Kupambana na utekaji, Mahakama itusaidie Wananchi kuandaa arrest guidelines (Miongozo ya Ukamataji)

Kalamu Nzito

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2015
Posts
349
Reaction score
805
Mahakama imekua na utaratibu wa kuandaa Guidelines (Miongozo) kwenye taratibu mbalimbali za kisheria.

Mathalani mpaka sasa kuna guidelines kama;
1. Bail Guidelines (2020)
2. Execution Guidelines (2020)
3. The Tanzania Sentencing Guidelines (2023)
4. Exhibit Management Guidelines(2020)

Hii ni baadhi tu ya miongozo. Kwamba, japo taratibu zipo ndani ya sheria husika, Mahakama iliona ni vyema kudadavua taratibu hizo ili kuepusha mkanganyiko.

Nashauri sasa Mahakama ituletee ARREST GUIDELINES (Miongozi ya ukamataji) Taratibu za ukamataji wa washukiwa wa uhalifu zidadavuliwe na ziwekwe sawa ili tujue kutofautisha kati ya Utekaji na ukamatwaji unaofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama.

Ikumbukwe kuwa kanuni moja wapo ya haki inaeleza kuwa, ni bora kuwaachia watu mia wenye hatia, kuliko kumfunga mmoja asiye na hatia.

Kwa namna hii tutakomesha matukio ya utekaji yanayofanywa na Askari waliokosa weledi na wanaotumika kisiasa.
 
Mhimili wa mahakama ni dhaifu mno, unafanya KAZI kwa kufuata amri kutoka ccm, na ccm ndio adui yetu mkubwa, kwani dhuluma hii ya uhai hufanywa na wao.
 
Na hiyo miongozo itolewe na kwa kiswahili jamani.

Kinge ni shida plus lugha ya mahakama sasa nayo ngumu unaweza rudia sentensi mara tatu kapaa basi unageuza karatasi tu huku na huku unaweka kando.
 
Kwa kweli mkuu,huu ni udhaifu sana .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…