kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Inafahamika wazi kuwa kama utapandisha bei ya mafuta utapandisha pia bei zote za vitu vyote kwa wakati mmoja, na gharama yote itakwenda kwa mwananchi wa kawaida anaetumia huduma.
Wananchi wa vijijini wanategemea watoto na ndugu zao walioko mijini (machinga) kutumiwa pesa kwa simu ili waweze kupata mahitaji muhimu ambayo kwa bahati mbaya yamepanda bei kutokana na upandishwaji huo wa bei ya mafuta.
Miamala ya simu inawahusu wanakijiji moja kwa moja. Sasa unapopandisha tozo za kutuma na kutoa hela kutoka kwenye simu maana yake ni sawa na kumfanya mwananchi asonye mara mbili, kupanda kwa mafuta na kupanda tozo ya kutolea kijisenti chache. Na mara nyingi anausonya utawala.
Inafahamika pia kuwa hii pesa wanayotumiwa kwenye simu wakishaipata mbali ya kutozwa tozo kubwa lakini pia wataipeleka kwenye manunuzi ya bidhaa ambazo pia zina kodi, VAT. Hivyo, huyu mwananchi analipa kodi nyingi sana kwa wakati mmoja ambazo zinapunguza uwezo wake wa manunuzi (purchasing power), wakati huohuo hawana uhakika wa kupata huduma za dawa kwenye zahanati, maji, umeme, ada za watoto, bweni, nk. Wanalazimika kwenda kununua dawa na maji mitaani.
Ongezeko la tozo kwenye miamala, mafuta na umeme ghafla kwenye awamu ya Sita huenda ikawa hujuma kwa mama ili alaumiwe na wananchi. Sio kweli kuwa waziri na wabunge hawajui kuwa kupandisha bei ya mafuta, miamala na umeme (kodi ya majengo) vinaenda kuzalisha mtafaluku kwa wananchi ambao hawana uhakika wa matibabu, maji, umeme, elimu, wala masoko ya mazao yao.