Kupambana na watu wasiojulikana: Ukija kukamatwa na polisi bila uniform na hajaambatana na kiongozi wa eneo husika piga firimbi, kusanya nzi

Kupambana na watu wasiojulikana: Ukija kukamatwa na polisi bila uniform na hajaambatana na kiongozi wa eneo husika piga firimbi, kusanya nzi

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu kwema,

Watu wasiyojulikana siyo maneno mageni kwetu, na mambo haya yameanza kitambo kuanzia enzi za Kikwete na Ulimboka (kusoma tukio hilo zaidi hasa kwa Gen Z soma hapa - Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana aliyetekwa na watu wasiyojulikana na kukukwa ametupwa kwenye msitu akiwa ameteswa sana na kung'olewa meno.

ulimboka.jpg

Kadri awamu zilivyobadilika na ndivyo matukio haya yamezidi kuongezeka, na sasa wamekuja na mbinu mpya.

Wanakuja watu wanaojitambulisha kama polisi na kutaka kukukamata, lakini wanakuwa wamevalia kiraia yaani hawana gwanda za polisi, watakuonesha kitambulisho (lakini hivi hata vya mchongo vinapatikana), wakiwa pia na gari binafsi, nyingi ambazo zimekuwa zikihusika ni Noa nyeupe au nyeusi, au zile Cruza, lakini pia jamaa huibuka wenyewe wenyewe tu bila kiongozi wa husika.

Kuelewa zaidi haki yako pale polisi anapokuja kukukamata soma: Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Mfano wanakuja mtaani kwako lakini mjumbe wa eneo husika hana taarifa, au anafika sokoni lakini hawaambatani na uongozi wa soko.

Polisi wakishutumiwa kuhusika na matukio haya wanakana, kwamba waliofanya matukio hayo siyo polisi, wanauliza uongozi wa eneo hilo ulikuwepo? Walikuwa na uniform? Walitoa vitambulisho? Walikuja na gari ya polisi?

Ukiangalia ni kweli sababu hawaendi na utambulisho wowote kuwa wale ni polisi, ni tobo (loophole) tunalotakiwa kuliziba, huku polisi wakitoa matamko polisi akija kwa namna hiyo (bila utambulisho official) basi mtuhumiwa anatakiwa kukataa kukamatwa!

Pia soma: Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana

Hapa kwenye kukataa kukamatwa ndio kunaleta ka ugumu, maana tuambiane ukweli kuwadindishia wajeda labda na wewe mwenyewe uwe na msuli, vinginevyo unapigwa makofi mawili, unashikwa kwenye pindo ya suruali huyo ndio umeenda hivyo.

TUFANYAJE SASA KUKABILIANA NA HAWA JAMAA WANAOITWA WATU WASIYOJULIKANA?

Bila wananchi kushirikiana hatuwezi kushinda hili, inabidi tuwe na umoja kama tunavyoshadadia mambo ya kijinga.

Kwenye maandamano yanayoendelea Kenya ili mwandamaji aepuke kukamatwa ovyo walikuwa wanatembea na firimbi, akiona ameshindwa anaichomoa fastaa anaipuliza wenzake wanajaa kuhoji kuna nini, tuitumie njia njia hii.

~ Ukiona watu wanaojitambulisha kama polisi hawajavaa uniform zao, wana gari private na wakati mwingine hakuna plate number, na wala hawajaambatana na uongozi wa mtaa/eneo husika wanang'ang'ana kukuchukua usiende kizembe, puliza firimbi yako, puliza kwa nguvu zako zote kushutua watu wajae.

- Huna filimbi siyo kesi, piga kelele, yaani PIGA KELELE kwa nguvu zako zote mpaka watu wajae, hapa na wewe usiwe mzembe, sema hawa wanadai ni polisi lakini hawana uthibitisho kuwa wao ni polisi.

- Tutumie simu zetu vizuri, wakati jamaa aliyeshikwa anapayuka na kelele zake, wengine rekodini kila kitu, tupate sura zao, pamoja na usafiri waliokuja nao. Namba halisi ya gari huwa inaandikwa kwenye kioo cha gari pale mbele upande wa dereva kama sijakosea, maana kuna uwezekano mkubwa plate iliyotumika ni fake chukueni video na ya namba hizo. Wengine mko vizuri kwenye utaalamu wa mitandao ya kijamii, badala ya kurekodi kwenye simu yako ingia kwenye mtandao wowote wa kijamii na urushe tukio hilo live, amini nakwambia ni dk 0 tu litakuwa limeshasambaa nchi nzima na hao jamaa hawatochomoka.

- Wakati hayo yanaendelea wahojini watu hao ni kina nani na wanatoka wapi, kwa kiasi kikubwa ili kuua soo wataingia kwenye gari na kusepa ili wasitambulike zaidi, ikiwa watatoa silaha, ni muhimu kujilinda, wakifanikiwa kuondoka na jamaa walau tutakuwa na utambulisho wao wote kuanzia sura mpaka namba kamili za usajili.

Kufanya hivi itakuwa rahisi kuwatambua watu hawa wanaotekeleza matukio hayo, na tukiwabaini ni polisi, Jeshi la Polisi litatueleza vizuri kwanini wanashiriki kwenye mauaji ya raia.

Kama nilichokiweka kina manufaa sambaza ujumbe kwa ndugu na jamaa tushirikiane kukomesha watu hawa wasiyojulikana.
 
Hatujaona uwajibishaji wa hao watekaji kikamilifu, ni kama bado wanakingiwa kifua. At least Leo nimesoma taarifa ya polisi 6 wako mahakamani kwa tuhuma za mauaji.

Imagine kama viongozi wakuu wanasema ni "drama " tu, kwa staili hiyo wanaendelea kufanya uovu.

KAULI MOJA TU KUTOKA KWA VIONGOZI WAKUU, PAMOJA NA KUWAWAJIBISHA IPASAVYO WASHIRIKI WA MATUKIO HAYO! Vinginevyo tutaendelea kulalamika tu
 
Uwoga ni matokeo ya utaeala dhalimu wa CCM
When mtanzania ataamka kutoka usingizi na kuondokana na uoga waliokaririshwa?
Maybe ni ccm, but kama raia wamefanya nn kuondokana na hiyo hali?

Uoga kuhoji, uoga kudhubutu, uoga kudai haki , uoga kutambua haki zako?
Why?
 
Hiyo mbinu yako inaweza kufanya kazi endapo tu watakuja mchana kweupe au hata usiku ktk halaiki ya watu lakini mazingira tofauti na hayo ni ngumu hata kupiga yowe/filimbi.

Wakija nyumbani kwako either kwa kuvunja mlango au kwa kubisha hodi au wakikuta sehemu tulivu huku wamekushikia mtutu wa bunduki hautakua na hiyo nguvu ya kupiga yowe, zaidi watakuambia ingia ndani ya gari kabla hatujakumwaga mavi muda huo huna nguvu ya kowahoji hapo ni kutii amri yao tu.

Labda utupe mbinu wakikukuta upo nyumbani pekeyako au na mumewako/mkewako na watoto kipi cha kufanya.
 
Hiyo mbinu yako inaweza kufanya kazi endapo tu watakuja mchana kweupe au hata usiku ktk halaiki ya watu lakini mazingira tofauti na hayo ni ngumu hata kupiga yowe/filimbi.

Wakija nyumbani kwako either kwa kuvunja mlango au kwa kubisha hodi au wakikuta sehemu tulivu huku wamekushikia mtutu wa bunduki hautakua na hiyo nguvu ya kupiga yowe, zaidi watakuambia ingia ndani ya gari kabla hatujakumwaga mavi muda huo huna nguvu ya kowahoji hapo ni kutii amri yao tu.

Labda utupe mbinu wakikukuta upo nyumbani pekeyako au na mumewako/mkewako na watoto kipi cha kufanya.
Utaoga mateke ya kutosha, kimsingi tuna jeshi la kijinga haswa bora hata ya majambazi
 
Back
Top Bottom