Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Ni bora kupata 1% kutoka kwenye elfu moja kuliko kupata 50% kutoka kwenye 10 (hapo utaona kwenye 1% utapata 10 na kwenye percent 50% utapata 5.
Serikali imeamua kuongeza mapato kupitia miamala ya simu; unless otherwise sababu ni kuziua hizi kampuni za simu ili ushindani urudi kwenye mabenki (jambo ambalo sidhani sababu litakuwa ni kurudi nyuma na kupambana na teknolojia). Hata kama ikiwa ni kweli ndio matarajio yao hii itakuwa ni mpiga ngumi ukuta..., sababu pia ikumbukwe kwamba mteja mkubwa sasa hivi wa mabenki ni hii mitandao ya simu..., hivyo impact ya haya makampuni ni kubwa.
Kama sababu sio kupunguza nguvu za hii mitandao na ni kuongeza mapato nadhani huenda wasipate wanachokusudia au kupunguza ambacho wangepata kama wasingeongeza hizi tozo, yaani ingekuwa bora kama wangezipunguza kuongeza watumiaji na sio kuwapunguza watuamiaji kwa kuwaongezea kero.
Wadau Wakubwa katika miamala ni watatu; Serikali akiwa ni mnufaika tu;
- Makampuni,
- Watumiaji
- Mawakala
Kumbuka hata kabla ya hili ongezeko Serikali ilikuwa inachukua tozo mbalimbali na kila faida aliyokuwa anapata wakala (commission mwisho wa mwezi) serikali ilikuwa inachukua Kodi ya zuio 10% kwahio kwa miamala mingi zaidi ya wakala inayopelekea faida nyingi kwake na Serikali ilikuwa inapata faida nyingi zaidi.
Kwa kuibana kampuni kwa tozo tofauti huenda isilete impact kubwa sana kama wao bado wataendelea kupata faida (na walivyo na economy of scale huenda wakaendelea kupata faida). Ukizingatia ni vigumu kwa hizi kampuni kumbana sana mtumiaji wa mwisho kwa kuhofia kumpoteza.
Kwa kuwabana mawakala huenda bado impact isiwe kubwa sana sababu mtu akiona hio 10% ya zuio hana jinsi kama bado anapata faida (something is better than nothing). Ingawa nao ukiwabana sana wanaweza kuona hii ni biashara kichaa hence kuacha kuchangamkia kutoa hio huduma
Watumiaji
Kwa kuwabana watumiaji direct ni kwamba umewabana wote, yaani makampuni, mawakala na hata serikali kupunguza kupata kile kidogo katika kingi walichokuwa wanapata. Sababu kama mtumiaji akianza kuona kutumia simu kunamgharimu atatumia njia mbadala, wakati miamala ingekuwa gharama zake ni ndogo kuliko usumbufu wa kutumia pesa kila mtu mwisho wa siku angetumia ukizingatia tunakotaka kuelekea ni kwenye Cashless Society (ambayo mwisho wa siku ni faida kwa nchi kwa ujumla kupunguza gharama za ku-maintain currency.
Ushauri Nini Kifanyike
Serikali sio tu kwamba iondoe hizi tozo ilizoleta bali iwashauri hata mitandao wapunguze zaidi na hizo faida wawekeze kwenye elimu na kuhamasisha watu wengi zaidi watumie simu zao katika shughuli zao..., kwa kufanya hivyo Serikali itapata kidogo kutoka kwenye watu wengi zaidi hivyo mwisho wa siku kupata zaidi, ukizingatia ile 10% ya faida ya kila wakala bado wanachukua na wataendelea kuchukua. Kama hilo wakiona pia halifai ni bora kuongeza tozo ya zuio kwa wakala kutoka hio 10% hadi hata 15% au vinginevyo sababu kama wataendelea kupata miamala mingi zaidi ndio faida zaidi kuliko hivi sasa kuna hatari ya biashara zao kupungua kwa watu kutafuta njia mbadala.
Kama wakiona hilo haliwezekani na hii mitandao inapata sana pesa basi sio vibaya wakiwekeza kwenye Kampuni zao ambao wana hisa nyingi Airtel na TTCL ili nao wafanye biashara za kushindana na hizo kampuni nyingine ili wale hizo faida ambazo wanadhani hao wengine wanapata.
Hitimisho
Kwa kumuumiza mtumiaji wa mwisho direct ni kama mkulima anayekula mpaka mbegu za kupanda mwisho wa siku atakosa mazao yote na kufa njaa, Ingawa huenda akashiba kwa siku moja.
Upvote
13