wakuu heshima kwenu. naombeni kufahamishwa chanzo halisi na tiba ya tatizo la kuota vinyama sehemu ya haja kubwa, Tatizo hili huambatana na maumivu yanayovuta na kuachia kama vile una kidonga au jipu linalotunga usaha kimaumivu. Je kuna dawa ya kutumia pasipo kufanyiwa operesheni na mtu akapona kabisa?? Naombeni msaada kwa kuzingatia mazingira pia ya kitanzania( hofu yangu ni kukomaa kwa tatizo hadi mtu kulazimika kupelekwa ughaibuni), Msaada tafadhali
huo ugonjwa nimeteseka nao sana ila sikutumia dawa yeyote ile ila kula vyakula vilaini na kunywa sana maji
daa asee, hili ni tatizo tena serious. vyakula vya nyuzinyuzi ni vipi hivyo? je ni kama vile parachichi ama?