Kupanda kwa Gharama za Manunuzi ya Mahindi na Unga ni Shangwe kwa Wanafunzi wa Bweni.

Bernard bakari

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2016
Posts
407
Reaction score
781
Nakumbika sana wakati nasoma kidato cha tano na sita nikiwa naishi kwa mara ya kwanza bwenini. Tulikuwa tunakula ugalo na maharage Jumatatu, jumanne, Alhamis, Ijumaa na Jumapili. Siku ya Jumatano na Jumamosi ni siku ya kula Wali.

Siku hizo za kula wali lazima kidogo ugomvi utatokea kati ya mgawaji na baadhi ya wanafunzi na kati ya wanafunzi na wanafunzi. Tulikuwa tunajitahisi tupate wali mwingi ili japo kibaki kiporo cha kesho asubuhi mambo ya bwenini hayo, siku hiyo kwetu ndo siku bora katika maisha ya shuleni kwetu.

Lakini katika utawala huu wa awamu ya Tano maisha yamebadilika shule nyingi za bweni wameonekana kufululiza kula wali badala ya ugali hii kutokana na gharama ya unga kuwa juu ukilinganisha na mchele. Wanafunzi wengi huwa hawapendi ugali sasa kutokana na mabadiliko haya imekuwa Neema kwao hata wazazi ile mizinga imepungua kwa kiwango kikubwa.

Kweli kila jambo linafaida na Hasara yake wakati wananchi tulio wengi hapa nchini tukilalamikia kupanda kwa gharama za unga wanafunzi wa shule nyingi za bweni ni Neema na furaha kwao.

Watanzania wenzangu tuungane na wanafunzi wa bweni tukimbilie wali unga utatufilisi hii nchi kwa sasa haitazami vitu vya lazima vya binadamu na kuhakikisha bei zao zinakuwa katika uangalizi wa Taifa matokeo yake kila ukiamka unga unapanda bei sukari ndo usiseme. Kula lazima lakini siyo Lazima kula Ugali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…