Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Ripoti ya “Viashiria vya Nguvu Laini Duniani Mwaka 2025” imetolewa hivi karibuni huko London, Uingereza, na nafasi ya China imepanda hadi pili duniani. Hii ni mara nyingine ya kupanda kwa nafasi hiyo ya China, baada ya kupanda kutoka nafasi ya tano hadi nafasi ya tatu mwaka jana. Nafasi hii inaonesha kuendelea kukua kwa ushawishi wa kimataifa wa China.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa China imepata ukuaji mkubwa katika nyanja sita kati ya nane za nguvu laini, hasa katika nyanja tatu kuu za utamaduni na urithi, biashara, na elimu na sayansi.
Tangu mwaka 2020, China imeshika nafasi ya kwanza duniani katika viashiria vya “urahisi wa kufanya biashara” na “uwezo wa maendeleo katika siku zijazo”, na nafasi yake ya “uongozi wa teknolojia na uvumbuzi” imepita Marekani, na kushika nafasi ya pili duniani.
“Kiini cha nguvu laini ni mvuto, sio kulazimishwa.” Ripoti hiyo inasema China inaendelea kupendwa na kuaminiwa na jumuiya ya kimataifa kupitia usikivu wa kitamaduni, mafanikio ya kiuchumi na utoaji wa teknolojia.
Nguvu laini ya nchi inajikita katika maelewano ya utamaduni na maafikiano ya thamani. Ustaarabu ulioendelea kwa maelfu ya miaka umetoa msingi mkubwa kwa nguvu laini ya China. Katika miaka ya hivi karibuni, vitu vingi vya utamaduni wa China, kama vile Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, majira 24 ya jua, Tai Chi, na ujuzi wa kitamaduni wa kutengeneza chai, vimejumuishwa katika Orodha ya Wakilishi ya Turathi za Kitamaduni Zisizoshikika za Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), filamu ya “Ne Zha II” inaongoza katika historia ya filamu duniani, mitandao ya kijamii kama vile TikTok na Xiaohongshu imekuwa madirisha mapya ya kueneza utamaduni wa China.
Nguvu laini haiwezi kutenganishwa na nguvu halisi. China imeshika nafasi ya pili duniani kwa ukubwa wa uchumi kwa miaka mingi, na kuendelea kuchangia ukuaji wa uchumi wa duniani kwa zaidi ya asilimia 30 kwa miaka mfululizo.
Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” limevutia uwekezaji wa karibu dola trilioni moja za kimarekani katika muongo uliopita, na kuzisaidia nchi zinazohusika kuongeza ajira zaidi ya laki 4.2. Bidhaa za teknolojia za juu za China zikiwemo magari ya nishati safi, teknolojia ya 5G, na vifaa vya umeme zinakaribishwa katika soko la kimataifa.
Kutoka “kufuata” hadi “kwenda sambamba” na nchi zilizoendelea, ongezeko la nguvu laini ya China halitokani na bahati nzuri, bali linasababishwa na juhudi kubwa za China katika kuhimiza ushirikiano na kuwajibika.
Katika mwanzo mpya wa kuwa nchi ya pili duniani kwa nguvu laini, China itaendelea kuchangia hekima yake kwa jamii ya kimataifa.