Pole Kisima...mara nyingi mtu anapokuwa na matatizo ya moyo kupelekea moyo kuwa mkubwa au kutanuka, basi huo moyo huwa unashindwa kufanya kazi 'Heart failure', na mgonjwa anakuwa katika hali mbaya kwani damu haifiki kule inakopaswa kufika. Katika dawa alizopewa ipo 'Digoxin'? Kwani hiyo husaidia moyo unaoshindwa. Na pia dawa za kupunguzia mzigo moyo eg Lasix etc. Kama hapati dawa hizo, basi nashauri nenda kamuone daktari bingwa wa magonjwa ya moyo 'Cardiologist' kwa matibabu zaidi.
Ungeweka kwenye JF Doctor...huku watu wanapeana ushauri jinsi ya kurepair mioyo iliyovunjika!
pole,kama hali ni mbaya na huyo doctor ameshindwa kumtibu kwa nini usijaribu kuwaona wataalam wengine waliobobea zaidi?
Asante Dada Afro na Rose ntashukuru kwa Maombi make ndiyo tiba kuu ninayoitanguliza huku nikisaka matibabu kitaalam.
mungu awabariki sana.