pia ya kitanzania( hofu yangu ni kukomaa kwa tatizo hadi mtu kulazimika kupelekwa ughaibuni).

Msaada tafadhali
 
wakuu heshima kwenu. naombeni kufahamishwa chanzo halisi na tiba ya tatizo la kuota vinyama sehemu ya haja kubwa, Tatizo hili huambatana na maumivu yanayovuta na kuachia kama vile una kidonga au jipu linalotunga usaha kimaumivu. Je kuna dawa ya kutumia pasipo kufanyiwa operesheni na mtu akapona kabisa?? Naombeni msaada kwa kuzingatia mazingira pia ya kitanzania( hofu yangu ni kukomaa kwa tatizo hadi mtu kulazimika kupelekwa ughaibuni), Msaada tafadhali

ngoja wataalamu wafike humu utajibiwa
 
Haemorrhoids ni uvimbe ambao unaweza kutokea katika njia ya haja kubwa (mkundu)na sehemu ya mwisho ya puru(rectum). Kuna mtandao wa veins ndogo (mishipa ya damu) inayopita ndani ya mkundu na sehemu ya chini ya rectum. Hizi veins mara nyingine zinakuwa pana na kujaa damu zaidi kuliko kawaida. Mishipa hii iliyoja damu pamoja na tishu zilizojuu yake inaweza kufanya uvimbe mmoja au zaidi uitwao haemorrhoid.
Sababu halisi kwa nini mabadiliko haya hutokea na kusababisha haemorrhoids hazijulikani. Hata hivyo, inadhaniwa kwamba shinikizo(pressure) katika ama karibu na mkundu inaweza kuwa sababu kubwa katika kesi nyingi. Kama shinikizo katika ama karibu na mkundu limeongezeka, basi ni wazi kwamba hii inaweza kusababisha haemorrhoids kutokea Baadhi ya sababu zinazopelekea hali hiyo ni
-kufunga choo ama kupata choo ngumu
-ujauzito
-sababu za kiurithi-baadhi ya watu wanaweza kuwa na kuta dhaifu
Dalili
Dalili zinaweza kutofautiana. Haemorrhoids ndogo kwa kawaida haina maumivu. Dalili ya kawaida ni kutoka damu baada ya kwenda choo. Haemorrhoids kubwa huweza kutokwa majimaji kama makamasi, maumivu kiasi, kuwasha, na kujikuna. Unaweza kuwa na hisia za haja kubwa , au hisia ya kuwa bado unahitaji kwenda haja kubwa hata baada ya kujisaidia.Wakati mwingine damu huganda kwenye haemorrhoids na hivyo huleta maumivu makali. Maumimu haya hudumu kwa siku kadhaa lakini baadae hukoma.
Matibabu
Hakikisha unapata choo la laini wakati hivyo unaweza kufanya yafuatayo.
-Kunywa maji mengi
-kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi mfano matunda mboga za majani na vyakula vya nafaka.
-Epuka dawa za maumivu zenye codaine mfano
-Nenda chooni mara tu unapohisi haja.Usijaribu kubana.
Njia hizo zote hapo juu zitasaidia kupunguza dalili mfano damu kuacha kuvuja.
Hata hivyo kuna dawa nyingine ambazo unaweza kupaka amu kuingiza kwenye mkundu. Dawa hizi hazimalizi tatizo bali husaidia kupunguza dalili.
Matibabu mengine ni upasuaji ambayo inaweza kuwa kufunga(banding)au kuondolewa(haemorrhoidectomy).


ukisoma hapo hijaridhika mkuu pitia na hapa uelewe zaidi https://www.jamiiforums.com/jf-doct...yama-sehemu-za-siri-bawasiri-hemorrhoids.html
 
daa asee, hili ni tatizo tena serious. vyakula vya nyuzinyuzi ni vipi hivyo? je ni kama vile parachichi ama?
 
na hizo dawa za maumivu zisizopaswa kutumiwa je ni pamoja na panadol? cz bila hizo dawa za maumivu kwa kweli hata kukaa ni shida na furaha yote inapotea
 
huo ugonjwa nimeteseka nao sana ila sikutumia dawa yeyote ile ila kula vyakula vilaini na kunywa sana maji
 
pole aisee, ni ugonjwa mbaya nilishaupata ukaa kama miez kadhaa hiv maumivu yakaisha,kukawa na kinyama kisicho na maumivu baadae nacho kikapotea, lkn baada ya mwaka mmoja kilirud tena vikawa vinyama viwil badala ya kimoja na maumivu yakawa makal zaid ya wakati uliopita hata kukaa ilikua ni shida sana.kwaushauri kwasababu nimeshapitia kiti kama hicho nenda hospital kafanyiwe upasuaji kwasababu ni upasuaji mdogo wala usiogope baada ya wiki 1 au wiki 2 maumivu ya upasuaji yatakua yamekwisha kabisa. bora ufanye matibabu vikiisha vyenyewe vitakavorudi vitarud kwa kasi kuliko mwanzo
 
daa asee, hili ni tatizo tena serious. vyakula vya nyuzinyuzi ni vipi hivyo? je ni kama vile parachichi ama?

mchicha hasa vile vishina vyake, ndizi(usitoe vile vinyuzi baada ya ganda)
 
Back
Top Bottom