Viongozi wanaohusika kusimamia watumishi wa UMMA jaribuni kuwatendea haki watumishi wenu, kupata barua ya uhamisho kutoka Wizara ya UTUMISHI imekuwa kero sana.
Taratibu za mtumishi kufuata ili kupata uhamisho zinawekwa na wizara lakini bado barua zinachukua zaidi ya miezi Sita (6) kutoka huko Wizarani, mtumishi anaomba kujigharamia uhamisho lakini bado barua yake inachelewa.
Swali: Kuna sababu gani ya kukaa na barua ya uhamisho ya mtumishi ambae amefuata taratibu zote kuanzia kwa mwajiri wake wa sasa hadi anakotaka kuhamia?
Ni kweli kuwa hapo wizarani hakuna kitengo kinachohusika na tathmini kuona ni kwa namna gani mtu anaathirika ki utendaji kazi pindi anaposubiri barua yake ya uhamisho?
Wizara imeanzisha utaratibu wa ESS (Online employees self services) tukidhani kuwa itapunguza urasimu wa uhamisho hapo Wizarani lakini bado shida ipo pale pale.
Kama barua inachukua kipindi cha miezi zaidi ya 6 kwenu nyie PEPMIS mnajazaje?
Badilikeni, mtu anatoka Sumbawanga kufuatilia barua UTUMISHI, Wizara inakuwa kero sasa.