Kupanda kwa bei za vitu kunasababishwa na nini?

Kupanda kwa bei za vitu kunasababishwa na nini?

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2018
Posts
439
Reaction score
742
Kwa siku za karibuni mtaani tumeshuhudia kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali kuanzia pembejeo za kilimo (mbolea), sukari, mafuta ya kupikia, mafuta ya vyombo vya moto kwa maana ya dizeli na petroli, gesi majumbani pamoja na bidhaa za vyakula.

Je, sababu ni nini? Siasa au?
 
Sababu ni Serikali ya CCM! Imeshindwa kusimamia maslahi ya wananchi. Na badala yake imewaacha wafanyabiashara wasio waaminifu, wafanye wanavyotaka.
 
Sababu ni katiba mpya.Ikipatikana tu katiba mpya bei za vitu na huduma zote zitashuka sana sawa na bure.
Sarcasm .Take it with a pinch of salt or with a face value.
 
Duniani kote ni hivyo Mkuu
Bei zimepanda kwa kila kitu
Tena huko afadhali wengine mpaka PAYE tax inaongezeka na kodi zingine pia
Chakula na hata fuel vimepanda siku nyingi

Hali ni ngumu duniani, tena bahati wazungu wameomba suluhu na Putin la sivyo tungekoma
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Sababu ni Serikali ya CCM! Imeshindwa kusimamia maslahi ya wananchi. Na badala yake imewaacha wafanyabiashara wasio waaminifu, wafanye wanavyotaka.
Kwani bado unauza pears zako kwa bei ya 2019?
Inflation ni tatizo la dunia nzima.
 
Sababu ni Serikali ya CCM! Imeshindwa kusimamia maslahi ya wananchi. Na badala yake imewaacha wafanyabiashara wasio waaminifu, wafanye wanavyotaka.

Siungi mkono suala la serikali kuoanga bei elekezi kwa kitu
Vingine iache tu soko liamue
 
Back
Top Bottom