Pole , unadhani walioanzisha hawatambui hizo changamoto zote, Cha msingi timiza wajibu mkuu.Wasalaam ndugu zangu jukwaa la elimu
Kumekuwa na taarifa kuwa waalimu watakaopanda vyeo KIGEZO CHA asilimia za ujazaji wa e utendaji.
Hiki KIGEZO kitawanyima walimu wengi haki Yao ya msingi kwasababu zifuatazo.
1. Uelewa mdogo wa mfumo
Tangu serikali iunde mfumo huu ni watumishi wachache sana walipewa semina namna ya kutumia na wengi wao hawana uelewa wowote kuhusu mfumo huo.
2. Ugeni wa mfumo Kwa wakuu wa shule
Mfumo wa pepmis unahusisha pia mkuu kuweka performance indicator.. ambazo hizi sasa zitatengeneza total score. Kwa hiyo hizi zikisetiwa vibaya mwalimu hata upandishe vipi taarifa zako kwenye mfumo hiyo total score inakuwa ndogo.
3. Matatizo ya kimfumo
Wakati mwengine mfumo unasumbua hasa kwenye maeneo yenye shida ya kimtandao. Pia unaweza jaza asilimia mia ila report ya mfumo inaonesha asilimia chache kuliko zile ulizoweka. Nani wa kulaumiwa? Changamoto
4. Matatizo ya mtandao
Hapa Tanzania yapo maeneo network ni ya shida sana na walimu wapo huko
5. Uelewa mdogo wa maswala ya mtandao
Kwahakika hapa Tanzania Kuna watumishi ni paper based. Hivi vitu vya mfumo wanahitaji mazoezi ya muda mrefu sana.
6. Kutokujua athari kabla
Swala la kufikisha asilimia 75 za upande daraja walimu wengi wameona kwenye waraka wa mwaka huu. Ukijumlisha na ugeni wa mfumo kwakweli hurima inahitajija Kwa mwaka huu
7. Taarifa zq mfumo hazithibitishi utendaji
Ni kweli tunatakiwa kuripotia kwenye mfumo kila tunachofanya. Lakini wapo wengi wanajituma na kazi wabazofanya zinaonekana ila tu walisahau au walishindwa kuripotia. Huruma inahitajika
8. Mkuu kushindwa kuzifanyia kazi taarifa za mfumo
Kuna baadhi ya walimu wameripotia taarifa zao vizuri ila unakuta mkuu wake ndio ameshindwa kuzifanyia kazi ila inakula Kwa mwalimu
Changamoto ni nyingi siwezi andika zote.. naomba tu vyombo vya habari zipaze sauti walimu wahurumiwe.. MFUMO NI MPYA
NAWASILISHA
Sijalaumu,Acha lawama ndugu yangu ,kama ni mfumo unajza kila wiki siku moja , inakuwaje ukose 75% kwa mwaka nzima ? Labda itokee mkuu wako hajaaprove na kakufanyia roho mbaya.
Unazungumzia tu Pepmis sisi wengine mifumo mikubwa hata seminar ya siku moja hatujapewa zaidi ya kudownload Manual na kusoma ili kujua...Labda useme hamna vitendea kazi ila hata simu unaweza kujaza ... Kingine hata kusimamizi wako awe anajua kwamba leo iko hivi kwa sababu wengine ni wavivu labda chini yake kuna watu zaidi ya 10 anawasimamia so sio rahisi akuapprove kwa wote.
Sasa Wewe hata mwaka haujaisha ushafika 100% labda kwa baadhi ya Task ,pale unajzaa hata 3 kwa kila wiki inategemea na uzito wa kazi yako...ikitokea uko chini ya hapo unaweza ku'appeal.Sijalaumu,
Unajaza progressive report.. na unaweka percentage za performance, mkuu ana approve.. unaona progression zinapanda na tulijaza mpaka 100.
Ila mfumo umeweka 88 kama progressive percentage na 62 kama total score. Sasa ilitakiwa nifanye nini ambacho sijafanya?
Na pia elewa idadi ya walimu na level zao za uelewa., huwezi linganisha na kada zenye watu wachache wanaoweza kujifunza Kwa manual guide.
Hivi unayajua mazingira ya walimu wote tz.. nasemea wengi pia
Progress percentage Ikiwa 100 = Total score ya 70.Nafikir pia tunahitaji elimu ya namna pepmis invyo calculate score
Huo ndio uongo mwenyewe,100% umeipataje kabla ya June,30,2025?Kama nimejaza progression mpaka 100%
Unataka nitimize wajibu Gani mwengine?
Umenielewa vizuri SanaaVip mnapata communication allowance ili mnunue vocha mpate mb za kutosha kujaza hizi taarifa kila wiki/siku/mwezi?? Kingine huu mfumo si mgumu sana kama mazingira na seminar za mara kwa mara zingefanyika kuwajengea watumishi uelewa wa hii mifumo..NB watumishi wengi hasa waalimu mifumo mingi ya computer mfano mdogo microsoft Excell kwao ni kipengele