Kupanda bei mafuta ya kupikia hadi kufikia tsh7,000 hadi 7,500 kwa lita Serikali iingilie kati

Kupanda bei mafuta ya kupikia hadi kufikia tsh7,000 hadi 7,500 kwa lita Serikali iingilie kati

Mamaya

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
5,067
Reaction score
4,434
Habari ya weekend wana bodi

Natumaini Waziri mwenye dhamana pamoja na serikali huwa wanapita humu JF,

Hoja yangu ni juu ya kupanda bei kwa mafuta ya kupikia kila siku iitwapo leo. Mafuta ya alizeti lita moja ilikuwa inauzwa 3,000-3,500 ila kwa sasa imefikia 7,000 hadi 7,500 kwa lita, mafuta ya kawaida yaliyozoelekea kwa jina mafuta ya korie, lita moja imefika sh 6,000 hadi 6,500 kwa lita tofauti na awali yalikuwa sh 2,500-2,800

Je jambo hili Serikali hailioni? Waziri wa kilimo,Waziri wa viwanda na biashara hawaoni mfumuko huu wa bei unaathiri wananchi? Huu ni mwezi januari, ndio kwanza wakulima wa alizeti wanapanda, mpaka ije kufikia Mei au Juni bei si itakuwa imefika tsh.10,000 kwa lita?

Je serikali haiwezi kufanya jambo kama inavyofanya kwenye sukari kwa kuagiza nje? Au wanasubiri wananchi waendelee kuteseka? Au wachuuzi wameficha mafuta kama sukari? Serikali haitaki wanachi wale kiepe yai? Au tule vya kuchemsha tu kumwenzi Prof Janabi?
 
Bashe ananufaikaje na kuongezeka ugumu wa maisha?
Anayeweza kunufaika ni mfanyabiashara yule wa bei ya jumla, hawa wadogo uwezo wa kununua unapungua (demand and supply theory)
 
Back
Top Bottom