SoC01 Kupanda kwa Bei za Miamala ya Mitandao ya Simu ni "BANK ECONOMIC STRATEGIES"

SoC01 Kupanda kwa Bei za Miamala ya Mitandao ya Simu ni "BANK ECONOMIC STRATEGIES"

Stories of Change - 2021 Competition

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
11,622
Reaction score
26,005
Nawasalimia kwa Jina La JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Kabla ya yote mimi si Mjuzi sana wa mambo ya Uchumi au siasa ya uchumi ila kwa kuwa nimepata ushauri kwa wasomi wa uchumi na mambo haya ya siasa ya uchumi ningependa niwamegee kidogo kuhusu mambo nikiyoelekezwa kuhusu Trending marks iitwayo "UPANDISHWAJI WA BEI ZA MIAMALA YA SIMU" (Kama utaona mapungufu naomba marekebisho).

Kwa rejea nzuri naomba soma Luka 1:1-4 (kwa niliyoongea hapo juu) kwa wale watu wa Dini lakini...

Tuendeleee....


Kwanza ningependa turejee Tafiti mbalimbali zilizo jikita katika kuangalia uhai wa mabenki hasa COBAT,BOT na World Bank (Rejea tafiti mbalimbali kutoka COBAT "wadau wa jumuia ya mabenki ya wananchi")

Mwaka 2017 Serikali kupitia Gavana mkuu wa serikali ilifungia mabenki matano ikiwemo Mbinga Community Bank PLC ikiwa ni kwa kuwa na upungufu mkubwa wa mtaji,Na usalama wa sekta ya fedha na amana za wateja..,Na baadae kutoa onyo kwa mabenki mengine MATATU...

Kabla ya hayo yote naomba kuwapeleka darasani kidogo kuhusu somo la mtaji wa kibenki (Banking capital) ili tuelewe wanaposema mabenki yameishiwa mtaji maana yake nini?


Mtaji wa kibenki(banking capital):-

Mtaji wa kibenki ni tofauti ipatikanayo kati ya miliki za benki (banki assets) na dhamana au dhima ya benki husika (bank liabilities).

Kwa lugha ya wenzetu ningesema;- Banking capital is the different between bank assets and bank liabilities

Bank assets au Milki za benki ni zile shughuri zote za kifedha ambazo benki inazifanya kujiingizia kipato au kile kiasi cha mikopo iliyotolewa na benki kwa serikali u mashirika mengine na vingine vinavyofanana na hivyo.

Mfano mwingine wa assets za benki ni CASH yaani fedha zipatikanazo kutoka kwa watu... yaani chukulia wewe umeemda kuweka pesa banki hiyo kwao inakuwa ni assets yaani mali inazomiliki au wewe umekopa pesa banki hiyo inakuwa ni mali miliki ya benki. Wenyewe wanazitenga kweye solid assets (eg account) na liquid assets (cash).

Na Bank liabilities ni zile dhamana benki iliyonazo kwa mfano Kodi malipo mbalimbali,TRA , malipo ya jengo malipo ya mishahara na mikopo mbalimbali ambayo benki inaweza ikawa imeingia kwa uendeshaji...

Nafikiri kwa hapo juu tutakuwa tumeelewana saana sasa twende tuingia kidogo mwanzo wa mada kabla sijatoa maelezo.

Kutokana na kuzidi kwa gharama za uendeshaji wa benki nyingi ikiwemo malipo ya kodi kuwa makubwa na gharama nyingi ambazo zingine zitazielezea imefanya mabenki mengi kuwa na liabilities nyingi sana wakati huohuo assets kubaki kama zilivyo au kupungua kabisa.. Hivyo kusababisha mashirila mengi ya kibenki kuingia hasara kuliko faida wanayopata.

JINSI BENKI INAVYOWEZA KUFANYA KUONGEZA KIPATO NA KUONGEZA UCHUMI

Benki hukusanya fedha zilizohifadhiwa (bank assets) yaani kutoka kwenye account mbalimbali na kuwakopesha wafanyabiashara,wahisani, Viwanda na hataa serikali kwa riba maalumu ambayo nayo huchangia mzunguko wa pesa ili kurahisisha biashara kuendelea.kwahyo serikali hupata pia pesa kutoka na Income tax inayotokana na benki.

MASHIRIKA YA SIMU YAMECHANGIAJE KUSHUSHA THAMANI YA BENKI(KUPUNGUZA MITAJI YA MABENKI)?

Ni swali ambalo wengi wanajiuliza sana ila nitajatibu kulijibu kutumia maelezo niliyotoa hapo awali.

Jamii nyingi ya kitanzania imeona vyema kuhifadhi pesa kwa njia ya simu ili kwanza kurahisisha miamala ya kifedha ,pili kupunguza makato mengi na kutuma na kupokea pesa tatu urahisi wa kupata huduma hizo za benki za simu (sitazitaja lakini hizi huduma za pesa kwenye simu)

Kwani mara nyingi mtu anaweza kuweka pesa kwenye simu bila kupata makato ya uendesheji ya kila mwezi au pesa ya ATM au mengine yanayofanana na hayo hivyo..kufanya wimbi kubwa la watu kuhamia katika huduma hizi za simu.

Na kuacha huduma za Banki ambazo zimekuwa na makato makubwa ya kiuendeshaji....Watu wengi kuacha kufanya miamala ya kibenki na kuanza kufanya miamala katika mashirika ya simu,Kumepunguza wateja wengi kujiunga au kuendelea kutumia huduma za kibenki hivyo kufanya huduma hizo kushuka kidogo (kwani assets imeshuka au kubaki constant while liabilities kuzidi kupanda).

Kutetereka kwa assets kumefanya benki nyingi kushindwa kujiendesha na nyingine kufilisika.

KUPANDA KWA MIAMALA YA SIMU NI BENKI ECONOMIC STRATEGIES

Sasa kwakuwa serikali ilikuwa ikipata pesa kwa ajili ya kutekeleza ama bajeti au baadhi ya miradi imekuja na hii strategies ili kupata tozo ya miamala moja kwa moja kutoka katika mitandao ya simu hii itarudisha aidha uhai wa benki kwani watu wataona bora waweze kuweka pesa benki kuliko kwenye mitandao ya simu au serikali itapata pesa moja kwa moja na kuongeza pato la uchumi wetu ...kwahiyo Kwa asilimia fulani naona uhainwa Baadhi ya benki ukirudi kwani tozo za Benki bado zipo chini ukilinganisha na tozo za simu..

Yaliyoandikwa juu ni mawazo yangu na ningependa mwenye mawazo makubwa kuliko mimi anisahihishe

Asante

Dr Mambosasa Asante
 
Upvote 8
Kufanya hivyo hakutawabadilisha au kuwashawishi watu waweke au watumie huduma za benki kama mbadala wa mobile money.
Cha muhimu ni sera za sera bora za kiuchumi na kisiasa. Mfano mzuri ni yaliyowakuta watu wa bureau de change na fedha za watu kutekwa benki. Aliyepatwa na madhila kama hayo hawezi tena kuamini kutumia huduma za kibenki.
 
Upo sawa kabisa,ni kweli watumiaji wengi wa miamala ya simu watarudi kwenye kutumia mabenki kutuma na kupokea fedha zao. Kunauwezekano mkubwa mabenki yamefanya lobbying kea kuishawishi serikali iweke kodi kwenye miamala,ili kuimarisha uhai wa hayo mabenki,hilo linawezekana kabisa kufanyika hasa kwenye uchumi ambao upo kwenye mfumo wa capitalist (ubepari) mambo mengi huwa yanafanyika nyuma ya pazia ilikunufaisha vyombo vyenye nguvu.
 
Upo sawa kabisa,ni kweli watumiaji wengi wa miamala ya simu watarudi kwenye kutumia mabenki kutuma na kupokea fedha zao. Kunauwezekano mkubwa mabenki yamefanya lobbying kea kuishawishi serikali iweke kodi kwenye miamala,ili kuimarisha uhai wa hayo mabenki,hilo linawezekana kabisa kufanyika hasa kwenye uchumi ambao upo kwenye mfumo wa capitalist (ubepari) mambo mengi huwa yanafanyika nyuma ya pazia ilikunufaisha vyombo vyenye nguvu.
 
Kwahiyo sasa hivi kila upupu munauweka kwenye hili shindano la Melo
 
Kufanya hivyo hakutawabadilisha au kuwashawishi watu waweke au watumie huduma za benki kama mbadala wa mobile money.
Cha muhimu ni sera za sera bora za kiuchumi na kisiasa. Mfano mzuri ni yaliyowakuta watu wa bureau de change na fedha za watu kutekwa benki. Aliyepatwa na madhila kama hayo hawezi tena kuamini kutumia huduma za kibenki.
Sure hili litabadilisha saaana
 
Huu ni ukweli ambao wengi wanashindwa kuuamini
Upo sawa kabisa,ni kweli watumiaji wengi wa miamala ya simu watarudi kwenye kutumia mabenki kutuma na kupokea fedha zao. Kunauwezekano mkubwa mabenki yamefanya lobbying kea kuishawishi serikali iweke kodi kwenye miamala,ili kuimarisha uhai wa hayo mabenki,hilo linawezekana kabisa kufanyika hasa kwenye uchumi ambao upo kwenye mfumo wa capitalist (ubepari) mambo mengi huwa yanafanyika nyuma ya pazia ilikunufaisha vyombo vyenye nguvu
 
Inafikirisha kidogo, mimi siungani moja kwa moja na wewe. Sidhani kama hii imetumika kama strategy ya kuyainua mabenki yapate faida ili yajiendeshe.

Kwanza benki zinapata faida kupitia mikopo na uwekezaji wa bank husika nje na pia kwenye miamala anayofanya mteja (hii ya mwisho haiingizii benki faida kubwa kama hizo mbili za mwanzo) . Hizi tozo nadhani ni kama serikali ilivosema inawezekana serikalini pesa hakuna na sehemu ya haraka kupata pesa ni pale ambapo wananchi wanatumia sana. Na hapo ni kweny hii miamala ya simu.

Lakini pia benki hazijateteleka kwa kiasi hicho kwasababu shughuli za kibenki na mitandao ya simu zina muingiliano mkubwa, kuathirika kwa mitandao ya simu na benki pia inaathirika kwa namna moja ama nyingine.
 
"Lakini pia benki hazijateteleka kwa kiasi hicho"
Ningependa urejee hotuba zifuatazo kama unaweza kuzirudia
1.Hotuba ya aliyekuwa waziri wa fedha Dk Philipo mpango hutuba ya tarehe 12/05/2017 akizungumzia kuhusu ufanisi na ustawi wa kibenki Tanzania (aliongea kwa niaba ya waziri mkuu)

2.Hotuba ya Aliyekuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Hayati JPM hotuba ya Tarehe 11/05/2017 alipokuwa anafungua tawi la CRDB jijini DODOMA

3.Kauli ya waziri mkuu mwaka 2017 kuhusu BOT kufungia mabenki yamayoteteleka kibiashara
Naomba ukipata muda zitafute hizo hotuba kama huna nitafute ntakupa
 
Back
Top Bottom